Ndani pachungu

Yeye ndio kawa Kama mwenye nyumba yan Mimi nifate anavyotaka akifanya kitu usiniulize ...ukimwachia hela ya matumiz usimuulize chenji ananuna hajibu nami nashinda kazin
Kwa tabia hiyo anaweza hata kukupindua kwa mumeo huyo na akampa tunda Mjomba..
 
Anatambua anachofanya ni kosa, anatambua unachokemea uko sawa, lakini bado anafanya hivyo, ni kwa sababu ana "inner conflicts" ndio maana anaonyesha "aggressive behaviour". ZUNGUMZA nae kistaarabu mkiwa peke yenu, ujue tatizo lake. Ukimya utamtenga zaidi
 
Ni vzru tukisikia pande zote mbili...inawezekana na wewe una mapungufu kibao tu...anyway hapo ni kwako tia heshima.
 
Mwache ndo anapevuka vizuri akikua ataacha
 
Njia pekee ni kumpeleka bweni...tofauti na hapo mtakosana tu na ndoa yako itakuwa changamoto.
 
Pole sana mkuu vipi ulishajaribu kutishia kuonfoka endapo mjomba ake anaendelea kumruhusu kufanya hayo kwako?
 
There is this Poem which mirrors exactly the societal differences we are undergoing, "A Freedom Song'" by Marjorie Oludhe Macgoye...............
"Since she’s my sister’s child
Atieno needs no pay
While she works my wife can sit,

Atieno’s sly and jealous
Bad example to the kids,

That girl stays too long at market
Who will teach her what is right?,

Atieno’s soon replaced
Meat and sugar more than all
She ate in such a narrow life
Were lavished in her funeral
Atieno’s gone to glory
Atieno yo."
 
Hii nlishakutana nayo nliletewa Mtoto wa ndugu yangu nikae nae wee akapata marafiki konki wale wa kinondoni watoto wadogo wa cheza chura wakapewa jina utumbo ndizi, nliwatimua hao mashoga bint kapiga simu kwa mama yake, naona nkimpigia simu mama yake hapokei, kumbe kamind.
Nikaona isiwe tabu nikaset ground rules zangu, jioni narudi nawakuta wamejazana sebuleni singeri sauti juu nikatimua.
Mtoto akamind namnyanyasa and the like ataondoka, kanunua akatoka imefika saa 2 usiku nafatwa na marafiki zake Mtoto ametekwa na kisu eti niwatume vijana wakamuokoe, vijana waliokuwepo wakataa, ikabidi sasa nisimame kama Shangai niwaamuru waende kumuokoa asije fanyiwa mabaya.
Mambo mengi ila mwisho nlimpaki kwa mama yake mpaka sasa mama yake hatupo karibu tunakutana tu kwenye issues ila hatupigiani simu wala nini.
Ndugu lawama nachokuambia wewe weka sheria zako azifate basi ukimchekea atakuharibia nyumba, nyumba ni ya mwanamke si mwanaume na Mtoto akiharibika lawama ni za mwanamke si mwanaume.
 
Kama anarudia mitihani huyo atakuwa ameshindikana mpotezee uzuri sio mwanao ila kwa hiyo ya kujifanya mwenye nyumba kazi unayo na mwezi wa kumi na moja utaona mbali hatari
 
Kuishi na Mtoto wa mtu Ni kazi.
Ningekuwa ndio Mimi ningemrudisha kwao..kukaa na Mtu mwenye kiburi siwezi.
Anataka kukaa Basi awe mpole,hawezi aondoke
 
Kwa mara ya kwanza naona watu wamekuja kutoa ushauri bila kejeli na masimango.
Hongereni sana πŸ‘ πŸ‘ πŸ‘
 
Pole Sana,kupangiwa nyumbani kwako ni kazi kweli.Kama kuna hosteli Karibu mlipie aende huko, Ila angekuwa kwangu bora lawama kuliko fedhea ningemtimua tuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…