Ndege ya Uingereza F35 yaanguka Baharini

Ndege ya Uingereza F35 yaanguka Baharini

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2020
Posts
5,547
Reaction score
14,209
Wale wanazi wa F35, njooni hapa

====

Ndege ya kivita ya Uingereza F-35 imeanguka baharini wakati wa operesheni ya kawaida katika bahari ya Mediterania, Wizara ya Ulinzi imesema.

Rubani aliondoka na amerejea salama kwa meli ya kubeba ndege ya Royal Navy HMS Queen Elizabeth na uchunguzi umeanza, MoD aliongeza.

Tukio hilo lilitokea saa 10:00 GMT juu ya maji ya kimataifa na hakuna ndege nyingine iliyohusika. MoD alisema haitakuwa muafaka kutoa maoni wakati wa uchunguzi.

Waziri wa Ulinzi Ben Wallace alisema ndege hiyo ilishuka mara baada ya kupaa.

Alisema: "Tunafurahi kwamba rubani yuko salama na amerejea kwenye ndege."

Bw Wallace aliongeza kuwa safari za ndege za za mafunzo ndani ya HMS Queen Elizabeth zinaendelea licha ya kisa hicho.

Kuna F-35B nane za Uingereza kwenye meli hiyo na 10 kutoka Jeshi la Wanamaji la Marekani. Wameendesha takriban safari 2,000 za kupaa na kutua kwenye HMS Queen Elizabeth bila tukio lolote kubwa katika kipindi cha miezi sita iliyopita.

Ndege hizo ni ndege za hali ya juu zaidi na za gharama kubwa zaidi za Uingereza. Zinagharimu karibu £100m, zinaweza kutua wima, sawa na Harrier Jump Jet, na kuchanganya teknolojia ya siri ya kukwepa rada na kasi kubwa zaidi.

Huku rubani akiwa amejitoa salama na sasa amerejea kwenye meli ya ndege, juhudi sasa zitakuwa kuirejesha ndege hiyo, ambayo kila moja itagharimu takriban £100m.

F-35 imejaa teknolojia na data nyeti sana.

Ndege yenye uwezo mkubwa iliyoundwa na Marekani - ambayo ni vigumu kutambulika kwenye rada - ni mojawapo ya miradi ya gharama kubwa ya ulinzi inayofanywa na jeshi la Marekani.

Hii ni mara ya kwanza kwa ndege ya F-35 ya Uingereza kuanguka, lakini kumekuwa na visa kadhaa vinazohusisha ndege za Marekani.

Mnamo mwaka wa 2018 Pentagon ilisimamisha kwa muda ndege zote za F-35s baada ya ugunduzi wa shida na mirija ya mafuta ya ndege gizo. Hayo yalikuwa yametatuliwa.

Uchunguzi tayari unaendelea kubaini kwa nini ndege hiyo ya Uingereza ilianguka.

Bila ndege zingine zinazohusika au vitendo vya uhasama uchunguzi huo unaweza kuzingatia hitilafu ya kiufundi au makosa ya kibinadamu.

Ndege kutoka HMS Malkia Elizabeth hapo awali zilishiriki katika mashambulizi dhidi ya mabaki ya kile kinachoitwa Islamic State nchini Iraq na Syria.

Meli hiyo ya kubeba ndege ye tani 65,000 inarejea Uingereza kutoka kwa misheni yake ya kwanza, ambayo ilijumuisha mazoezi na jeshi la India.

Ilikuwa ni sehemu ya kundi la msafara wa meli kubwa za kivita kupelekwa katika eneo la Indo-Pasifiki huku kukiwa na mvutano mkubwa na China.

F-35s zinaendeshwa na kikosi mashuhuri cha 617, kinachojulikana kama "Dambusters".

Ndege hizo za F35 ziliundwa na kampuni ya Marekani ya Lockheed Martin, na huendeshwa na marubani kutoka Jeshi la Wanahewa la Royal na Royal Navy, iliyoko RAF Marham huko Norfolk.

Waziri wa Mambo ya Nje Liz Truss alikuwa kwenye meli hiyo kwa muda mwezi uliopita katika siku ya mwisho ya ziara yake ya siku mbili nchini India.
 
Back
Top Bottom