Nchi yetu inahitaji ukombozi


Shayu

Shayu

Platinum Member
Joined
May 24, 2011
Messages
526
Likes
825
Points
180
Shayu

Shayu

Platinum Member
Joined May 24, 2011
526 825 180
Nchi yetu inahitaji watu watakao jitolea kwa dhati kwaajili ya ukombozi wa taifa letu, Vijana watakaosimama katika ukweli na kupigania haki na kulisimamisha taifa letu liwe imara, ili kulinda kizazi chetu dhidi ya mabeberu, Sisi kama taifa lazima tukue ,mimi naamini hatujawa taifa ili tuondoe umaskini tuu au tuondoe ujinga tuu bali tumekuwa taifa ili tutawale, Lakini hatutafikia huko hadi tupambane na ujinga na adui maradhi, jitihada zetu za pamoja zitatufikisha huko.

Ni jukumu la kila mmoja wetu kupiga vita ubinafsi unaogawa taifa letu. Ni jukumu la kila mmoja wetu kupinga mfumo unaoanza kujitokeza ndani ya taifa letu la baadhi ya jamii kujifanya wao ni first class citizen au wao watawala na kujiona wana haki zaidi ya wengine, hili ni taifa letu sote na jitihada zetu za pamoja pekee ndizo zitakazo nyanyua taifa hili. Viongozi lazima wajue hawawezi kujenga taifa hili pasipo nguvu za wananchi! Wakati umefika tupate kiongozi atakayewaambia vijana wa taifa hili ni nini majukumu yao kwa taifa, Sisi kama taifa lazima tuwe na malengo na dira, lazima tujue sisii ni watu wa namna gani na msimamo wetu ni upi na kwanini tuko pamoja kama taifa! Lazima kuwe na kitu kinachotuunganisha pamoja, katika dunia hii kila siku ni mapambano ni lazima tupambane ili tusimezwe na mataifa mengine ili tusiwe watumwa wa mataifa mengine.

Ni jukumu letu kila mtanzania mzalendo kuamua na kujenga roho ya uzalendo ndani yake na kujifunza kutokana na utumwa waliopitia mababu zetu. Lazima tujiulize ni nini tunajivunia kama taifa? ni kitu gani tunachoweza kusema mbele ya mataifa mengine na kujivunia ? wakati umefika kwa taifa hili kuacha kuendelea kuishi bila malengo, lazima tujitoleee nafsi zetu na maisha yetu kwa ajili ya ukombozi wa taifa hili. Mimi kila wakati naamini kama tutahangaika kwa pamoja, kama tutakuwa wazalendo kwa kulipenda taifa letu na kulitumikia tutafanikiwa, sijaona popote duniani watu walipokuwa na lugha moja na nia moja walifeli katika harakati zao, Ni lazima tufanye harakati za ukombozi wa taifa hili, lazima tutangaze vita, vita ya kulinyanyua taifa hili dhidi ya maadui aliosema mwalimu nyerere, kufikiria uvumbuzi na kuacha kuwa watu wa mizaha na kufuata mambo ya kijinga tuwe wamoja na tujenge taifa letu kwa nguvu moja.
 
N

NIMIMI

Senior Member
Joined
Apr 2, 2011
Messages
170
Likes
2
Points
33
N

NIMIMI

Senior Member
Joined Apr 2, 2011
170 2 33
Panga mashambulizi usiishie kuongea kama mtanzagiza.
 
Shayu

Shayu

Platinum Member
Joined
May 24, 2011
Messages
526
Likes
825
Points
180
Shayu

Shayu

Platinum Member
Joined May 24, 2011
526 825 180
Mimi siishii kuongea kwanza unanifahamu? ukinifahamu ndio utaongea kwamba mimi ni mtu wa kuongea tu bila mikakati au la!
 
Ringo Edmund

Ringo Edmund

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2010
Messages
4,893
Likes
39
Points
0
Ringo Edmund

Ringo Edmund

JF-Expert Member
Joined May 10, 2010
4,893 39 0
mkombozi ni nape na mwigulu.
 
Shayu

Shayu

Platinum Member
Joined
May 24, 2011
Messages
526
Likes
825
Points
180
Shayu

Shayu

Platinum Member
Joined May 24, 2011
526 825 180


Acha utani wewe unanitajia watu gani hao? acha masihara kwenye mambo ya msingi nape nae mtu? Sis tunahitaji wanaharakati halisi watakaokomboa taifa hili, Nape hana uwezo zaidi ya kuongea na kutafuta sifa tuuu.
 
Shayu

Shayu

Platinum Member
Joined
May 24, 2011
Messages
526
Likes
825
Points
180
Shayu

Shayu

Platinum Member
Joined May 24, 2011
526 825 180
umoja wetu ndio nguvu yetu
View attachment 37608

Acha utani wewe unanitajia watu gani hao? acha masihara kwenye mambo ya msingi nape nae mtu? Sis tunahitaji wanaharakati halisi watakaokomboa taifa hili, Nape hana uwezo zaidi ya kuongea na kutafuta sifa tuuu.
 
Ghost

Ghost

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2010
Messages
429
Likes
2
Points
0
Ghost

Ghost

JF-Expert Member
Joined Apr 20, 2010
429 2 0
Pamoja kiongozi....SALUTE!
Solidarity + Patriotism
A luta Continua...
 

Forum statistics

Threads 1,235,836
Members 474,742
Posts 29,237,727