Nchunga bado ngangari, Yanga haijapinduliwa na "wazee" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nchunga bado ngangari, Yanga haijapinduliwa na "wazee"

Discussion in 'Sports' started by KIM KARDASH, Apr 29, 2012.

 1. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #1
  Apr 29, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  NCHUNGA AUNGURUMA JANGWANI, AWAPASHA WAZEE, AMTIMUA SEIF MAGARI  [TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
  [TR]
  [TD="align: center"][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption, align: center"]Nchunga kushoto[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  MWENYEKITI wa Yanga, Wakili Lloyd Baharagu Nchunga amejibu mapigo ya Baraza la Wazee la klabu hiyo, waliotaka kuichukua timu kufuatia mgogoro unaoendelea klabuni.
  Lakini Nchunga amekataa ombi au taarifa ya kujiuzulu kwa Mjumbe wa Kamati ya Usajili na Kamati ya Mashindano, Abdallah Ahmed Bin Kleb, wakati huo huo akimkubalia Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Seif Ahmad Magari kuachia ngazi.
  Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari asubuhi ya leo, makao makuu ya klabu makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam, Wakili Nchunga alisema kwamba Kamati ya Utendaji katika kikao chake cha jana imekubali kujiuzulu kwa Seif, lakini imekataa kwa Bin Kleb.
  Aidha, kuhusu Wazee kuchukua timu, Nchunga alisema kweli alifanya nao kikao ana akawaambia atakuwa tayari kuwaachia timu waihudumie kwa mujibu wa Katiba, lakini kwanza lazima watoe vielelezo juu ya vyanzo vyao fedha ili ajue uhalali wake, wasije wakaiingiza klabu kwenye matatizo.
  Alisema anahofia wasije wakawa wanapata fedha kutoka kwa watu wenye kufanya biashara haramu ya dawa za kulevya- wakaiingiza Yanga kwenye matatizo.
  Nchunga alisema iwapo watamuhakikishia vyanzo halali vya mapato, kwa mujibu wa Katiba atawaachia jukumu la kuihudumia timu na si kuhodhi madaraka ya uongozi.
  Kwa kuwa Wazee walitaka kuanzia kazi kwenye mechi dhidi ya Simba Mei 5, mwaka huu, maana yake wao watahudumia timu, lakini mapato ya mechi watachukua akina Nchunga.
  Baada ya kuifunga JKT Oljoro 4-1 wiki hii, wachezaji wa Yanga walipewa mapumziko na jana walikusanyika tayari kuanza mazoezi, ingawa walikwama kwa sababu ya mvua.
  Mwenyekiti wa Yanga, Nchunga amesema timu sasa itaingia kambini kesho na kuanza mazoezi moja kwa moja chini ya makocha Fred Felix Minziro na Salvatory Edward, wakati huo akisikilizia Wazee kama watatekeleza masharti yake awakabidhi timu.
   
 2. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #2
  Apr 29, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Jamani tuweni wakweli. Hivi wale wazee wanavyoonekana kama wao ndiyo wanahitaji pesa hata ya kujikimu kuliko Yanga na wachezaji muwakabidhi timu? wale wazee nao wanafikiria tu mapato ya mechi na Simba na si vinginevyo. Kwani wanavyoonekana wao wenyewe ni wahitaji wa pesa.

  Poleni sana watani kwa haya yanayowakuta sasa.

  TELO.
   
 3. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #3
  Apr 29, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  wazee wanatumika tu pale,nchunga kawaambia ukweli,watoa vielelezo kuonyesha vyanzo vya mapato watakayotumia kuihudumia timu,bonge la mtego kawapa,ndio maana wanatapa tapa tu mpaka muda huu hawajawasilisha vielelezo.
   
 4. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #4
  Apr 30, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Huyu Jamaa Mjanja sana kamkatalia Bin Kleb kujiuzulu ksbb anajua angeondoka na Niyonzima
   
 5. RasJah

  RasJah JF-Expert Member

  #5
  Apr 30, 2012
  Joined: Nov 5, 2009
  Messages: 697
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Hizo sinema zen msije mkasusia kuleta timu tar 5.. ohoooo
   
 6. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #6
  Apr 30, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 934
  Trophy Points: 280
  Walishamgomboa yule dereva kule Arusha?
   
Loading...