Ndoa Yangu haina mapenzi

Jikaze na huyo huyo mkeo kama vile unakunywa klorokwini! Siku moja mapenzi yatarudi!
 
avatar kuonesha msisitizo kwamba aliyemchoka mwenzie sio mume ni mke.....
@Max duh sijakusoma kihivi longi sana mkubwa!!!
thanks I will keep that in my mind till the time comes!!!
 

kwakweli nakushukuru kwa kusoma ushuri wako nimehisi kupunguza kitu maana umegusa mambo mawili kama sio matatu ambayo nadhani ni chanzo cha kuchoka ila nashukuru umenipa pia mwanga Ahsante sana tena sana mungu akuongoze uwe mshauri mwema
 
Mkuu mapenzi unayajenga mwenyewe, sivyo utaishia kuishi na mkeo kwa mazoea tu! (and this makes most of the holy unions)
 
Naona hujawa muwazi na mkweli. Lazima una sababu au kisa kinacho kufanya umchoke mwenzako hata kama sababu hiyo haina maana sana. Vinginevyo wewe ni UNIQUE duniani. Kama wewe ni mkristo piga magoti umwombe mungu aitoe hiyo pepo ya chuki bila sababu na uendelee kuishi na mkeo maana alichokiunganisha mungu binadamu hawezi kukitenganisha. Kama wewe ni mwisilamu oa mke mwingine ili kuepuka dhambi ya zinaa na pengine HIYO itakupa nafasi ya kugundua kwamba mkeo wa kwanza ni bora na utaendelea naye pia.
 
Mie sikushangai Ngoma zom........
Ila jaribu kumuomba mwenzi wako akupe muda hata wa wezi mmoja ukae peke yako kama likizo au anything .ujaribu kurefresh mind yako hayo ndo maisha ya ndoa yana mambo mengi na majaribu ya kila namna...
Pia nadhani kuna mambo hujasema kuhusiana na mwenza wako
 

ndugu... ndoa siyo kitanda cha mawaridi kisichokuwa na miiba.
Ndoa tunaingia kwa pupa bila kutafakari hasa nini maana ya kuji- commit kwa mtu mmoja kwa maisha yetu yote.Unasema umemchoka mwenzio japo hajakufanyia lolote baya! Hii ni ajabu maana kuchokana kwenye ndoa mara nyingi huletwa na mambo tunayofanyiana ya kuumiza au kukera yenye kujirudiarudia.Huwezi wewe kuamua kumchukia mtu uliyempenda kiasi cha kufunga naye pingu za maisha pasina sababu kubwa ya msingi - sababu inayotikisa mizizi ya uhusiano.Huwezi wewe kumchoka kipenzi chako aliyekuwa anakufanya uzuzuke kila ukimuwaza bila chanzo chochote. Avatar yako inaoonyesha wewe ni mwanamke. Mara nyingi wanawake huwa na commitment ya ajabu sana kwenye ndoa zao.Ukiona mwanamke kaamua kufanya tofauti na alivyoji commit ujue kuna kisa au jambo lenye kugusa moyo zaidi ya kugusa hisia za mwili.
1. jE, uliiingia kwenye ndoa shauri ya kitu - na hicho kitu sasa hakipo?
2. Umeshajiweka kwenye viatu vya mwenzio ukajipima kuona kama ungefanyiwa hivyo wewe ungejisikia vipi?
3. Ndoa yako ina umri wa zaidi ya miaka 5? kama hapana, uliingia kwenye ndoa kwa sababu gani - ulifuata mkumbo?
4. Maisha siyo kujisikia vizuri tu wewe binafsi. Ni pamoja na kujitoa kwa sababu ya furaha ya wengine.Je wewe unajitoa au ni mtu mbinafsi mwenye kujifikiria wewe mwenyewe tu?
5. Unadhani ukibadilisha na kuwa na mwenza mwingine, utaweza kudumu naye au ndio baada ya muda naye utamchoka maana wewe humchokaga mtu hata kama hajakufanyia baya lolote. Mwisho wako utakuwa vipi?
6.Ukitizama umri wako, inaelekea wewe bado ni kijana sana.Je ukiwa na umri mkubwa bado utakuwa na hulka hiyo ya kumchoka mwenzio?...
TAFAKARI...............
 
duh! huyu dada yuko level nyengine, hii ushauri imetulia sana aisee, ushauri kama hii ughaibuni wanalipia bana! senksi kwa kuiweka free.
 
mama signatory yako mbona nzuri sana
ingia kimaombi zaidi utauona muujiza
Ee bwana utete nao wanao teta nami pigana nao wanao pigana nami... Zab 35:1-28🙂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…