Nchi yahamia Dodoma

MASSANGE

JF-Expert Member
Oct 17, 2014
207
195
Ngarambe ya kisiasa imehihamishia Nchi mjini Dodoma, Imeandikwa na Kiogo Mpina;

Hali ya joto la kisiasa linavyopanda,limepanda na watanzania wote wanashauku ya kutaka kujua ni nani Atakayechukua mikoba ya Jakaya kikwete kukimbiza kijiti kwa upande wa CCM.

Ni kama nchi nzima ipo hapa Dodoma, kwani Mh Rais Jakaya yupo, makamu wa Rais yupo, waziri mkuu anayemaliza muda wake pia yupo hapa, Baraza la mawaziri ambao baadhi pia ni Wagombe na wajumbe wa NEC ndani ya CCM wapo hapa pamoja na marais wastahafu na wazee mashuhuri waliowahi kuwa viongozi wa serikali katika awamu zilizopita nao wapo hapa mjini Dodoma.

Gumzo limekuwa sio dogo kwani watu mbalimbali na wanachama wa CCM wanasubiria kusikia ni nani atakayekuwa mwenyekiti ajaye.

Ni kweli Tanzania ni nchi ya kidemokrasia yenye vyama mbalimbali vya kisiasa ila Nguvu ya CCM bado inaonekana ndani ya nchi hii kupitia mchakato huu, unaoendelea hapa mjini Dodoma makao makuu ya nchi na chama pia vilevile.

Wengi wameelekeza maskio na macho yao hapa na kuna baadhi wamekuja kushuhudia
Ni mrithi yupi kati ya thelathini na nane (38) waliorudisha fomu,atakayekuwa mtetezi wa wananchi na mkombozi wao baadhi ya wakazi wa Dodoma wana maoni yao pia hali kadhalika pia na viongozi ndani ya chama.

Walitoa maoni yao. Juu ya watia nia ambao wanajitokeza midomoni mwa watu wengi hapa makao makuu ya nchi.

Miongoni mwao ni Naibu waziri sayansi na Teknolojia Mh January Makamba, waziri mkuu mstaafu aliyejiuzulu Edward Lowassa pamoja na jaji Agustino Ramadhani.

"Hivyo ni vyema zaidi kamati ikaangalia uwezo wa ziada katika watu waliomba nafasi hii, kama mtu hana uwezo wa kueleza maono yake basi hana jipya la kufanya. Huyo anatakiwa aachwe binafsi mimi katika watu wenye vision na mikakati mizuri nampa January makamba" Mjumbe mmoja ndani ya NEC ambaye hakupenda jina lake litajwe akitoa maoni yake.

Unajua ndani ya chama kuna ilani au sio lakini je rais ambaye sisi tunamtaka analo jambo jipya gani? Vilevile hata kuisimamia ilani ya chama kunahitaji uwezo binafsi na mipango ya kiongozi husika.

Hii nafasi nampa makamba anaweza pia ukiangalia ni kijana ataitendea haki hii nafasi kwasababu ana umri mdogo hatopenda kuwaangusha watanzania Pendo Tesha mhadhiri chuo kikuu Dodoma (UDOM )

CCM mwaka huu wakituopolea January makamba mimi ntamwaga kura zangu kwasababu gani ndugu mwandishi; ukimwangalia yeye na wagombea wengine hawa rika lake yeye ana kitu Tofauti kidogo yeye ana msimamo ,hakurupuki kujibu hoja yupo makini alafu masuala haya ya Kashfa za kijinga hana sijawahi kumskia. Mashaka wa eneo la Wajenzi Dodoma.

CCM ni chama Tawala ambacho kina kanuni na Taratibu zake za kupata wagombea wajumbe wanafahamu hilo, hapa Tuanatakiwa kufanya kwa umakini uchaguzi huu wa kuteua mgombea, tuteue mgombea anayeuzika na atakayelinda amani ya nchi yetu spika mstahafu,Mh Pius Msekwa akielezea maoni yake alipohojiwa na mwandishi wetu.

Katika maeneo mengine ambapo kuna mikusanyiko ya watu hapa na pale vijana wamekuwa wakibishana sana .

"hizi siasa ni za kidemokrasia bwana yule anayeshinda ndiye anayepewa nafasi ya kuongoza Mtu kama Lowassa watu wanamkubali sana sema wanachokiogopa ni mtandao alioujenga ni hatari " Issa Rashidi mwalimu wa sekondari Dodoma.

Kwa upande mwingine jina linalosikika pia na kutajwa ni Jaji Agustino Ramadhani.

