kujiita Mtanzania maana yake wewe ni mtanganyika+mzanzibar,Tanzania ni muungano wa nchi mbili au ndoa ya nchi mbili(ikawa mwili mmoja) ndizo zikamzaa mtanzania,wazazi wangu wote wana asili ya Tanganyika hivyo mimi ni Mtanganyika ila sina ubaguzi,kujiita mtanganyika sio ishara ya ubaguzi,mbona mtu anajiita mzigua na anaoa mbondei.Tanganyika nakuita popote ulipo urudi,nimekumisi sana Baba,ingawa walikuzika ila Mungu amekufufua,ameeenii!!
!
!
na mimi ni mtanganyika pua
historia, nimesoma japo si sana inaonekana hukunielewa vizuri kwa vile post imekaakaa kaa shairi fulani hivi, laki my point is:
1. Tanganyika ni nchi iliyobuniwa na kubatizwa jina hilo na wakoloni
2. Tanzania ni nchi iliyobuniwa na kubatizwa jina hilo na wazalendo
3. mimi na wingine wenye umri usiofikia miaka 47, tumezaliwa Tanzania na sio Tanganyika
4. muungano ni kielelezo cha umoja wetu na licha ya mapungufu yake, ni bora kuliko kutengana
5. changamoto tuliyonayo ni kuondoa mapungufu yake, iwe ni kwa kuunda serikali moja, tatu au kubaki na mbili za sasa, vyovyote vile, muhimu tuondoe kero zinazohusiana na muungano
kilichotufanya tusindwe kuijenga Tanzania si muungano uliopo, bali masuala mengi tu tunayojadili hapa kila siku kama ufisadi nk. kwa hiyo hata tukiuvunja muungano, tutashindwa kuijenga Tanganyika pia kama hatutapambana na matatizo haya (ufisadi nk)
mimi sio mtanganyika,
sikuzaliwa Tanganyika,
maana ya neno Tanganyika, siijui,
Tanganyikailitoka wapi, sijui,
ilibatizwa jina na nani, sijui
nilizaliwa Tanzania,
nilizaliwa Afrika
nilizaliwa duniani
nlizaliwa na mwanadamu
kwa hiyo;
mimi ni mtanzania
mimi ni mwafrika
mimi ni mdunia
mimi ni mwanadamu
maana ya Tanzania, najua
maana ya Afrika, najua
maana ya Dunia, najua
maana ya mwandamu, najua
nawauliza wazanzibari,
nini maana ya Zanzibari,
nani aliipa jina Zanzibari,
kwa nini wajivunie uzanzibari?
kwa nini wasijivunie utanzania?
Hakika wewe ni mzalendo wa kweli sana , sasa ngoja nikutoe wasiwasi , Tanganyika IMERUDI RASMI .Nasikia mara ohhhh, wabara wanatuonea, wabara wanatudharau. Sisi si wabara, ni watanganyika bana!
Muungwana haachi asili. Nia yangu si kuanzisha thread ya kupinga muungano, bali sipendi kuitwa mbara na ndio maana ninasema sisi sio wabara, ni watanganyika.
Ukisema Tanganyika ni jina la kikoloni, basi kataa pia majina ya Tabora, Mwanza, Dar es salaam, Tanga na mengine mengi yanayopatikana katika ramani iliyochorwa na mkoloni.