Naomba kuwauliza mlioa jamani...
Hivi ukimuomba msaada kaka yako wa damu kabisa uwe ni wa pesa au hata kitu chochote ambacho kipo ndani ya uwezo wake lakini yeye badala ya kukupa wewe mdogo wake anakwambia kwamba unatakiwa ukamuulize mke wake kwanza yaani shemeji yako, akikubali ndio utapewa.
Unaamua kumwambia kaka yako aongee na mkewe basi kuhusu hilo ombi lako lakini anakwambia kaongee naye wewe mwenyewe. Hivi hii inamaanisha brother yako anakuwa hana sauti au ndio mambo ya ndoa yanavyokuwaga.
Nawasilisha....