"sisi tunahitaji kiongozi lakini naskia chama kina mgombea wao huyu ambaye ni yule jaji mstaafu sasa unafikiri huyu mtu ataenda kinyume na chama kwa sababu ameandaliwa na chama. hawezi kwenda kinyume" mashaka wa Area C ambaye kauli yake iliungwa mkono na wengi katika kijiwe chao cha kazi ni kazi.

Wakati huo huo hali ya Ulinzi na usalama imeendelea kuboreshwa katika. Kuzuia uwezekano wa kutokea vurugu zozote zile.

Ulinzi ni mkali katika kila maeneo vilevile mkuu wa Mkoa na kamanda wa polisi wametahadharisha mikusanyiko isiyokuwa ya lazima.

Ni vyema wakazi wa hapa baada ya shughuli zao za kawaida wakaenda majumbani kupumzika, kujiepusha na Kadhia yoyote inayoweza kutokea mkuu wa Mkoa Dodoma bibi chiku akizungumzaa na waandishi wa habari.

Imeandikwa na,
KIOGO MPINA,
Dodoma.
 
milioni milioni

JF-Expert Member
Mar 25, 2013
1,849
2,000
Naunga mkono hoja,ila hatuna waziri mkuu mstaafu aliyejiuzulu'tuna waziri mkuu aliyejiuzulu'napokea taarifa yako kwa mikono miwili.
 
kimbilimbi

Member
Jul 3, 2015
12
0
tunaitaji kiongozi mwenye upeo wa kuona mbali na mbinu za kutatua matatizo ya wananchi karata yangu naitupa kwa January anaupeo mkubwa sana
 
assuredly4

JF-Expert Member
Nov 7, 2011
1,216
1,250
MASSANGE

msilishwe maneno, mbona watanzania tuko kwenye mikoa yetu tunachapa kazi huko Dodoma hatupo wala hata hatuna habari nako

nchi haitajengwa na chama bali na kila mtanzania kuwajibika katika nafasi yake pasipo kuendekeza malalamiko yasiyo na tija
 
Last edited by a moderator:

Jay One

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
14,639
2,000
Si Lowassa ndio anapitishwa, ndio habari ya uhakika hiyo... chukua
 
kiluvya

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
1,331
2,000
Mh acha uongo mleta mada..mie nimeulizia ndugu zngu wote wapo sumbawanga hakuna hata mmoja aliyepo dodoma..mimi mwenyewe nipo namtumbo...siasa bwanaa ni shidaar lol
 
NGOSWE2

JF-Expert Member
Dec 19, 2013
368
250
msilishwe maneno, mbona watanzania tuko kwenye mikoa yetu tunachapa kazi huko Dodoma hatupo wala hata hatuna habari nako

nchi haitajengwa na chama bali na kila mtanzania kuwajibika katika nafasi yake pasipo kuendekeza malalamiko yasiyo na tija

Naunga mkono hoja. Anataka kutuambia tuliobaki mikoani sio WATANZANIA?
 
Bibititi1

JF-Expert Member
Sep 28, 2014
406
250
Ngarambe ya kisiasa imehihamishia Nchi mjini Dodoma, Imeandikwa na Kiogo Mpina;

Hali ya joto la kisiasa linavyopanda,limepanda na watanzania wote wanashauku ya kutaka kujua ni nani Atakayechukua mikoba ya Jakaya kikwete kukimbiza kijiti kwa upande wa CCM.

Ni kama nchi nzima ipo hapa Dodoma, kwani Mh Rais Jakaya yupo, makamu wa Rais yupo, waziri mkuu anayemaliza muda wake pia yupo hapa, Baraza la mawaziri ambao baadhi pia ni Wagombe na wajumbe wa NEC ndani ya CCM wapo hapa pamoja na marais wastahafu na wazee mashuhuri waliowahi kuwa viongozi wa serikali katika awamu zilizopita nao wapo hapa mjini Dodoma.

Gumzo limekuwa sio dogo kwani watu mbalimbali na wanachama wa CCM wanasubiria kusikia ni nani atakayekuwa mwenyekiti ajaye.

Ni kweli Tanzania ni nchi ya kidemokrasia yenye vyama mbalimbali vya kisiasa ila Nguvu ya CCM bado inaonekana ndani ya nchi hii kupitia mchakato huu, unaoendelea hapa mjini Dodoma makao makuu ya nchi na chama pia vilevile.

Wengi wameelekeza maskio na macho yao hapa na kuna baadhi wamekuja kushuhudia
Ni mrithi yupi kati ya thelathini na nane (38) waliorudisha fomu,atakayekuwa mtetezi wa wananchi na mkombozi wao baadhi ya wakazi wa Dodoma wana maoni yao pia hali kadhalika pia na viongozi ndani ya chama.

