Ndoa ya kiislamu: Alimuacha mkewe, anataka nimuoe alafu nimuache amuoe tena

Za jioni wakuu,

Ninahitaji ushauri wenu awdau, na nitaanza na historia kidogo.

Kuna rafiki yangu mmoja tuemshibana sana, ni rafiki yangu wa kufa na kuzikana, mi na yeye ni zaidi ya rafiki na hata kama ni udugu basi huu wetu ni zaidi ya udugu. Jamaa yangu huyu tumejuana toka Sekondari Miaka kama 20 iliyopita, tukaenda wote Chuo pamoja. Kifupi ni kwamba huyu jamaa ni rafiki yangu mno toka miaka hiyo mpaka sasa.

Sasa bwana huyu tukiwa chuo alibahatika kupata mwenza wa maisha mnamo mwaka 2000, binti wa Kimanga, shombe shombe, mtoto mkali, kwao geti kali, getini mbwa mkali na pengine kitandani atakua ni mtamu zaidi ya asali. Binti huyu ni kifaa hasa, ameumbika, si mwembamba lakini pia katika mabinti wanene hayupo, na ukipishana nae lazima utageuka tu kumuangalia taka usitake. Yaani kifupi huyu binti pale chuo alikua ndio kifaa, na hata Jamaa kumpata ilikua kama zali hivi.

Jamaa baada ya kumuoa huyo binti bana maisha yakasonga, miaka hiyo ndoa ina furaha tu haina migogoro, shida imeanza mwaka jana, shetani kaingilia kati, kila siku ugomvi mwishowe mwaka jana mwezi wa saba wakaachana kabisa kwa talaka. Cha ajabu baada ya talaka ndio wakagundua kua wanapendana sana na hawawezi kukaa bila kuonana hivyo wanahitaji kurudiana na kua pamoja kama zamani.

Sasa kwa mujibu wa ndoa za Kiislamu, mkishaachana kwa talaka, ili mje mrudiane tena inabidi mke aolewe kwanza na mtu mwengine kisha aachike ndio umuoe tena. Mshikaji wangu huyu kafikiria wee, kaja na jibu kua atafute mtu akubaliane nae kua amuoe ex-wife wake kisha aachane nae ndio yeye amrudie, na mtu mwenyewe aliemchagua wa kumuoa ex-wife wake ni MIMI. Ukweli mmoja ni kua mimi ni mmoja kati ya waliokua wakimfukuzia huyu Binti kabla hata ya mshikaji wangu hakumpata miaka hiyo chuo, na miaka yote hiyo nimekua katika wakati mguu sana kila nimuonapo huyu shemeji yangu, kwa jinsi alivyo mrembo.

Huyu rafiki yangu anataka eti mimi nimuoe mtalaka wake kisha baada ya mwezi nimuache, anadai kua mimi ni rafiki yake sana hivyo nitafanya uaminifu, kwamba akimpa kazi hiyo mtu mwengine anaweza akamgeuka baada ya kuoa akabaki na mke. Mimi nimejifikiria sana hili jukumu alilonipa ukweli naona ni mtihani tu huu napewa. Manake mkewe ni mzuri sana, mimi akishakua mke wangu manake ni halali kumuingilia kimwili.

Sijaelewa hapa ni Mungu au shetani ndio ananijaribu, au pengine hao nawasingizia bali najijaribu mimi mwenyewe. Jamaa anataka Wikiend hii tutkutane watatu, yeye, mii na ex-wife wake tupange tutakavyoicheza hii issue, nawaza hata siku hiyo niingie mitini ili achaguliwe mtu mwengine.

Hivi nitawezaje kua na mke mzuri kama huyu kihalali kabisa, demu nilikua nikimfukuzia miaka hiyo leo nakabidhiwa kihalali kabisa halafu eti nikamuacha tu? Hata nikipita nae sio dhambi kwa Mungu, itakuaje dhambi kwa binadamu?

kiukwel kwanza kabisa ww huhitaji ushauri hapa, kutokana namaelezo yako ulivyo eleza kabala yayote huyo shemeji ako kabla hajawa shemeji ako uliwah kumtongoza lakin hukufanikiwa bahati mbaya au nzuri kwa sasa kisha kuwa shemeji ako, sa utawezaje kuishi na mwananke ambae ulikuwa unamtaman nainaonekan mpaka sasa ijapo kuwa nishemeji ako lakin bado unamtamani usiweze kufanya nae tendo..!? pili kitendo anacho kifikiria huyo jamaa yako cha kumrudia huyo dada alie kuwa mke wake kwa kufanya udanganyifu mbele ya Allah (s.w) eti mpange kuwa umuowe wewe kimkataba kisha umuache ili yeye aweze kupata fursa ya kumrudia kuwa mke wake halali mbele za mungu nidhambi na dhambi hiyo ww pia utahusika kwa sa7bu mkisha panga kuwa ww umuoe alaf baada ya mwez 1 umuache ili yulejamaa yako apate uhalali wa kurudiana na huyo mwanamke kama mke na mme haita hesabika kuwa hawa wawili eti waishi katika ndoa bali watakuwa wanaishi kama mtu na hawara yake ko watakuo kila wanapo shiriki tendo mbele ya Allah inahesabika kuwa wanazini ko dhambi ya hawa wanao zini nawe ndio kiunganishi lazima utahusika nayo na si vinginevyo., ko nakushaur nakuomba usishiriki ktk huu mpango...
 
y
hii ni story ya uongo kabisa talaka moja anamrudia vizuri tu,kajipange bro
Talaka moja ya toka July 2016 kila mmoja akakaa kwake na mali washagawana si ni sawa na wameachana tu??
Hata jamaa akajaribu kuanza mahusiano mengine hapo kati ila akajikuta moyo uko kwa ex-wife wake. Shem nae sijui kamanae alipata mtu maana after breakup sikua nae karibu although sometimes alikua akinipigia kuomba nimkutanishe na mshikaji
 
Kweli umeongea kitu,
kumbe kwa vile ndio kwanza amemuacha basi anaweza kumrudia bila hata ya mimi kuingilia kati,
Nitatafuta wanazuoni wataalam nihakikishe hili
Ongea nae kk, asikurupuke.. Mimi nshanotice tatizo
 
Ima ni story ya kutengeneza ama laaah jamaa yako na huyo mtalaka wake hawaujui uislam!
 
Hadithi ya shigongo hii,
Sheria yenyewe haukubaliani na kufanya udanganyifu kama huu wa kuowa na kuacha, kama mpango wake huo anajidanganya tu
 
Makubaliano ni only one onth ndio nimpe talaka, makubaliano engine ni kwaba nisimguse. Kwa kifupi ni kua Jumamosi ndio tunakaa kikao cha kupanga mipango mizima

Wewe umeshaoa?
Ukimwoa huyu mwanamke utakaa nae kwako au atakuwa anakaa kwa mumewe? au kwao?
Je hamuoni kuwa hapo mnamdanganya Mungu, mwambie rafiki yako ni kuwa , sheria inataka aoelewe, aingiliwe, then akitalikiwa yeye ndio anaweza kumwoa tena.
Ndio ajifunze kuacha wanawake kijinga jinga, unafikiri hiyo sheria iliwekwa kwa sababu gani? Kuwafundisha watu kama yeye kuacha kuchezea ndoa.

Kama wewe hutaki niambie mimi nije nimwoe nilale nae mwezi mzima, kama huyu mwanamke hajakataa kutalikiwa...
 
Katika dunia yetu ya sasa vitu vikubwa vi 2 vinavunja urafiki na undugu PESA na MAPENZI. Swala la rafiki yako liweke pembeni na jiulize wewe mwenyewe unahitaji na unataka nini??? Kama una mapenzi ya dhati na huyo mwanamke na yeye akaridhia kuolewa na wewe kwa upendo wake kwako basi fanya taratibu zako mwenyewe. Mungu anachukia talaka na ndoa za mipango. Tambua MAHITAJI YAKO
 
We miss chagga ukioa huwezi kumwita mkeo kama hujamwingilia kimwili. Sasa hapo atampaje talaka wakati hawajakamilisha hitimisho la ndoa???
 
Kuoa kwa mipango ili umuache arudiane na mtalaka wake haiswihi. Kuoa bila kumpa haki yake ya unyumba mkeo pia haiswihi.
 
ALIYEOZESHA NDOA YAO YUPO WAPI?
MAANA KWA UCHACHE WA ELIMU YANGU YA DINI YA KIISLAM SHERIA YA KUTOA TARAKA ZIPO IVI;

TARAKA MOJA; UKIMPATIA MKEO TARAKA MOJA INA MAANA YA KUWA KABLA YA KUONDOKA UTAKAA NAE NDANI SIKU 90 BILA KUMUINGILIA NA ZIKIMALIZIKA HIZO SIKU UNA MUAACHA. NA PIA TARAKA MBILI HII INA MASHARTI KAMA YA IYO TARAKA MOJA.

TARAKA TATU HII UKIMPA MKEO TARAKA TATU INATAKIWA HAURUHUSIWI KUMUOA MPAKA AOLEWE HUYO MWANAMKE NA AACHIKE NDIPO UMREJEE MKE WAKO,PIA HAIRUHUSIWI KUTOLEWA TARAKA TATU MOJA KWA MOJA NA ATA KAMA UMETOA WALE WALII WAKO NA WALIOZESHA WANAITEBGUA NA INAKUWA UMETOA TARAKA MBILI. (HAIRUHUSIWI KUMTUMA MTU AKAMUOE MWANAMKE WAKO ALAFU AMUACHE ILI UPATE KUMRUDIA)

TARAKA INAKUBALIKA KWA KUONGEA AU KUANDIKA NA KATIKA VITU VITATU VISIVO NA MZAHA KWA ALLAH NI TARAKA ATA UKISEMA KWA MASIHARA UWA KWELI.
 
Uwongo wa kutosha, talaka mwisho 3 time ndio huwezi kumrudia hadi atakapo olewa na kuachwa na mtu mwengine ndipo huyo x aweze kuposa upya mahari mapya, kama una Dreams za kupata muarabu utaota sana, labda uwoe mrangi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom