Ndoa imara hujengwa na mwanamke imara

Ndoa imara hujengwa na mwanamke imara

simba songea

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2016
Posts
1,496
Reaction score
1,219
Habari wana JF, heri ya sikukuu ya muungano,

Kitambo hatujajuliana hali humu ndani. Pengine ni mihangaiko ya Dunia.

Basi bila kupoteza muda tuanze na mada tajwa hapo juu.

Tukianzia kitabu cha mwanzo kinasema ubavu mwanamke wa kushoto umetokana na mwanaume. Mwanamke ni msaidizi wa mwanaume, mwanamke ndo dira ya mwanaume maishani. mwanamke ndo chanzo cha ulimwengu. Dunia bila mwanamke bure haina muendelezo.

Tukija katika maisha ya ndoa. Tunaambiwa wana ndoa muinganiko wa hiari kati ya mwanaume na mwanamke na kuwa mwili mmoja.

Wanawake wengi kwa kutokujua thamani yao wamekuwa wakivunja ndoa kwa makusudi. Wanasahau hao ni kioo hao ni mapambo ya Dunia, kuna usemi unasema DUNIA INA MAAJABU YAKE UKIACHA PESA MAGARI KINACHOFUATA NIA MWANAMKE.

Wake wengi wa ndo si wanyeyekevu ni waoga, Mwanamke ukiwa mnyonge mme atakudharau, ukiwa mnyenyekevu mme atakupenda. Wake wengi wa ndoa waliposikia mwanaume ni kichwa basi kakariri kila kitu kwamba kila kitokacho kwa mwanaume ukiogope.

Wanawake wengi wa ndoa ni viburi si wanyenyekevu kwa waume zao. Kiburi hatambui anaweza nini wala kwa wengine, majivuno anatambua anaweza nini, mnyenyekevu anatambua kasoro.

Wanawake wengi wa Mungu wanajua kasoro zao ndio maana unyenyekea. Wanawake wengi wanaumia sana kwa vile wanadhani wanapendwa. ndomana ujikuta wanakuwa viburi.

Wanawake wengi wanajua ili uweze kuwa na furaha basi uwe na mali. Wanasahau furaha si mali ni hali mwenye furaha ni yule anayefurahia. Ukiwa na uwezo kununua kila kitu si tajiri una mali, hakuna tajiri anayeweza kununua kila kitu.

Nimalizie kwa kusema 'DUNIANI UTAKUMBUKWA KWA VITU VIWILI, MATATIZO ULIYOTATUA NA MATATIZO ULIYOSABABISHA.
 
Back
Top Bottom