Nchi ya wanoni

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,504
Reaction score
872,365
Wamenona kweli kweli, siha zao c haba, mutukari zao ni fii x fii 8, visim vyao ni kuanzia dolari mia 5, focha zao ni elfu kumi kumi, misosi yao ni uma na kisu na karatasi inaitwa tishu, usiniulize bei,
Shida zetu ndio kula yao, ndio kura yao, viwalo vyao wee acha tu havifuliwi na foma au mbuni ni dry cleaner
Ndio hawa wanaona kuwa kulipia laini ya Simu kwa mwezi buku wanaona ni ishu ndogo , wamesahau kuwa c wote wanaotumia simu wana kipato kama chao, wengine hawana kabisa. Kuna wanafunzi,wanachuo nk, kuna Sisi wa dajara la Chini ambazo kipato chetu ni mpaka tuuze karanga matunda mihogo vichwa vya kuku, makanyagio na viduchuri, tutamudu vp buku ya kulipia laini wakati muda mwingi tunaishi kwa kukopa muda wa maongezi?
Watutembelee waone tunavyoishi huku uswazi, mtu akinunua vocha ya buku anaulizwa kama ana msiba ,huku kwetu vocha ni 250 mpaka 500 basi hakuna mwenye uwezo wa kununua vocha ya buku 2 au tano njoni mwone,
Wanoni wa nchi hii msifikiri maisha muishiyo nyie ndio yetu sote,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…