shuka chini
JF-Expert Member
- Feb 27, 2024
- 1,549
- 3,088
Ndoa ni ya Me wenye uanaume tu na Ke wema wala si Wavulana, zingatia "uanaume".Ndoa hizi zitatuua.Jamani ipo hivi .Mimi ni mme mwenye mke mmoja na mtoto mmoja.Mke huyu tumetoka nae mbali tulianza nae enzi tunasoma mwaka 2008 kipindi hicho nipo kidato cha tatu yeye kidato cha kwanza.
Changamoto aliyo nayo ni kelele na wivu uliopitiliza yani sina amani ndani akianza kuongea hamalizi .
Nimeshapiga sana mpaka basi kiufupi tabia yangu niyakawaida sichepuki sana. Sasa juzi hapa kafanya kituko nimetoka mapema asubuhi kumbe huku nyuma kafanya vurugu kwa majirani yupo mama mmoja ni msimbe sasa mke wangu anahofia kuwa natembea nae .
Kiukweli huyu mama hata sijawahi kumtongoza ila mke wangu anamuhofia bure.Hili jambo linanipakero sana.
Mungu kajaria tumejenga sasa kila siku ananitisha kwamba tutauza nyumba tugawane.
Vurugu ikizidi sana hii ndoa itakuja kufa bora kuanza upya kuliko kuishi bila amani.
Hivi wadau mnaishije na aina hii ya wanawake. Ninachangamoto sana yani hapa nimekaa juu ya jiwe kijiweni nawaza namna ya kurudi nyumbani maana nikifika tu ni kelele.
Nawasilisha wakuu.
Anamaanisha anataka mtalikiane mgawane mali kama hiyo nyumba?ananitisha kwamba tutauza nyumba tugawane
Ndio mkuuAnamaanisha anataka mtalikiane mgawane mali kama hiyo nyumba?
Ukiona mwanamke kidogo tu anakimbilia kusema tugawane maliNdio mkuu
Da wako vipiKwanza wa kwako ana afadhali.... mpe muda atatulia tu