Ndani ya siku 20 tu, Mabasi 34 ya DART, yashapata ajali

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,486
Zaidi ya mabasi 34 katika mradi wa mabasi yanayoenda haraka yamepata ajali kwa kipindi cha siku 20 toka kuanza rasmi mradi huo kutokana na baadhi ya wananchi na madereva wa magari ya kawaida kutumia barabara maalum za mradi wa DART.
mabasi ya kwenda kasi.jpg
 
Madereva wabovu
Kuna mbwa mmoja kidogo anigonge wakati anaona taa zimemkataza kupita yeye akapita kwa lazima
Huyo mbwa bora afukuzwe kazi maana angenitoa roho bure wakati abiria wapo muda wote na hadaiwi hesabu
Namuombea ajifunze maana asipojifunza atakuja ua mtu bure kwa uzembe
 
Ajali 34 kwa siku 20 kwa mabasi 150+ ni kawaida sana kwa biashara ya mabasi ya abiria Dar. Waliowahi kufanya hii biashara wanajua ..
Mkuu niko huku niliko kuna mabsi kama hayo na yanapita njia moja na gari nyengine ila sijawahi kuona ajali ya hayo mabasi hata kama zipo ni kidogo, tatizo la tz ni Mifumo, sera na Mipango.
 
Mwanzoni kwenye majaribio, walianza kwa kufanya majaribio ya ndani kwa kuning'inia kwenye vyuma. Sasa hivi ndio wakati wa majaribio ya nje.... Tuendelee kufuatilia hadi mwisho wa hizo torture tests.
 
Zaidi ya mabasi 34 katika mradi wa mabasi yanayoenda haraka yamepata ajali kwa kipindi cha siku 20 toka kuanza rasmi mradi huo kutokana na baadhi ya wananchi na madereva wa magari ya kawaida kutumia barabara maalum za mradi wa DART.
Takwimu hizo zimetolewa na meneja uhusiani wa mabasi yao -UDART- Bwana Deus Gugaiwa baada ya kuibuka kwa ajali ya mara kwa mara ambapo amesema ajali hizo zimesababisha hasara ya zaidi ya shilingi milioni 94 kwa ajili ya ukarabati hali inayohatarisha uwezekano wa mradi huo kuwaendelevu.
Akielezea hatua zinazochukuliwa dhidi ya wanaoendelea kukiuka sheria, meneja uhusiano wa DART Bwana William Gatambi amesema Dart kwa kushirikiana na jeshi la polisi, wizara ya mambo ya ndani, Tanroad pamoja na jiji la Dar es Salaam wako katika hatua za mwisho za kutayarisha rasimu ya sheria ndogondongo zitakazo toa adhabu kwa wanaokaidi utaratibu wa matumizi sahihi ya miundombinu hiyo Dart.

Source ITV
 
Hapo kwenye kutayarisha sheria au akanuni kwa msukumo wa........ Kuna harufu mbaya.
 
Hii mwendo kasi ni nzuri inasaidia sana lkn wamejiona wao ni wababe wa barabara wanagonga hata watembea kwa mguu
 
Madereva wabovu
Kuna mbwa mmoja kidogo anigonge wakati anaona taa zimemkataza kupita yeye akapita kwa lazima
Huyo mbwa bora afukuzwe kazi maana angenitoa roho bure wakati abiria wapo muda wote na hadaiwi hesabu
Namuombea ajifunze maana asipojifunza atakuja ua mtu bure kwa uzembe
Matumizi ya lugha yameharibu hata maana ya hoja yako, wewe nawe uliwahi kuitwa "mbwa"?
 
Hawa madereva wa DART muda mwingine wawe wanatumia common sense sasa anaweza kuona hatari mbele yeye ataendelea tu kutembea speed kubwa kisa yuko njia yake... Mpaka mwaka uje kuisha yatakuwa screpa tu sijui hata kama vipuli vyake vinapatikana nchi hii
 
Kama leo kuna ist nusu tuigonge pale posta uhindini aliingia kwa makusudi ndan ya barabara ya mwendo kasi bahati nzuri jamaa wa udart alishika brake vzuri jamaa akafanikiwa pita salama...
 
Sijui wametumia vigezo gani katika kuajili, nazani ndio tatizo lilipoanzia.
Ila ndio yale yale ya kujuana , rushwa ndio tatizo linapoanzia sasa wanatafuta sababu, mwisho wataweka sharia kama za treni.
 
Gongweni tu hamfuati sheria
Mkuu tema mate chini IPO cku yako hivi unaweza dhubutu kusema hivyo umesahau Mara hii kauli iliyomponza kiongozi mkubwa hapa tz kwa kauli kama yako...yy alisema wapigwe tu...so jipange shetani asije akakugeuzia kibano.
 
Adhabu iwe kali na itolewe hadharani (ktk media) ili wananchi wawe makini.
Wana dsm tuna matatizo gani hatuelewi?
 
Baada ya miezi sita watapandisha nauli mpaka sh1000 kwa kisingizio cha uendeshaji ni gharama, kisa wanapigwa pasi ama wao wanawapiga pasi wengine
 
Back
Top Bottom