Ndege yatunguliwa Ukraine

Ndege yatunguliwa Ukraine

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
27,898
Reaction score
63,523
110726170343_morocco_plane_crash_386x217_afp.jpg

Mabaki ya ndege ya kijeshi ya kubeba mizigo

Waziri wa Ulinzi nchini Ukraine amesema kuwa mojawapo ya ndege zake za kijeshi za kubeba mizigo imedunguliwa na wapiganaji wanaounga mkono Urusi ilipokuwa ikitua katika uwanja wa ndege wa Luhansk mashariki mwa taifa hilo.
Ndege hiyo ya jeshi la angani la Ukraine ilikuwa ikiwabeba wanajeshi pamoja na vifaa.

Ripoti zinaarifu kuwa wafanyikazi wa ndege hiyo pamoja na wajeshi wote 49 wamefariki.

Idara ya maswala ya kigeni mjini Washington ,Marekani imesema kuwa ina hakika kwamba mizinga pamoja na silaha nyengine kali zinazomilikiwa na wanamgambo wanaotaka kujitenga nchini Ukraine zilitoka nchini Urusi.
Msemaji wa Idara hiyo amesema kuwa mizinga iliokuwa katika kambi moja ya silaha za kijeshi kusini magharibi mwa Urusi iliondolewa katika kambi hiyo.

Waziri wa maswala ya kigeni nchini Uingereza William Hague amesema kuwa kuingia kwa vifaa hivyo nchini Ukraine hakuwezi kukubalika.

Chanzo:BBC
 
Hivi haiwezekan kabisa binadam tukaacha kuchokonoana. Ili tubakie kufa kwa ajali, magonjwa na uzee??
 
Naoana SAM units zishaingia Eastern Ukraine.Inawezekana kabisa Spetnaz ndo wameiangusha hiyo plane

Mchanganyiko wa Spetnaz na Chechen militias ni janga kwa Raisi mpya wa Ukraine
 
Kama kweli ya "mizigo" ilikuwa na haja ya kudondolewa???!!!
Ilikuwa inatoka wapi na kwenda wapi???!!
Kuna mchezo wa kuingiza silaha hapo watu wakastukia wakaona bora lawama kuliko fedheha ndio maana westerners wanalalamikia shifting ya silaha na kambi na waliohamisha walijua tu kwa hali hiyo traffic control ni muhimu!!!!!

Ilisemekana sumu iliyotumika Syiria iliingizwa baada ya mgogoro sasa huku naona watu wako macho!!!!!

Ila 49 wengi sana pia!!!!!
 
hiyo ndege ya jeshi ya mizigo iliyokua na wanajeshi 49 ilikua ILU-76...na jana hiyohiyo jet fighter SU-24 ilitunguliwa na anti ukraine militants wanaotaka kujiunga na Russia....Lakini US& UE wapo kimyaa nadhani baada ya vitisho dhidi ya Russia wakaona PUTIN hatetereki wakaamua NATO& US kufanya mazoezi ya kijeshi mpakani mwa Russia na Putin akaagiza yafanyike mazoezi apoapo mpakan kwa idadi ileile ya wanajeshi..Mbaya zaidi US ipo kwenye pressure nyumbani kwake kwa konachoendelea IRAK kwani magaidi ya ISIL and Levant wanaofungamana na alqaida wameteka miji kadhaa Irak na wameteka pia wanajeshi wa Turkey na wafanyakaz wa ubalozi wa uturuki mbaya zaidi hawahawa ndo waliokua wanapewa silaha na fedha na US na washirika wake uko Syria sasa wamegeukia Irak .....seneta J Maccain amemtaka US secretary of state kujiudhuru na viongozi waandamizi wa kiintellejensia kwa kishindwa kwa foreign policy yao......So ASSAD is very safe now kwan dunia nzima imeona jinsi alivyodili na magaidi na pongez za pekee zinaenda kwa Putin, Iran na hezbollah bila kisahau CHINA
 
That is history. Mambo yanaanza kumbadilikia US. Hao NATO ndo hoi kabisa. Yaani hata wakiungana hawamuwezi Rassia kwa lolote. Majeshi yake ni ya uhakika kuzidi ya hivyo vinchi vya ulaya. Amerika alishangaa kuona midege ya ajabu ya ki russia ikipita pembezoni mwa California bila kujua yametokea wapi. na ilivyogeuka ndo rada zikaona makombora yaliyokuwa yamebebwa na hizo ndege yenye uwezo wa air to air strike na air to land strike.
Ki ukweli wale jamaa wa eastern ukraine russia anawaback up ki taaram sana. Obama anapiga soga tu. eti nikikutana na putini nitamwambia atoke CRIMEA na aache kuwasaidia waasi wa ukraine. Maneno hayo ni kama umemkuta simba kashikiria swala anamtafuna alafu unatoa kibesi hacha! acha!
 
Asee ndugu tupo pamoja sana mimi pia nabarikiwa sana na matendo ya Urusi.Crimea imekombolewa na urushi bila hata ya risasi moja kurushwa.
Embu ona balaa linalowapata wa Ukraine baada ya OBama na EU kupeleka pua zao huko..Mi nazani hofu ya marekani nikushuhudia Soviet Union ikiundwa upya.na hivo kum challenge Usa as a world super power.
 
Kama kweli ya "mizigo" ilikuwa na haja ya kudondolewa???!!!
Ilikuwa inatoka wapi na kwenda wapi???!!
Kuna mchezo wa kuingiza silaha hapo watu wakastukia wakaona bora lawama kuliko fedheha ndio maana westerners wanalalamikia shifting ya silaha na kambi na waliohamisha walijua tu kwa hali hiyo traffic control ni muhimu!!!!!

Ilisemekana sumu iliyotumika Syiria iliingizwa baada ya mgogoro sasa huku naona watu wako macho!!!!!

Ila 49 wengi sana pia!!!!!

Inawezekana ndani ya hiyo Cargo plane kulikuwa na mzigo muhimu sana ambao ungebadilisha facts on the ground.Yaweza kawa Black Water/Academi mercenaries au silaha nzito nzito kuifanay iwe high value target

Kulikuwa na reports RT kuwa Ukraine forces wanatumia white phosphorus kweny mji wa Slavayansk.Sasa sijui sumu nyingine zipi zitatumika tena kama Syria

49 ni wengi si kitoto
 
hiyo ndege ya jeshi ya mizigo iliyokua na wanajeshi 49 ilikua ILU-76...na jana hiyohiyo jet fighter SU-24 ilitunguliwa na anti ukraine militants wanaotaka kujiunga na Russia....Lakini US& UE wapo kimyaa nadhani baada ya vitisho dhidi ya Russia wakaona PUTIN hatetereki wakaamua NATO& US kufanya mazoezi ya kijeshi mpakani mwa Russia na Putin akaagiza yafanyike mazoezi apoapo mpakan kwa idadi ileile ya wanajeshi..Mbaya zaidi US ipo kwenye pressure nyumbani kwake kwa konachoendelea IRAK kwani magaidi ya ISIL and Levant wanaofungamana na alqaida wameteka miji kadhaa Irak na wameteka pia wanajeshi wa Turkey na wafanyakaz wa ubalozi wa uturuki mbaya zaidi hawahawa ndo waliokua wanapewa silaha na fedha na US na washirika wake uko Syria sasa wamegeukia Irak .....seneta J Maccain amemtaka US secretary of state kujiudhuru na viongozi waandamizi wa kiintellejensia kwa kishindwa kwa foreign policy yao......So ASSAD is very safe now kwan dunia nzima imeona jinsi alivyodili na magaidi na pongez za pekee zinaenda kwa Putin, Iran na hezbollah bila kisahau CHINA

Wapo wachache sana wenye mtazamo kama wako wengi wanaamini kila wanachoambiwa na CNN na BBC
 
Inawezekana ndani ya hiyo Cargo plane kulikuwa na mzigo muhimu sana ambao ungebadilisha facts on the ground.Yaweza kawa Black Water/Academi mercenaries au silaha nzito nzito kuifanay iwe high value target

Kulikuwa na reports RT kuwa Ukraine forces wanatumia white phosphorus kweny mji wa Slavayansk.Sasa sijui sumu nyingine zipi zitatumika tena kama Syria

49 ni wengi si kitoto

Wataumia watu wengi ila hapa sasa wenye macho wataona tofauti ya propaganda na uwezo halisi
 
Back
Top Bottom