Ndoa/Harusi

Shayu

Platinum Member
Joined
May 24, 2011
Posts
608
Reaction score
1,658
Haijalishi ukubwa wa harusi uliyofanya kitu cha muhimu ni unachokwenda kukijenga baada ya harusi, baada ya watu wote kuondoka na kuwaacha peke yenu mwende nyumbani, mkaanzishe maisha yenu. hiko ndicho cha muhimu na ndicho kinachotakiwa kupewa umakini mkubwa. Usisahau hilo jua kwamba una kazi kubwa mbele yako, na usichukulie harusi kwa ukubwa usiostahili zaidi ya kile unachoenda kukijenga. "Familia"

Harusi ni ya siku moja, lakini unachokwenda kukijenga huenda kikaishi muda, zaidi ya uhai wako. Kwakuwa misingi utakayo wajengea watoto wako ndio misingi hiyo hiyo watakayo wajengea watoto wao. Ubora wa familia yako huenda ukawa pia ubora wa familia zao. Inategemea ulivyolelewa na wewe utawalea hivyo hivyo. Kwahiyo kwa mwanamume hana haja ya kufurahia harusi bali kufikiri kazi iliyo mbele yake. Kulea watoto katika maadili na nidhamu. Kulea watoto kama simba walio nyikani, ili wakabiliane na changamoto zote za duniani. Kwasababu maisha ya duniani sio rahisi sana yanahitaji busara kukabiliana nayo. Unawezaje kufanya harusi kubwa na kujenga baadae kisicho na thamani? Ewe kichwa cha familia? Watu wengi sasa hivi walinya harusi kubwa lakini ndoa haijasimama na nyingine zimesambaratika. How great failure you are! Kazi ya kichwa cha nyumba ni kuunganisha familia kuifanya iwe moja.

Harusi si kitu ndoa ndio msingi, Ndoa inahitaji busara, hekima na maarifa kuijenga na kuiendeleza. Ndio yenye thamani kuliko harusi. Waambieni wanaume waheshimu familia zao. Kwakuwa huo ndio uanamume.

Love, respect , courage and faithfulness, are the pillar and foundation of marriage.

Jua kwamba sababu ya kuwepo wanaume na wana wake ni kujenga familia. Kutiisha watoto na ku mantain order on the earth. Ni bora usioe kama huna uhakika na unachokwenda kukijenga kwenye ndoa. Kwasababu kuingia kwenye ndoa na kuibomoa kwa mikono yako ni ujinga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…