Hakuna kitu wanandoa wengi tunakosea kama kuchanganya ndoa na ndugu zako. Kwa maana kwamba kuona ndugu zako ni muhimu kuliko mkeo au mumeo. Sio kwamba hawatakiwi kuwa muhimu ila mwenzio wako ni muhimu zaidi maana anakujua vilivyo. Inashangaza kuona mume anapelekeshwa na mawazo ya ndugu au mke kadhalika. Tujifunze wana ndoa kutofautisha hivi vitu.