Walitoa maoni yao. Juu ya watia nia ambao wanajitokeza midomoni mwa watu wengi hapa makao makuu ya nchi.

Miongoni mwao ni Naibu waziri sayansi na Teknolojia Mh January Makamba, waziri mkuu mstaafu aliyejiuzulu Edward Lowassa pamoja na jaji Agustino Ramadhani.

"Hivyo ni vyema zaidi kamati ikaangalia uwezo wa ziada katika watu waliomba nafasi hii, kama mtu hana uwezo wa kueleza maono yake basi hana jipya la kufanya. Huyo anatakiwa aachwe binafsi mimi katika watu wenye vision na mikakati mizuri nampa January makamba" Mjumbe mmoja ndani ya NEC ambaye hakupenda jina lake litajwe akitoa maoni yake.

Unajua ndani ya chama kuna ilani au sio lakini je rais ambaye sisi tunamtaka analo jambo jipya gani? Vilevile hata kuisimamia ilani ya chama kunahitaji uwezo binafsi na mipango ya kiongozi husika.

Hii nafasi nampa makamba anaweza pia ukiangalia ni kijana ataitendea haki hii nafasi kwasababu ana umri mdogo hatopenda kuwaangusha watanzania Pendo Tesha mhadhiri chuo kikuu Dodoma (UDOM )

CCM mwaka huu wakituopolea January makamba mimi ntamwaga kura zangu kwasababu gani ndugu mwandishi; ukimwangalia yeye na wagombea wengine hawa rika lake yeye ana kitu Tofauti kidogo yeye ana msimamo ,hakurupuki kujibu hoja yupo makini alafu masuala haya ya Kashfa za kijinga hana sijawahi kumskia. Mashaka wa eneo la Wajenzi Dodoma.

CCM ni chama Tawala ambacho kina kanuni na Taratibu zake za kupata wagombea wajumbe wanafahamu hilo, hapa Tuanatakiwa kufanya kwa umakini uchaguzi huu wa kuteua mgombea, tuteue mgombea anayeuzika na atakayelinda amani ya nchi yetu spika mstahafu,Mh Pius Msekwa akielezea maoni yake alipohojiwa na mwandishi wetu.

Katika maeneo mengine ambapo kuna mikusanyiko ya watu hapa na pale vijana wamekuwa wakibishana sana .

"hizi siasa ni za kidemokrasia bwana yule anayeshinda ndiye anayepewa nafasi ya kuongoza Mtu kama Lowassa watu wanamkubali sana sema wanachokiogopa ni mtandao alioujenga ni hatari " Issa Rashidi mwalimu wa sekondari Dodoma.

Kwa upande mwingine jina linalosikika pia na kutajwa ni Jaji Agustino Ramadhani.

"sisi tunahitaji kiongozi lakini naskia chama kina mgombea wao huyu ambaye ni yule jaji mstaafu sasa unafikiri huyu mtu ataenda kinyume na chama kwa sababu ameandaliwa na chama. hawezi kwenda kinyume" mashaka wa Area C ambaye kauli yake iliungwa mkono na wengi katika kijiwe chao cha kazi ni kazi.

Wakati huo huo hali ya Ulinzi na usalama imeendelea kuboreshwa katika. Kuzuia uwezekano wa kutokea vurugu zozote zile.

Ulinzi ni mkali katika kila maeneo vilevile mkuu wa Mkoa na kamanda wa polisi wametahadharisha mikusanyiko isiyokuwa ya lazima.

Ni vyema wakazi wa hapa baada ya shughuli zao za kawaida wakaenda majumbani kupumzika, kujiepusha na Kadhia yoyote inayoweza kutokea mkuu wa Mkoa Dodoma bibi chiku akizungumzaa na waandishi wa habari.

Imeandikwa na,
KIOGO MPINA,
Dodoma.

kweli joto limepanda demokrasia inatabia ya kuonyesha ukweli na ukweli una tabia ya kujilipiza hata kama ukipuuzwa ipo siku utaonekana, vijana wapewe nafasi ni wakati wenu sasa tunakuombea kheir January makamba.
 
gnassingbe

JF-Expert Member
Jun 14, 2015
4,831
2,000
Not all those aspirant they deserve to be involved on threads

Mwandishi amefanya kazi kulingana na maoni ya watu.

kwa hiyo kwa maoni ya wengi ambayo hatujawekewa utafiti tuamini mzee wa kutuvusha hadeserve kuwa involved really? are sure?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom