Gideon Mwasabwite
Member
- Sep 10, 2012
- 23
- 8
Siwezi kushangaa wana CCM wanapobadilika hata baada ya hapo awali kuonyesha wazi wazi kuwa wanataka serikali tatu. Haka ni kamfumo ambako kamo ndani ya chama hiki ingawa wengi wataona ni mageni haya kwao. Sishangai kuona hata wale ambao tuliwaamini kuwa ni wazalendo kwa Taifa hili nao leo wanaimba wimbo wa wakubwa.
Ndivyo walivyo, maana tangu mwanzo waliimba wnyimbo za mapacha watatu, siku 90 mafisadi wang'oke, huyu ni fisadi wa majengo pacha twin tower ya BOT lakini mwenyekiti bila soni akamshika mkono jukwaani na kusema ni mtu safi huyu mpeni kura. Baadae kwenye kipindi maalum cha luninga akasema "watu wanashangaa kumnadi, sasa walitaka ni mnadi mtu wao wakati huyo ndiye mtu wa chama changu"?
Nape Nnauye mwaka 2007 aligombea uenyeketi wa UVCCM moja ajenda kubwa aliyosema inamkera na lazima aishughulikie ulikuwa ni mradi wa jengo la kitega uchumi la Umoja wa Vijana Lumumba. Alisema kuna ufisadi mkubwa sana akimtaja mzee Edward Ngoyai Lowassa kuwa ndiye fisadi wa mradi huo na hawezi kuukubali ukaendelea. Alimsema sana mzee huyu tena kwenye vyombo vyote vya habari. Mzee huyu wakati huo alikuwa ndiye mlezi wa UVCCM, lakini alipigwa chini kwa kigezo cha kumaliza muhula wa uongozi akiwa amezidi mwaka mmoja.
Alipoteuliwa kuwa katibu wa itikadi na uenezi wa kamati kuu, ndipo alipokuja na nyimbo nyingi za mafidi, kujivua gamba, siku tisini, wajitathimi, mapacha watatu n.k. lakini hakuna hata moja lilotimia zaidi wamegeuka na kuwatumia hao kama sehemu ya nguvu ya chama. Hii ndiyo CCM na wajumbe wake. Nape Nnauye anajisifu hivi sasa kwakuwa chama kina jengo la kisasa la kitega uchumi ambalo alimchafulia Edward Ngoyai Lowasa pasipo kurudi kwenye vyombo vya habari kuwaambia Watanzani kuwa mzee huyu nilimchafua naomba radhi kwake na kwa Watanzania wote. Alichokuwa anakikataa kuwepo kwake leo hii anakipamba chama chake kwa hicho mzee huyu akiwa hajamsafisha machoni pa watu kwa njia zile zile alizotumia kumchafua. Hii ndiyo CCM na wanachama pamoja na viongozi wake walivyo.
Hivyo usishangae kutokana na kubadilika kwao maana hadi leo zile siku 90 za mwaka 2012 hazijatimia na wale wale waliokuwa wanasemwa kuwa wanavuliwa magamba wanapewa nafasi kwenye kamati zao mbali mbali na kwa kura nyingi tu. Hivyo hata wale uliowaamini wasikushangaze wanapobadilika ghafula kwenye kuijadili rasimu ya katiba ya Tanzania ijayo. Kuwekeza uaminifu kwa mwana CCM ni sawa na kuwekeza imani yako kwa mwana chui ambaye wakati wowote atabadilika na kukuua zaidi akiangalia tumbo lake wala si wale utakaowaacha endapo hatakuangamiza leo.
Mungu ibariki Tanganyika, Mungu ibariki Zanzibar Mungu libariki shirikisho la Tanzania.