Nchi za Kiafrika ziige (kwetu) katazo la Siasa kwa wasiochaguliwa!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,817
Nazishauri nchi za Kiafrika kama zinataka kuendelea na kuepukana na Siasa za kiharakati ambazo hazina nia ya kujenga bali kubomoa jamii, basi waige kutoka kwetu, hili katazo la watu wa vyama vya Upinzani ambao hawajachaguliwa au niseme kura zao hazikutosha kupewa dhamana, kufanya Siasa kipindi ambacho siyo cha Uchaguzi ni moja kati kati ya maamuzi ya Kiakili kuwahi kuchukuliwa nchini mwetu na Afrika kwa ujumla!

Kwamba, Wabunge waende kwenye majimbo yao na huko wafanye Siasa wanavyotaka kwani ndicho kilichowaingiza Bungeni, na kama kweli Wabunge wetu wangefwata huu utaratibu kama nchi tungepiga hatua sana, lkn hawataki wanataka wazunguke nchi nzima kupiga blah blah tena kwa Wananchi ambao hawajawachagua, sasa kwanini Tundu Lisu aende kwa mfano Mwanza na siyo Singida Mashariki walikomchagua? Au kwa nini Lowasa akafanye Kampeni za Kisiasa wkt hajachaguliwa na Wananchi?!

Big Up Serikali yetu kwa uamuzi wa akili kama huu!
 
Naona Lowassa na Tundu lissu wanakuchanganya hueleweki mbona huzungumzii wakuu wa mikoa na wilaya wanaotumika kisiasa wakati hawakuchaguliwa na wananchi.
 
Back
Top Bottom