Shark
JF-Expert Member
- Jan 25, 2010
- 29,635
- 29,509
Za jioni wakuu,
Ninahitaji ushauri wenu awdau, na nitaanza na historia kidogo.
Kuna rafiki yangu mmoja tuemshibana sana, ni rafiki yangu wa kufa na kuzikana, mi na yeye ni zaidi ya rafiki na hata kama ni udugu basi huu wetu ni zaidi ya udugu. Jamaa yangu huyu tumejuana toka Sekondari Miaka kama 20 iliyopita, tukaenda wote Chuo pamoja. Kifupi ni kwamba huyu jamaa ni rafiki yangu mno toka miaka hiyo mpaka sasa.
Sasa bwana huyu tukiwa chuo alibahatika kupata mwenza wa maisha mnamo mwaka 2000, binti wa Kimanga, shombe shombe, mtoto mkali, kwao geti kali, getini mbwa mkali na pengine kitandani atakua ni mtamu zaidi ya asali. Binti huyu ni kifaa hasa, ameumbika, si mwembamba lakini pia katika mabinti wanene hayupo, na ukipishana nae lazima utageuka tu kumuangalia taka usitake. Yaani kifupi huyu binti pale chuo alikua ndio kifaa, na hata Jamaa kumpata ilikua kama zali hivi.
Jamaa baada ya kumuoa huyo binti bana maisha yakasonga, miaka hiyo ndoa ina furaha tu haina migogoro, shida imeanza mwaka jana, shetani kaingilia kati, kila siku ugomvi mwishowe mwaka jana mwezi wa saba wakaachana kabisa kwa talaka. Cha ajabu baada ya talaka ndio wakagundua kua wanapendana sana na hawawezi kukaa bila kuonana hivyo wanahitaji kurudiana na kua pamoja kama zamani.
Sasa kwa mujibu wa ndoa za Kiislamu, mkishaachana kwa talaka, ili mje mrudiane tena inabidi mke aolewe kwanza na mtu mwengine kisha aachike ndio umuoe tena. Mshikaji wangu huyu kafikiria wee, kaja na jibu kua atafute mtu akubaliane nae kua amuoe ex-wife wake kisha aachane nae ndio yeye amrudie, na mtu mwenyewe aliemchagua wa kumuoa ex-wife wake ni MIMI. Ukweli mmoja ni kua mimi ni mmoja kati ya waliokua wakimfukuzia huyu Binti kabla hata ya mshikaji wangu hakumpata miaka hiyo chuo, na miaka yote hiyo nimekua katika wakati mguu sana kila nimuonapo huyu shemeji yangu, kwa jinsi alivyo mrembo.
Huyu rafiki yangu anataka eti mimi nimuoe mtalaka wake kisha baada ya mwezi nimuache, anadai kua mimi ni rafiki yake sana hivyo nitafanya uaminifu, kwamba akimpa kazi hiyo mtu mwengine anaweza akamgeuka baada ya kuoa akabaki na mke. Mimi nimejifikiria sana hili jukumu alilonipa ukweli naona ni mtihani tu huu napewa. Manake mkewe ni mzuri sana, mimi akishakua mke wangu manake ni halali kumuingilia kimwili.
Sijaelewa hapa ni Mungu au shetani ndio ananijaribu, au pengine hao nawasingizia bali najijaribu mimi mwenyewe. Jamaa anataka Wikiend hii tutkutane watatu, yeye, mii na ex-wife wake tupange tutakavyoicheza hii issue, nawaza hata siku hiyo niingie mitini ili achaguliwe mtu mwengine.
Hivi nitawezaje kua na mke mzuri kama huyu kihalali kabisa, demu nilikua nikimfukuzia miaka hiyo leo nakabidhiwa kihalali kabisa halafu eti nikamuacha tu? Hata nikipita nae sio dhambi kwa Mungu, itakuaje dhambi kwa binadamu?