Ndoa ni kizungumkuti..Kutoa msaada hadi apate ruhusa kwa shemeji!

Glenohumeral joint

JF-Expert Member
Oct 29, 2017
2,054
2,885
Naomba kuwauliza mlioa jamani...

Hivi ukimuomba msaada kaka yako wa damu kabisa uwe ni wa pesa au hata kitu chochote ambacho kipo ndani ya uwezo wake lakini yeye badala ya kukupa wewe mdogo wake anakwambia kwamba unatakiwa ukamuulize mke wake kwanza yaani shemeji yako, akikubali ndio utapewa.

Unaamua kumwambia kaka yako aongee na mkewe basi kuhusu hilo ombi lako lakini anakwambia kaongee naye wewe mwenyewe. Hivi hii inamaanisha brother yako anakuwa hana sauti au ndio mambo ya ndoa yanavyokuwaga.

Nawasilisha....
 
nguvu ya limbwata hiyo, mwanaume hutakiwi kutolewa maamuzi na mkeo kwenye vitu vidogo kama hivyo
 
Anajua wazi kuwa Mke wake (shemeji yako) ni kikwazo kwa Ndugu, hivyo ana imani kuwa utagonga Mwamba...
 
Mkuu kuta za nyumba zimeficha mengi sana

Kaka yako kukuambia hivyo ni tabia aliyo jitengenezea kipindi cha uchumba na ndo anayo endelea nayo bila kujua madhara yake
 
Kama huyo shemeji yako ana mdogo wake mpigie cm halafu muulize kama anahitaji msaada nani anamfata? Sister wake au kaka yako
Nikijibu suali lako huyo kaka yako bwege au atakuwa hataki kukupa hio hela.



Ndukiiiii
 
Ndoa ni siri nyeti,kama mke wake ni chazo kizuri cha Mali zake kwanini asikuambie hvyo.
Kuna hela ndani ya familia ni za wote au zina bajeti yake na mtunzaji na wife kwanni asikiambie vile?
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom