Dingswayo
JF-Expert Member
- May 26, 2009
- 4,019
- 2,932
Nashangazwa sana kwamba mpaka leo bunge letu linatumia njia ya wabunge kusema 'ndio' au 'hapana' katika kupiga kura. Njia hii haioneshi kuwa bunge letu kipo makini katika kufanya maamuzi kwa njia ya kidemokrasia. Ni vigumu sana kuhesabu kura za ndio au hapana kwa masikio tu. Vile vile ni vigumu kwa mbunge kupinga mambo mengine kwa sababu atasikika na wenzake.
Kama serikali imekuwa na uwezo wa kujenga jengo jipya la bunge, imeshindwaje kuweka mtambo wa ki elektroniki wa kupigia kura ambao utaonyesha kwenye screen kura za ndio na hapana kwa hesabu ya waliopiga? Kura ya namna hii ina faida kubwa mbili.
Faida ya kwanza ni kuwa kila kura inakuwa ya siri, kwani haitaonyesha nani amepiga kura ipi. Faida ya pili ni kuwa na uhakika thabiti wa kura zilizopigwa hata ikiwa imezidi au kupungua kwa kura moja. Pamoja na kutaka kuimarisha demokrasia nchini, uimarishaji wake huo uanze katika chombo hicho cha bunge.