Rugby Union
JF-Expert Member
- Nov 21, 2012
- 402
- 257
Ndanda FC imemfuta kazi kocha wake, Denis Kitambi. Uongozi wa klabu hiyo umechukua uamuzi huo baada ya vipigo viwili dhidi ya Mtibwa Sugar na kile cha nyumbani jana dhidi ya Ruvu Shooting.
Taarifa nyingine zimeeleza kuwa Kocha wa Makipa, Mohammed Mwarami Shilton naye ametimuliwa pia.
Imeelezwa kumekuwa na kikao cha dharura leo asubuhi na viongozi wamefikia uamuzi huo.
Juhudi za kuwapata viongozi wa Ndanda FC zimekuwa zikikwama kutokana na viongozi hao kutopokea simu. Lakini mchezaji mmoja wa Ndanda FC amelithibitisha hilo.
Tumeambiwa kuwa wamemtimua kocha, ila bado viongozi hawajafika kutueleza, alisema.
Chanzo: Kabumbu