G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,593
- 36,012
Utashangaa mbiombio waziri (aliyekuwa) Charles Kitwanga anaachishwa kazi ya uwaziri kwa tuhuma ya kulewa huku nyuma akikingiwa kifua kutokana na kashfa ya ufisadi. Huo tunauita uamuzi wa mashaka! Mimi kama mdau ninayeona mbali nimezipuuzilia mbali hatua hizi zilizochukuliwa na rais! Rais ameiacha sababu ya msingi kwa muda mrefu na kushikilia sababu inayotia mashaka makubwa tena ndani ya muda mfupi sana!
Hakika uchumi wetu nao ni tatizo kubwa kwa sasa. Hatuoni dalili yoyote ile ya kujikwamua hadi sasa. Tunawasikia wanasiasa wa CCM wale wa kutafuna na kupuliza wakituambia kuwa "tufunge mkanda" kwa muda! Hivi Anne Makinda anayepata kila kitu anaanzaje kumtia moyo yule ambaye hata chai hapati eti yeye na yule wote kwa pamoja wafunge mkanda kwa muda? Hii siyo sahihi hata kidogo! Ukitazama tu kwa macho unaona hali halisi ya nchi kiuchumi. Sukari tu imekuwa ajenda mpaka kuitoa jasho serikali, vipi kwa mambo makubwa?
Kisiasa nako ni kama tumeufunika moto kwa blanketi kule Zanzibar! Bado nina mashaka makubwa sana na hatima ya kule!