Ndesamburo ni kikwazo Uchaguzi wa Kanda ya Kaskazini CHADEMA

Ufipa-Kinondoni

JF-Expert Member
Jan 3, 2012
4,582
2,783
Ni zaidi tunavyojua kwa sasa, ila nimewahi leta hapa haya:

Uchaguzi wa ndani CHADEMA 2018/19 Utaenda na wengi.

Taarifa ya gazeti la MwanaHalisi juu ya Ben Saanane na uhalisia wa mambo

Ndugu Petro E. Mselewa aliandika haya:
Kadiri Lowassa anavyojiimarisha CHADEMA, ndivyo chama kinavyofifia na kupotea.

Watanzania ni wepesi wa kusahau ya nyuma. Maandiko ya hapa juu kwa mfuatiliaji ataona kitu.

Habari za kuaminika ni kuwa uamzi ya Mbunge wa zamani wa Moshi Mjini, Mhe. Ndesamburo umeotokana na msukumo kinzani juu ya mwelekeo ya CHADEMA. Habari za ndani zinasema kuwa mfumo wa uendeshaji chama unaotumiwa na Mbowe ndio unaoonekana kutokubalika kwake kwa siasa za sasa.

Kwa muda mrefu Lowassa ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya chama na Waziri Mkuu alijihudhuri kwa kashifa ya mradi wa Richmond, amesema kauli zinazokizana na mkubwa wake. Mara baada tu ya Lowassa kwenye uongozi ndani ya chama alisema "CHADEMA ime-graduate siasa za harakati, kimekuwa chama cha siasa". Pia, katika ziara yake katika mikoa ya pwani wiki mbili zilizopita alisikika akisema tuachane na kuendeshwa na harakati, tuwe na sera za chama.

Kauli zake, zimekuwa zinaungwa na watu wengi wakiwemo Mhe. Ndesamburo. Ndesamburo aliamua kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Kanda akipambana na kijana Daniel Porokwa. Hii hakuwa bahati mbaya bali ilikuwa imepangwa kubadili sura na falsafa ya uanaharakati wa Mbowe miaka nenda rudi. Pamoja na Uongozi wa Mkoa wa Tanga, Ndesamburo amekuwa kipenzi cha wanachama wengi wa CHADEMA hata CCM.

Ndesamburo ameonekana kuungwa na Grace Kihwelu anayepambana na Evarist Silayo anayegombea nafasi ya Mweka Hazina wa Kanda. Kati ya wanaogombea nafasi ya Mwenyekiti wa Wabunge wa Kanda anaungwa na Julius Kalanga, Lucy Owenya na Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini. Katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti kumekuwa na minong'ono ya kuwa Anna Gideria anayepambana na Cecilia Peroso kuunga harakati za Ndesamburo na Lowassa ndani ya Chama. Aidha, viongozi wengi wa chama Mkoa wa Tanga wamekuwa kinyume na maagizo ya Mbowe.

Kwa sababu hiyo uchaguzi uliokuwa ufanyike jana, 29/03/2017, uliahirishwa ghafla Mkoani Tanga wakati wajumbe wakisubiri ratiba ya uchaguzi na mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA bila kutoa maelezo ya kutosha kwa wajumbe. Habari zilizopatikana zinaonyesha, Mbowe alitiishwa na kutokuungwa kwa hoja zake nyingi ndani ya chama kitu alichogundua hataungwa mkono katika kuteka uchaguzi huo kama alivyofanikishwa katika Kanda zingine, mfano Kanda ya Nyasa. Katika uchaguzi wa Nyasa, Mbowe akishirikiana na Mhe. Mnyika waliondoa jina la Mgombea mmoja kati ya wawili. Cha ajabu, Mhe. Msigwa aliyesimama kama mgombea pekee hakupata hata % 60 ya kula zilizopigwa wakipinga kitendo cha Mwenyekiti wao kuweka watu anaotaka tu.

Kwa kutumia nguvu yake binafsi, Mbowe aliamua pia kuwafukuza uongozi viongozi wote wa Chama wa Mkoa wa Tanga bila sababu za kueleweka.

