Sasa ninapata picha mbaya sana kuhusu maisha ya Raisi Kikwete baada ya kumaliza muda wake wa uongozi. Nadhani Mr clean atakuwa ana nafuu na watu watamsamehe kwa kulinganisha na kitu Kikwete anajiundia kumalizia muda wake wa u-Raisi.
Ingefaa sana washauri wake wakajaribu kumtahadharisha kuhusu hili. Na yeye atakuwa na busara kama atachukua hatua za haraka kurekebisha mambo haya.
Inabidi amtoe IGP haraka sana maana tunahakika kuwa hakuna ripoti zozote za kiinteligensia anazo weza kuudhibitishia umma kuwa zilikuwa zinaashiria uvunjifu wa amani kwenye yale maandamano. Kwanza kabisa inaonekana hili ni jambo walikuwa wamepanga tangu baada ya matokeo ya uchaguzi. Walikuwa wanangoja tu Chadema ifanye mkutano wa hadhara na Dr.Slaa ahutubie kutangaza hadharani kuwa hamtambui Rais ili watume wahuni wao wenyewe kuanzisha vurugu na hapo ndiyo ingewezekana kupata hata sababu za kuua hata viongozi wa CDM. Mungu ameepushia hilo. Sasa inaonekana wanatafuta mianya mingine.
Nina hakika kabisa mpaka viongozi wengi namna hiyo wa Chadema kuhudhuria maadamano hayo wafuasi wao walishaonywa na hao hao viongozi watu wazima kama Mzee Ndesamburo, Dr. Slaa nk. Haiwezekani na haingii akilini kwa watu wazima kama hao wachague kipindi hiki cha maisha na umri wao kuanza kufanya fujo au kushiriki kwenye maandamano ya uharibifu.
Watu wote waliofanya ile fujo pale ni makachero wa CCM na kwa makusudi. Ndivyo chama hiki kilichojeuka kuwa cha kibabe sana kinavyoendesha mambo yake siku hizi. Sasa CCM imefilisika kimawazo mbinu zao zote zinaeleweka kwa jamii nzima ya watanzania. Mambo haya yanataka busara la sivyo siku ya siku kutakuwa jambo kama hili usikie hawa viongozi wa CDM walipigwa risasi na Jeshi letu litadai ilikuwa bahati mbaya haikukusudiwa. Kama wafuasi wa Chadema wangeleta fujo za kupambana na Polisi kwenye ile hali hilo lingetokea kwa kisingizio hicho. Mungu ametunusuru na jambo la hatari kubwa. Kwa ajili hiyo basi tunawaomba CCM na haswa Raisi Kikwete waangalie upya wanakotaka kulipeleka Taifa letu.