NI KWELI KABISA....Watu wabishi walalamishi, hawataki kuzingatia kanuni, sharia na taratibu, mradi wa DART hawautaki mabasi yake yanagongwa kila siku, maeneo ya DART wamegeuza vijiwe na 'guest', jana walipinga ufisadi leo wanataka ufisadi, mbuga za wanyama zimemalizwa lakini majangili wakikamatwa wanasema haki za binadamu zimekiukwa, mawaziri wanakunywa na kulewa kazini mpaka bungeni, upinzani ajenda yao kususia vikao vya bunge lakini posho hawasusii na wananchi wanawaunga mkono, watumishi serikalini hawawezi kufanya kazi mpaka wasukumwe, watu wa form IV zero wanapata nafasi ya vyuo vikuu wakiondolewa wanatetewa na wananchi kwamba ni ukiukaji wa haki za binadamu, kiongozi akiwa mpole ameuza nchi akiwa mkali ni dikteta....