mtoto alipatikanaje?
aende kanisani au mahakamani
mkuu hebu tuambie vizuri kabla ya hapo ilikuaje hadi kufikia hatua wakazaa mtoto ba sasa miaka mitano kila mtu na chumba chake ... tueleze vizuri.. ili tujue tunashauri wapi...
Si aendelee na ustaarabu wake tu?
Ila walishakaa na kuzungumza? Kama wawili hawakufikia muafaka wazee wamehusishwa????
Duuhh, Miaka 3 pasipo kukutana/kukaa chumba kimoja kisa mila, hapo ndio tatizo lilipoanzia. Kwa nini walienda kufunga ndoa kanisani huku wangali wanazikumbatia mila & desturi? Ninachoshauri awaone wana sheria wampe upenyo wa kisheria utakaomsaidia kupata talaka.Baada ya kuzaa,mume akadai ampe mke muda wa kulea sababu mila za kwao wanatengana chumba miaka 3. Lakini hata baada ya miaka 3 kupita yule mume bado harudi chumbani. Wamekaa vikao vya ndugu, ila kama ujuavyo mdada anaambiwa vumilia. Mdada kachoka maisha hayo ndio kaamua kuangalia kama mahakama inaweza kutengua ndoa. Inaelekea jamaa si mzima, cha ajabu mume hataki kusikia kuachana. Anadai bado mkewe. Mdada hajui aanzie wapi kwenda mahakamani, hajui taratibu.
Wazee wamehusishwa,ila mdada anaambiwa vumilia. Mume hataki kuachana anadai yule bado mkewe.
Mke anataka waachane kisheria ili aendelee na life yake, mume hataki.