NDALICHAKO MSIOGOPE SOMO LA HISABATI

NDALICHAKO MSIOGOPE SOMO LA HISABATI

neema shamuhenya

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
312
Reaction score
216
WAZIRI wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako amewataka wazazi nchini kuwahimiza watoto kusoma masomo ya sayansi ili kuongeza idadi ya wahandisi watakaofanya kazi katika sekta mbalimbali.

Akizungumza wakati wa kongamano la nne la wahandisi wanawake lililofanyika jijini Dar es Salaam, Profesa Ndalichako pia amewataka wanafunzi kutoogopa somo la hesabu kwa kuwa ndiyo msingi wa kufanya vizuri katika maeneo mengi ya kazi.

Amesema sekta ya uhandisi inafanya kazi kubwa katika kukuza uchumi kupitia miradi licha ya uwepo mdogo wa wahandisi katika fani hiyo hususani wanawake, jambo alilosema ni vyema likajengewa msukumo kuanzia ngazi ya wazazi.

“Wazazi mna jukumu kubwa la kuhakikisha watoto wanafanya vizuri katika masomo, hususani ya sayansi ili kuwawezesha kuwa wahandisi wazuri hapo baadaye, bila ushawishi wa wazazi katika eneo hilo bado tutaendelea kupata idadi ndogo wa wanafunzi wanaosoma sayansi,” amesema Profesa Ndalichako.

Amesema, Serikali kupitia wizara hiyo ya elimu inaendelea kufanya maboresho katika sekta ya elimu ikiwemo kuongeza vitabu vya sayansi na ujenzi wa maabara kwa lengo la kufanikisha mpango wa kuwapata wahitimu wa kutosha katika masomo ya sayansi.

Mwenyekiti wa Chama cha wahandisi wanawake Alice Isibika, mbali na kutaja mafanikio yaliyofikiwa na chama hicho tangu kuanzishwa kwake, alisema changamoto inayowakabili kuwa ni pamoja na idadi ndogo ya waandisi wanawake katika maeneo mbalimbali.

Alisema katika idadi ya wahadisi zaidi ya elfu ishirini waliosajiliwa na bodi ya wahandisi nchini(ERB),wanawake ni asilimia kumi pekee hatua aliyosema kuwa kwa kiasi kikubwa inadhohofisha nguvu za wanawake katika ujenzi wa Taifa.
 
Tatizo mtahala Wa masomo yakibongo it makes no sense we unakutana na topic MTU Wa chuo mwaka Wa 3 anaisoma we unasoma form 4 au form 6. Ni ujinga mtupu
 
Anaongea kama mwana siasa wakawaida, sio academician tena waziri mwenye dhamana....badala ya kutueleza mikakati ya kuhamasisha soma la hisabati na mbinu wizara yake alioweka kimkakati ili somo la hesabu lifaulike kwasababu limesha kua sugu, anasema wazazi waambie watoto wao wasome hisabati....anaongea kama mtu wakaida unadhani sio professor duh.
 
Yupo sahihi Hisabati ni somo rahisi kuliko masomo mengi ni vile watu wanatishana tuu...naliita somo mfu kwa maana Vector,Logic, calculus kanuni zake ni zile zile mpaka aina ya mifano aliosoma baba yangu nami nausoma mtoto wangu atausoma kufeli Hisabati ni kujitakia tuu...
 
WAZIRI wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako amewataka wazazi nchini kuwahimiza watoto kusoma masomo ya sayansi ili kuongeza idadi ya wahandisi watakaofanya kazi katika sekta mbalimbali.

Akizungumza wakati wa kongamano la nne la wahandisi wanawake lililofanyika jijini Dar es Salaam, Profesa Ndalichako pia amewataka wanafunzi kutoogopa somo la hesabu kwa kuwa ndiyo msingi wa kufanya vizuri katika maeneo mengi ya kazi.

Amesema sekta ya uhandisi inafanya kazi kubwa katika kukuza uchumi kupitia miradi licha ya uwepo mdogo wa wahandisi katika fani hiyo hususani wanawake, jambo alilosema ni vyema likajengewa msukumo kuanzia ngazi ya wazazi.

“Wazazi mna jukumu kubwa la kuhakikisha watoto wanafanya vizuri katika masomo, hususani ya sayansi ili kuwawezesha kuwa wahandisi wazuri hapo baadaye, bila ushawishi wa wazazi katika eneo hilo bado tutaendelea kupata idadi ndogo wa wanafunzi wanaosoma sayansi,” amesema Profesa Ndalichako.

Amesema, Serikali kupitia wizara hiyo ya elimu inaendelea kufanya maboresho katika sekta ya elimu ikiwemo kuongeza vitabu vya sayansi na ujenzi wa maabara kwa lengo la kufanikisha mpango wa kuwapata wahitimu wa kutosha katika masomo ya sayansi.

Mwenyekiti wa Chama cha wahandisi wanawake Alice Isibika, mbali na kutaja mafanikio yaliyofikiwa na chama hicho tangu kuanzishwa kwake, alisema changamoto inayowakabili kuwa ni pamoja na idadi ndogo ya waandisi wanawake katika maeneo mbalimbali.

Alisema katika idadi ya wahadisi zaidi ya elfu ishirini waliosajiliwa na bodi ya wahandisi nchini(ERB),wanawake ni asilimia kumi pekee hatua aliyosema kuwa kwa kiasi kikubwa inadhohofisha nguvu za wanawake katika ujenzi wa Taifa.
wewe ulipata ngapi somo la hisabati
 
Back
Top Bottom