Ndoa hii ya CCM na serikali itavunjika lini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndoa hii ya CCM na serikali itavunjika lini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tikerra, Sep 13, 2008.

 1. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #1
  Sep 13, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Katika siku hizi za karibuni tumeiona nchi yetu ikitumbukia katika matatizo makubwa ya ufisadi wa kutisha,pamoja na ukweli kwamba uovu mwingine pia umeongezeka katika kiwango cha kutisha.Lakini kwa maoni yangu mimi,uhusiano huu ambao sio sahihi kati ya CCM na Serikali, umetuingiza katika matatizo makubwa sana.Tumeshuhudi fedha za wavuja jasho zikichotwa na kupelekwa kwenye uchaguzi.Hatujui kwa uhakika ni kiasi gani,lakini ninaamini zilizochotwa kupitia EPA sio picha halisi.Hatujui kwa uhakika za Richmond,EPTL nk.ziliishia wapi,inawezekana CCM.Ninachojiuliza siku zote ni kwamba hivi CCM haina ubunifu wa kutosha wa kujipatia fedha zake yenyewe mpaka iwaibie wananchi,ambao kwa bahati,mbaya inatamba kwamba inawatetea?Hivi CCM itaomba majamvi msibani mpaka lini?Wananchi hao hao inaosema inawatetea inazidi kuwafukarisha kupitia kwenye mgongo wa serikali.Kikwete amka bwanaaa.
   
Loading...