Ndejembi akutana na shehena kubwa ya mahindi Kibaigwa

ALWATAN KIZIGO

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
539
642
DC NDEJEMBI ASEMA TAIFA HALINA NJAA NA HALITAKUMBWA NA NJAA!

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mh Deogratius Ndejembi leo mapema, ametembelea Maghala ya Kuhifadhia Nafaka katika soko la kimataifa Kibaigwa.

DC Ndejembi amekagua Maghala hayo ili kujiridhisha na takwimu za uhifadhi wa chakula katika wilaya ya Kongwa.

"Kibaigwa ni Soko Kuu la kimataifa la Nafaka Nchini na kuna Maghala yakuhifadhi nafaka ambayo husambazwa nchi nzima na nchi za jirani. Akizungumza na uwongozi wa Soko hilo kubwa, DC alisema. "Nimekuja kujua kama kweli kuna Ujazo wakutosha ktk Maghala yetu, Nimeona kuna Chakula cha Kutosha na hakuna haja yakusikiliza maneno ya hao wanaotaka kutia Hofu watanzania yakuwa Eti Taifa linanjaa na litakumbwa na Njaa kwa kiwango cha aina yoyote".

Wanachi wa Wilaya ya Kongwa, Mkoa wa Dodoma na Tanzania kwa Ujumla Ondoeni Shaka Hakuna Njaa kwasababu chakula kipo. Na Wanasiasa Acheni Kupotosha Wananchi na kuwatia Hofu."


Mbali na hayo alizidi kufafanua akasema Kuna Hifadhi kubwa sana ya Nafaka na inazidi kutoka kuelekea maeneo mbali mbali Nchi, kama kuna mwenye uhitaji wa Mazao ya nafaka Aje Kibaigwa Kongwa atanunua Mazao Tani atakazo.

DC Ndejembi amesema "Kongwa kuna Vijiji kama HembaHemba, Ngomai, Kibaigwa , Mkoka na Mlali Vijiji hivi vina Akiba yakutosha ya Mazao ivo kwanini Mkuu wa Wilaya niseme kuna Njaa?

Alimalizia Mazungumzo yake ametoa wito kwa Watanzania kuwa Makini na Wafanya Biashara ambao hucheza dili za kuuza Mazao na wamezoea kuishi kwa kupewa Vibali vya serikali kwa kununua Mazao kwa bei nafuu kisha kuwauzia Watanzania kwa bei ya Juu!
Lakini wamekuwa wakiishi kwa kuanzisha Matatizo ili kutumia Fulsa hiyo kujinufaisha wao. DC Kasema Watanzania wawe makini sana pia na Wanasiasa ambao wameshaanza kupita nakuwadanganya kuwa Taifa halina Chakula na wao watawaletea Chakula huo ni uwongo mtupu. Naomba mfahamu kuwa Mh Rais na sisi wasaidizi wake Bado hatujashindwa kulihudumia Taifa hili.

Aliyasema Ndejembi Mkuu wa Wilaya ya Kongwa alipokuwa Kibaigwa katika Maghala yakuhifadhia Vyakula.
 

Attachments

  • VID-20170117-WA0138.mp4
    12.8 MB · Views: 26
Ameshalewa na hivo vijimilioni nne . Huwezi kuficha ndevu wala huwezi kuzuia mafuriko kwa beseni.
 
Asichokijua ni hio shehena imeongezeka kwa vile habari imeshakuwa mitaani kwamba njaa inakuja wenye pesa wanachukua haraka mzigo kabla haijawa nongwa.Na wanouza wanauza kwa vile shida za leo nazo ni kubwa kiasi cha kuwafanya washindwe subiri hadi njaa ipite.
 
Tangu msikie Zitto Kabwe atapeleka hoja ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais endapo mtu yeyote atakufa kwa njaa naona kuweweseka kumeongezeka!

Kelele nyingi za nini!!! Mara tunasambaza tani 1.5 Million; mara Kibaigwa kuna hindi nyomi... aaaaagrgh!
 
Ameshalewa na hivo vijimilioni nne . Huwezi kuficha ndevu wala huwezi kuzuia mafuriko kwa beseni.
Jamaa alisema huwezi zuia mafuriko kwa mikono, wewe umeona mikono ni midogo umeamua useme beseni. Bavicha aiseee!
 
Kibaigwa kuna ghala la serikali pale? Kama ndivyo lina tani ngapi? Serikali ina tani ngapi kwa ujumla na wafanyabiashara wana ngapi?
 
Njaa imehamia kichwani naona anakurupuka kama wenzie wameshikwa pabaya kila mtu anajaribu kumtetea bosi safari hii
 
Tani ngapi hyo? Walete takwimu
Hasemi tani ngapi. Nyingi kwa mwingine ni 5, 12, 20, 800...., nk. FF kusema watu wa namna hii walienda kusoma ujinga shuleni.
Mbaya zaidi hataji hata wastani wa bei. Mfanyabiashara hawezi kutoka Mtwara au Ukerewe kufuata mahindi Kibaigwa bila kujua bei yake.
 
Back
Top Bottom