njeeseka
JF-Expert Member
- Oct 19, 2012
- 1,371
- 979
Niliwahi kukaa na dobi siku moja na kujifunza jinsi alivyokuwa ananyosha nguo, mmh nilishuhudia nguo nyingine ili inyooke ilibidi kunyunyizia tumaji maji maana bila hivyo kazi haifanikiwi.
Juhudi zinazoendelea za kuinyoosha nchi ili ipendeze sio rahisi na mikunjo mingine lazima maji kidogo halafu mkandamizo hasaa!
Nampongeza mhe na timu yake, nchi itapendeza nyoosha nyoosha baba!
Wapo wanaorudisha nyuma juhudi zote za kufanya nchi ipendeze, hao ndo mikunjo.
Wengi tuko nyuma yako na Mungu atakulinda kwa dhamira yako safi, hamna baya litakalokukuta!