Tangu kutolewa kwa matokeo ya wahitimu wa kidato cha nne 2012 kumekuwa na maoni mbalimbali ikiwa ni pamoja na kumtaka Katibu Mkuu Mtendaji wa NECTA, Ndalichako, ajiuzuru. Leo naomba wanaJF tulidadavue hili kwa kina. Kwani nionavyo mm huyu mama hana kosa lolote, wala hakuchangia hata chembe ktk kufeli kwa wanafunzi hao. Huyu ni muonjaji tu wa pishi lililoandaliwa na Kawambwa kupitia wizara anayoiongoza. Alipoonja katoa majibu kuwa pishi halijaiva. Ni jukumu letu watz kuwahoji wapishi kupitia mpishi mkuu Kawambwa kuwa kwanin kaipua pishi lisiloiva vema?
Ningelikuwa mm ndiyo Kawambwa siku nyingi sana ningekuwa nimeachia ngazi. Pengine Kawambwa anashindwa kufanya hivyo kwa sababu zifuatazo.
a) Atakuwa amemsaliti aliyemteua ( rais wa nchi) ambaye ametamka wazi kwenye hotuba yake ya mwisho wa mwezi wa 2 kuwa hajui sababu za kufeli F4. Sasa kama mkuu wa nchi hajui Kawambwa naye hawezi kujiuzulu kwa kuwa bila shaka naye atajifanya hajui?
b) Atakuwa amekisaliti chama chake. Ikumbukwe kuwa hizi social clubs ambazo zilibatizwa jina la sekondari za kata ilikuwa ni karata ya kisiasa ya CCM, ili kuonyesha kuwa wanakuza elimu nchini wakati wanajua kuwa shule hizo hazina KILA KITU cha kuzifanya ziitwe shule.
Hivyo Kawambwa kujiuzuru ktk mazingira kama hayo unahitajika moyo wa kishujaa kama wangu.
Hata hivyo, wazazi na jamii ya watz kwa ujumla hatukwepi lawama hizi hata kidogo. Tukubali kabisa kwamba kabla hatujamnyooshea Kawambwa ama mtu mwaingine tujinyooshee sisi wenyewe kwanza. Kwanini?
1.Mafataki ndiyo sisi wenyewe tunaowapotosha watoto wetu kingono. Unamlaumu Ndalichako?
2.Kwanin hatukuhoji na kuandamana wakati ule serikali inatuhimiza tupeleke watoto wetu, tena wasiojua kusoma na kuandika ktk majengo yaliyobatizwa majina ya sekondari? Tulitegemea matokeo yapi hapo? Unamlaumu Ndalichako?
Mtoto wako ana simu nzuri kama vile anafanya kazi ikulu. Humuulizi katoa wapi? Mwanao anarudi nyubani saa 4 usiku kila siku eti katoka tuisheni. Husituki tu? Mwanao anasuka nywele kama vile anakwenda kufanyiwa sendoff. Huoni? Kule vijijini mtoto kapanga uswazi, mazingira duni halafu na msosi ni wa kugongea. Atafaulu huyo? Mwano anaongea na simu usiku kucha na mabwana wenye umri mkubwa kuliko babake. Hamuoni? Mnamlaumu Ndalichako? Kuna watoto wanaingia ubia na makonda ili wapate unafuu wa nauli, mwishoe wanakuwa nyumba ndogo au kubwa ya konda. Hamlijui hilo?
Shule za mission hakuna ujinga kama huo. Mwanafunzi wa kike ama wa kiume wote wananyoa nywele, hakuna kumiliki simu shuleni, hairuhusiwi kuwa na nguo za nyumbani shuleni. Halafu wote boarding. Tunatafuta mchawi ktk hilo? Tunaunda na tume? Nipeni mimi hiyo hela. Nikisikia Ndalichako anatjwa kuhusika ktk kufeli f4 roho inaniuma, na ninapata hisia kuwa anatolewa kama kafara ili kulinda mapapa walio madarakani. Kawambwa umenisikia?
Acha porojo wewe,kama kweli tunaka wototo wetu wapte elimu bora ni lazima baraza la mitihani lote livunjwe na kuundwa tena katika mfumo ulio bora,pia wizara ya elimu ifumuliwe yote kuanzia waziri mpaka mfagizi,tutengeneze wizara ya elimu mpya, hii ni kwa dharura tu,suluhisho la kudumu ni kuvunja mfumo mzima wa serikali ya tanzania kuanzia raisi mpaka mfagizi,tujipange upya ili tijenge nchi yenye kueleweka
maana hivi sasa nchi hii inaongozwa na wanasiasa walioshindwa katika maisha ambao tunaweza kuwagawanya katika makundi makubwa matatu:
A.Kundi la wanasiasa walioshindwa katika elimu,kundi hili linaongozwa na wafuatao;
1.Freeman Mbowe
2.John Mnyika
3.Maji maarefu/Ngonyani
4.Suleimani Bungara(mbunge kilwa kusin-CUF)
5.Joseph Mbilinyi/sugu
B.Kundi la wasomi walioshindwa katika fani walizosomea.Kundi hili linaongozwa na wafuatao;
1.Prof.Lipumba
2.Padri Slaa
3.Prof.Muhongo
4.Dr.Kafumu
5.Prof.Magembe
C.Kundi la wafanyabiashara walioshindwa kuwanyonya zaidi watanzania wakiwa nje ya siasa.Kundi hili linaongozwa na wafuatao;
1.Rostam Azizi
2.Ndesamburo
3.Lowasa
4.Abood wa morogoro
5.Mohammed Dewji
6.Kinana katibu mkuu wa CCM
Kumbuka hao ni mifano tu,lakini kuna wengine wengi tu ambao unaweza kuwaongoza katika kila kundi.
Watu hawa ukiwaona na kuwasikiliza wanavyoongea na kutokwa na mapovu Bungeni na kwenye majukwaa ya siasa utazani wanitakia mema nchi hii kumbe wapo katika haraki za kutafuata neema za matumbo yao na familia zao baada ya kushindwa ndot zao katika maisha.
Sasa kama taifa linaongozwa na watu kama hawa tunategemea nini kama sio matokea mabaya kama haya,umasikini wa kutupwa,na kila njanga katika taifa hili