mwembemdogo
JF-Expert Member
- Feb 28, 2016
- 2,282
- 1,252
Inashangaza sana kuona Nchi Yetu Tanzania inaendeshwa Kwa kutegemea kodi za wananchi wake ambao hata mlo wa siku unawasumbua.Kodi zenyewe ni za bia, sigara soda saloon Na kina mama ntilie.Tanzania in nchi yenye Rasmali nyingi kuliko Kenya lakini Kenya waliishaacha kutegemea kodi za sigara via Na soda.Tanzania inawatoza wananchi Kodi ya kuingiza Magari Kwa gharama kubwa kuliko faida wanayopata Wajapani Kwa kuuza Magari.Wakati umefika Kwa viongozi wetu kuwa wabunifu kwani Raslimali tulizonazo za Mbuga za wanyama, Bandari zetu 3,Maziwa mabonde ya kilimo Tuvitumie kupata fedha badala ya kuwanyonya masikini wa nchi hii Kwa kodi.Kodi za wananchi zisiwetegemeo Bali ziwe nyongeza lakini Serikali sio iwanyonye wananchi wake Kwa kisingizio cha eti kodi zenu ndio maendeleo yenu.