Ndoa ni taasisi tata jamani! kueni kabla ya kuianzisha

ndayilagije

JF-Expert Member
Nov 7, 2016
7,492
8,295
Heri ya Noeli waungwana

Nimewiwa kuwakumbusha na hili nalo tunapoelekea kuanza mwaka mpya tulitie moyoni.

Vijana wanazaliwa, wanakua, wanasoma, wanaoana na kujaliwa watoto. Hii inapendeza. Shida yangu ni hao tunaoanzisha nao familia.

Mwanaume ataacha wazazi wake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja.

Unapochagua sehemu yako ya kukamilisha mwili(mwenza) ni muhimu kuitazama siyo kesho yako ila keshokutwa yenu itakavyokuwa.

Kuna mengi ya kujiuliza kama kijana.

1. Je nikifukuzwa kazi huu ubavu utabakia?
Je, nikistaafu huu ubavu utaniheshimu?
Je, nikipata ulemavu tutaendelea kuwa pamoja kweli?
Na vipi kama hatutapata watoto tutaendelea kupendana?

2. Hivi tutakapokuwa wazee na watoto kutuacha kama tulivyowaacha wazazi wetu, purukushani za mji zikiwa ngumu kwetu tutaishije na wapi?

3. Vipi kama itatokea mmoja wetu kujikuta ana jukumu la kutunza ndugu/mzazi wake nitakuwa tayari kutoa msaada na kuvumilia?

4. Hivi wazazi wangu walipatia wapi na walikosea wapi?

Kimsingi ndoa inakupa mitihani kila siku na haitoi lecture hata siku moja, wala haisahihishi. Utasahihisha wewe na marks utajipa wewe. Ndiyo maana inahitaji uwe umepevuka ili kuyajua hayo na kuyakabili pia.

Hata hivyo ni muhimu tuoane tu, ila sasa kuishi kwa amani kwenye ndoa hiyo ni habari nyingine.

Ushauri.
Olewa /oa mtu na siyo watu/vitu.

Oa /olewa kwa ajili yako siyo watu wengine.

Chagua wakati sahihi kwako usiruhusu msongo wowote kutoka nje.

Usioe/olewe kama kulipa fadhila, epuka ndoa ya huruma.

Kubali kuwa ulivyo leo sivyo utakavyokuwa miaka 20 ijayo.

Jiandae na Mungu akubariki.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ushauri mzuri kwa wasio oa/olewa, na pia wale ambao wameingia kwenye maisha ya ndoa na huku wakiwa wanaichukulia ndoa kwa wepesi wepesi.
 
kuna watu niliachana nao wakaenda,niliumia sana mpaka kumpata niliye naye sasa hivi.lakini huwa najiuliza hivi fulani angeweza kuvumilia kuvukuzwa kwenye nyumba ya kupanga kisa kodi kweli.

ingawa huko waliko sio kuzuri zaidi yangu but huwa nasema wangeniumiza zaidi wakati ambao nahitaji faraja.
 
kuna watu niliachana nao wakaenda,niliumia sana mpaka kumpata niliye naye sasa hivi.lakini huwa najiuliza hivi fulani angeweza kuvumilia kuvukuzwa kwenye nyumba ya kupanga kisa kodi kweli.

ingawa huko waliko sio kuzuri zaidi yangu but huwa nasema wangeniumiza zaidi wakati ambao nahitaji faraja.
Akili za kimaskini hizi. Pambana bongo fursa kibao kama huna aibu
 
lazimauamini duniani wewe tu mwenye hati miliki ya kila kinachokuhusu furaha au huzuni kutegemea mwenza mshirikiane kubeba matatizo ni ulemavua wa akiri kama atakukimbia so what ? yule boss wa amazon kaachana na mke wake huku utajiri ukiongezeka , lazima tukubaliane hatukuumbwa kuishi pamoja.
 
Back
Top Bottom