Ndala(Kandambili) na Bangili zatumika kusafirisha DAWA za kulevya

Hii kitu mbaya sana aliyeianzisha sijui ni nani........inamaliza watu balaa ni zaidi ya ukimwi
 
Hii ni balaaa!! Kweli kuna kazi yakupambana na madawa haya yakulevya. Mungu atusaidie. Hapa wamestukiwa watabuni mbi umpya.
 
samahan wakuu hivi haya madawa ya kulevya huwa yanatengenezwa vipi? mpaka kukamilika kwa matumizi? nisaidieni.
 
Duh!! Nimerudi baada ya kuidownload hii video!! Kwanza hongera zake kwa aliyechukua hii video japo sifahamu kama bado yuko hai endapo hawa jamaa watashuku na kufahamu ni nani aliyewachukua. Swali langu ni Je hawa waswahili wanaonekana na wanaokaribishwa (karibu kwenye mapambano) je hawafahamiki na sisi tuliomo humu Jamiiforum? Kuna mchangiaji hapa amesema "ngoja tuone Magufuri kama atashinda hii vita ya madawa!!! Jamani Magufuri ni binadamu kama wewe na endapo hatutamsaidia kupambana na hii biashara kamwe hawezi kushinda pekee yake. Mfano ni hii video ilitakiwa apelekewe Magufuri moja kwa moja. Duh hawa jamaa hawataki kushindwa.
 
Jamaa naona wameapa kupambana na Mukulu aisee.

Yaezekana wana viburi vya baadhi ya wakubwa kutoka juu.
 
Hivi na hii kesi hapa chini iliishia wapi wakuu?

Wapakistan 12 Wanaokabiliwa na Kesi ya Kusafirisha Dawa za Kulevya Wameomba Wapigwe Risasi
Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Apr 25, 2015.
Wapakistan 12 Wanaokabiliwa na Kesi ya Kusafirisha Dawa za Kulevya Wameomba Wapigwe Risasi Baada ya Kesi yao Kuzungushwa Kisutu ‪[/h]

  1. 1.jpg

    Raia 12 wa Iran na Pakistan wanaokabiliwa na kesi ya kukutwa na kuingiza nchini dawa za kulevya aina ya heroin kilo 200.5, zenye thamani ya sh. bilioni 9.02, wamelalamikia kucheleweshwa kwa kesi yao katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.
    Washtakiwa hao ni Kapteni Ayoub Mohamed, Buksh Mohamed, Fahiz Dauda, Khalid Ally, Abdul Somad, Saeed Sahury, Bashir Afraz, Morad Gwaram na Hazir Azad, wote raia wa Iran ambao walikamatwa kwenye Bahari ya Tanzania.

    Wengine ni Buksh Mohamed, Rahim Baksh na Abdul Bakashi kutoka Pakistan ambao wote ni wavuvi.

    Mbele ya Hakimu Mkazi, Janeth Kaluyenda, Wakili wa Serikali Janeth Kitali, alidai mahakamani hapo kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa.

    Baada ya maelezo hayo, mshtakiwa wa kwanza Ayoub ambaye alikuwa nahodha wa meli iliyokutwa na shehena ya dawa hizo, alidai bora wapigwe risasi wafe kuliko kucheleweshewa hukumu yao.

    Alisema kila wanapofikishwa mahakamani hapo, wanaambiwa upelelezi haujakamilika na muda unakwenda wakizidi kuteseka gerezani ambako mazingira yake si mazuri.

    Hata hivyo, Hakimu Kaluyenda aliahirisha shauri hilo hadi Mei 5, mwaka huu, kwa ajili ya kutajwa na washtakiwa hao walirudishwa rumande.

    Inadaiwa Februari 4, 2014, washtakiwa hao walikamatwa na dawa za kulevya aina ya heroin kilo 200.5, zikiwa na thamani ya sh. bilioni 9.2, wakizisafirisha kwa njia ya bahari.

    at 3:20 PM - Vijimambo
 
Duh!! Nimerudi baada ya kuidownload hii video!! Kwanza hongera zake kwa aliyechukua hii video japo sifahamu kama bado yuko hai endapo hawa jamaa watashuku na kufahamu ni nani aliyewachukua. Swali langu ni Je hawa waswahili wanaonekana na wanaokaribishwa (karibu kwenye mapambano) je hawafahamiki na sisi tuliomo humu Jamiiforum? Kuna mchangiaji hapa amesema "ngoja tuone Magufuri kama atashinda hii vita ya madawa!!! Jamani Magufuri ni binadamu kama wewe na endapo hatutamsaidia kupambana na hii biashara kamwe hawezi kushinda pekee yake. Mfano ni hii video ilitakiwa apelekewe Magufuri moja kwa moja. Duh hawa jamaa hawataki kushindwa.
Hawa jamaa kama utawasikiliza vizuri kwenye video hii, utawasikia wakitamka neno Afande! Nafikiri hawa ni maaskari wapo kazini.
 
OK sauti haisikiki vizuri. Sasa mbona wanaonekana kama hawataki imwagike chini hata kidogo wasipate hasara!?
 
Sauti ya Afande inasikika wakati wanamkaibisha huyo mwenzao kwenye dakika ya pili! Utasikia pia wanazungumza kisukuma" kinehe"! hawataki imwagike kwani ni ushahidi wa kupeleka mahakamani na mkemia mkuu wa serikali ili ijulikane kama ni dawa au unga wa sembe. Vilevile wanataka kupima wajue ni uzito kiasi gani ili iwe rahisi kwao kukadiria thamani ya huo mzigo! japo mimi sipo kwenye hilo jopo, lakini nafikiri hizo ndiyo sababu zao.
 
Duh!! Nimerudi baada ya kuidownload hii video!! Kwanza hongera zake kwa aliyechukua hii video japo sifahamu kama bado yuko hai endapo hawa jamaa watashuku na kufahamu ni nani aliyewachukua. Swali langu ni Je hawa waswahili wanaonekana na wanaokaribishwa (karibu kwenye mapambano) je hawafahamiki na sisi tuliomo humu Jamiiforum? Kuna mchangiaji hapa amesema "ngoja tuone Magufuri kama atashinda hii vita ya madawa!!! Jamani Magufuri ni binadamu kama wewe na endapo hatutamsaidia kupambana na hii biashara kamwe hawezi kushinda pekee yake. Mfano ni hii video ilitakiwa apelekewe Magufuri moja kwa moja. Duh hawa jamaa hawataki kushindwa.
Umefeli kinoma babu....hao makachero wamekamata nyeupe ndio wanaisekeleeee,,usipotoshe umma...Na hata hapo alipomwambia mwenzake karibu kwenye mapambano ni mapambano ya kutokomeza biashara ya madawa
 
Back
Top Bottom