Ndege mbili za Urusi zatua nchini Venezuela

HMG

New Member
Joined
Feb 2, 2019
Posts
1
Reaction score
7
Ndege mbili za kijeshi za Urusi zilitua katika uwanja mkuu wa ndege wa Venezuela Jumamosi, zikiripotiwa kuwa na makumi kadhaa ya wanajeshi na kiwango kikubwa cha zana.

Ndege hizo zilitumwa "kutekeleza mkataba wa kijeshi wa kiufundi ", limeripoti shirika la habari la Urusi Sputnik limeripoti.

Javier Mayorca, mwandishi wa habari wa Venezuela, aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba aliona wanajeshi wapatao 100 na tani 35 za vifaa vikishushwa kwenye ndege.

Hii inakuja miezi mitatu baada ya nchi hizo mbili kufanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi.

Urusi imekuwa mshirika wa muda mrefu wa Venezuela, ikiikopesha nchi hiyo iliyoko Amerika Kusini mabilioni ya dola na kusaidia sekta yake ya mafuta na jeshi.

Urusi pia ilikuwa wazi kupinga hatua ya Marekani ya kuiwekea vikwazo serikali ya rais wa Venezuelan Nicolás Maduro.

Bwana Mayorca alisema kwenye Twitter ndege ya kijeshi ya Urusi ya mizigo Antonov-124 na ndege ndogo aina ya Jet zilitua karibu na mji mkuu Caracas siku ya Jumamosi.

Alisema kuwa Generali wa Urusi Vasily Tonkoshkurov aliwaongoza wanajeshi hao walipokuwa wakitoka ndani ya ndege.

Ndege ya kijeshi ikiwa na nembo ya bendera ya Urusi inaonekana kwenye uwanja wa ndege Jumapili. Picha kwenye mitandao ya habari ya kijamiipia zilionyesha wanajeshi wamekusanyika katika uwanja wa ndege.

chanzo bbc swahili
 
Attachments

  • _106163567_hi053153570.jpg
    _106163567_hi053153570.jpg
    9.1 KB · Views: 92
Operation chota dhahabu-Putin anahamusha dhahabu ya Venezuela serikali ya Maduro kuanguka muda wowote.Maduro kupewa hifadhi Moscow.
 
Shida zipo kila nchi hapa duniani muhimu Uhuru wa kujitawala.
Sasa wangewaletea hata madawa basi. Niļiangalia documentary moja inaelezea hali ya uko Vene nì mbaya sana haswa huduma za âfya, wamama wanaenda kujifungulia Colombia
 
Hakuna cha ajabu kwa wavenezuela kujifungulia Colombia wakati hapa Tanzania MBUNGE ANAKAA miezi 9 ughaibuni akilea mimba na KUJIFUNGULIA Marekani! We unashangaa watu kwenda kujifungua na kurudi,
 
Ndege mbili za kijeshi za Urusi zilitua katika uwanja mkuu wa ndege wa Venezuela Jumamosi, zikiripotiwa kuwa na makumi kadhaa ya wanajeshi na kiwango kikubwa cha zana.

Ndege hizo zilitumwa "kutekeleza mkataba wa kijeshi wa kiufundi ", limeripoti shirika la habari la Urusi Sputnik limeripoti.

Javier Mayorca, mwandishi wa habari wa Venezuela, aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba aliona wanajeshi wapatao 100 na tani 35 za vifaa vikishushwa kwenye ndege.

Hii inakuja miezi mitatu baada ya nchi hizo mbili kufanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi.

Urusi imekuwa mshirika wa muda mrefu wa Venezuela, ikiikopesha nchi hiyo iliyoko Amerika Kusini mabilioni ya dola na kusaidia sekta yake ya mafuta na jeshi.

Urusi pia ilikuwa wazi kupinga hatua ya Marekani ya kuiwekea vikwazo serikali ya rais wa Venezuelan Nicolás Maduro.

Bwana Mayorca alisema kwenye Twitter ndege ya kijeshi ya Urusi ya mizigo Antonov-124 na ndege ndogo aina ya Jet zilitua karibu na mji mkuu Caracas siku ya Jumamosi.

Alisema kuwa Generali wa Urusi Vasily Tonkoshkurov aliwaongoza wanajeshi hao walipokuwa wakitoka ndani ya ndege.

Ndege ya kijeshi ikiwa na nembo ya bendera ya Urusi inaonekana kwenye uwanja wa ndege Jumapili. Picha kwenye mitandao ya habari ya kijamiipia zilionyesha wanajeshi wamekusanyika katika uwanja wa ndege.

chanzo bbc swahili

Hii kitu siipendi hata kidogo...inasemekana miongoni mwa waliotua huko Venezuela ni mkuu wa majeshi ya ardhini ya Russia...Lolote linaweza kutokea huko...Inaelekea Russia wameamua...
 
Ukiona Urusi ametia mguu mahali ujue malengo ya Marekani hayawezi kutimia. Malengo ya Marekani Syria ilikuwa ni kumwondoa rais Assad ili wapandikize kibaraka wao ili iwe rahisi wao kujivunia mafuta kwa kisingizio cha kurejesha gharama walizotumia "kuwakomboa" wananchi!! Mahali penye maslahi ya Urusi hapagusiki, kama vile Crimea!!!!
 
Nchi inashida ya misaada ya jamii ila wanapelekewa tani 35 za silaha na vifaa vyà kijeshi
National interests. Kwanza, Money: Russia has invested heavily in Venezuela and new administration might jeopard this. Mbili Geopolitics: Venezuela is almost at US doorstep. Kuwa na military base pale it cost a lot. Tatu: "shida ya kijamii " ya mrusi ni nini? Tusisikie story za nje tu. Nne: who said that this is for free? Maybe Venezuela will pay for this for the next 10 years. Who knows?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom