NDOA NA MAHUSIANO

NDOA NA MAHUSIANO

EmmilyPM

Member
Joined
Nov 14, 2018
Posts
56
Reaction score
65
Katika busara na upuuzi wangu, leo nimekuletea vitu vya kuzingatia katika mahusiana au ndoa yako. Mimi bado nipo single so kama nimekosea unaweza kunirekebisha [emoji23]

Kila mwanadamu utakae chagua kuoa/kuolewa nae ana mapungufu. Ni Mungu pekee asiye na mapungufu.
Kwa hiyo ukifuatilia mapungufu ya mwenza wako huwezi kuona mazuri yake. so jitahidi kuvumilia mapungufu ya mwenzako.

Kila mtu ana historia yake yenye makosa, kwasababu siamini ya kwamba kuna mtu yupo duniani ambae hajafanya makosa. Kwahiyo usitake kufuatilia makosa aliyeyatenda zamani . Lakini unapaswa kufutilia kuwa kajirekebisha makosa yake. Je, katatua mapungufu yake. Samehe na sahau yale ya nyuma. Kwa sasa hebu tafakari mabadiliko chanya ya mahusiano yenu

Kila wapenzi wana changamoto tofauti tofauti. Mahusiano si kitendo tu cha mapenzi mubashara tu[emoji1787] ila kuna mdaa mahusiano yanabadilika kuwa ukuni wa moto . Mapenzi ya kweli yanajionesha pale ambapo mnayatatua kwa pamoja changamoto mlizo nazo. Kwa wale waliopo kwenye ndoa kumbukeni ahadi zenu ' mtakuwa katika mazuri na mabaya, pamoja maradhi na afya '

Kila watu walio kwenye mahusiano wanatofautiana. Usipende kuringanisha ndoa yako na ya mwenzio. Hata siku moja wanadamu hatuwezi tukawa sawa. Lazima kuna vitu tunataofautiana, sasa inabidi kuwa na subira na kuvumilia. Natumaini mkizingatia uvumilivu wenu mtafikia malengo yenu mliojiwekea.

Jueni kwamba kuolewa/kuoa ni sawa sawa na kuwa katika vita. '' kwahiyo usiitake ndoa kwa pupa '' lazima ujue kupigana vita vya kupinga ujinga, kutofanya ibada, kutosameana, kutosikiliza ushauri wa watu wanaotaka kuvunja mahusiano yenu, kukosa uaminifu, uvivu, kutoheshimiana na usaliti, mkiweza kushinda vita hivyo mahusiano yenu yatakuwa ya amaani ila ikishindikana itakwa kinyume chake.

#coped
 
Back
Top Bottom