Habari zaidi zinaonyesha kuwa Mbowe amejipanga kupambana na kila aina watu wanaoitwa "Wa Lowassa" ndani ya chama chake. Habari zinazojulikana kwa watu wengi ni kuwa Lengo la Lowassa limekuwa kuteka chama cha CHADEMA na kukipa sura na sera mpya za kichama. Ametumia ushawishi wake, kuingiza timu yake ndani ya chama kama vile nafasi ya Uenezi Taifa anayoshikilia mtu wake anayeitwa Ally na hivi karibuni Masha ameingizwa kuwania nafasi ya Ubunge wa Afrika Mashariki.

Kilichobaki ni kuwa mpaka 2019, CHADEMA itahimili siasa za ndani kama CCM?

Updates 8/4/2017
Ukweli mchungu sana.

20170408_045850.jpg


Ndesamburo alivyoipasua Chadema Kaskazini
 
Wenye akili tumekuelewa, ni suala la muda tu Mbowe kufungashiwa virago....Watu wanaandaa mikakati mdogo mdogo.
 
Yaani sawa na mtu aliyeuza nyumba halafu ukaomba muda kujihifadhi, sasa mwenye nyumba anataka nyumba yake huna budi kuondoka!
 
Wakuu imebainika kuwa uchaguzi wa mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Kaskazini uliokumbwa na mizengwe lukuki umeacha kovu baya la usoni kati ya CHADEMA pro Mbowe na Chadema pro Lowassa.

Uchaguzi ule ulikuwa na mizengwe na fitna lukuki ambapo ilielezwa kuwa mh. Mbowe alikuja na mgombea wake mfukoni (Ndesamburo) na kulazimisha kuhakikisha anasimikwa uenyekiti wa chama hicho kanda ya kaskazini hali iliyozua tafrani kubwa kwani wanachama wengi walimtaka Porokwa ambaye ni muumini mkubwa wa Lowassa.

Ni wakati muafaka sasa kwa CHADEMA kuzingatia misingi ya kikatiba na sheria ili kiweze kukua na hatimaye kuchukua dola
 
Ubaguzi unaitafuna CHADEMA....eti wameenda kufanyia mkutano Tanga cha ajabu hakuna hata mgombea mmoja kutoka Tanga wote wametoka Moshi na Arusha
 
Wenye akili tulishaona chama kimetekwa na kugeuzwa timu Lowassa toka 2015.
Mpaka sasa hakuna namna ya kukiokoa chama imebaki kujipendekeza kwa waliokiteka.
 
Wishful thinking, Mbowe ni Kiongozi anayependwa na Kuheshimika. Lowassa hana uwezo wa kukisimamia Chama! Kwa Umri wake na mikiki ya Upinzani. Kusimamia Chama na Kuwa Mgombea wa Chama ni vitu viwili tofauti. Mbowe is the Greatest Politician ever ukiacha Mwalimu Nyerere. Amerecruit the best Politician katika chadema na kuwaweka pamoja!
 
Wishful thinking, Mbowe ni Kiongozi anayependwa na Kuheshimika. Lowassa hana uwezo wa kukisimamia Chama! Kwa Umri wake na mikiki ya Upinzani. Kusimamia Chama na Kuwa Mgombea wa Chama ni vitu viwili tofauti. Mbowe is the Greatest Politician ever ukiacha Mwalimu Nyerere. Amerecruit the best Politician katika chadema na kuwaweka pamoja!
Mbowe kwa kuuza chama kwa mafisadi is the best kweli
 
Huu uzi mbona unawachangiaji wachache hivi? Nyumbu wameenda kunywa maji? Angalieni mamba wasiwale. He hee
 
Hizoo ni propaganda CHADEMA ni chama imara. Wasomi na wenye vyeti wapo wakutosha
viongozi wana maono.

2020 CCM lazima jasho liwatoke.
 
Sikuungi mkono, lakini kuna minyukano ya chini chini ndani ya CHADEMA.
WASIPOANGALIA WATAJUTA.
 
Back
Top Bottom