Nchi ya Morocco imewa-prove wrong


Sasa kama tatizo sio lugha, mbona unakazania kulitatua kwa kutumia utatuzi wa lugha?
 

Sema sasa hilo tatizo lingine ni lipi.
 
Naomba kujifunza kutoka kwako:
Unaonaje masomo kama vile physics, chemistry, biology na sheria, unazani itatusaidia kupata wataalamu wa masomo hayo iwapo tutafundishwa kwa kiswahili.
 
Naona povu linawatoka kutukuza lugha ya mkoloni naona kuna watu wanajiaminisha bila kufundisha masomo kwa kiingereza tutafeli wakati si kweli Binafsi kwa hili naliunga kwa asilimia 100.
 
Naomba kujifunza kutoka kwako:
Unaonaje masomo kama vile physics, chemistry, biology na sheria, unazani itatusaidia kupata wataalamu wa masomo hayo iwapo tutafundishwa kwa kiswaahili.

China hayo masomo yote yanafundishwa kwa kichina na still wamepiga hatua kwenye hii inshu option zilikuwa mbili tu aidha kufundisha kwa kiingereza kuanzia vidudu mpk chuo kikuu au kutumia kiswahili kuanzia vidudu mpk chuo, nashukuru serikal imechagua moja maana ilikuwa mvurugano shule ya msingi miaka 7 unafundishwa kiswahili unaingia secondary unafundishwa kwa english.
 
Naomba kujifunza kutoka kwako:
Unaonaje masomo kama vile physics, chemistry, biology na sheria, unazani itatusaidia kupata wataalamu wa masomo hayo iwapo tutafundishwa kwa kiswaahili.

Sijakuelewa vizuri unachomaanisha kwenye hilo swali lako embu jaribu kufafanua vizuri kama ukiweza.
 
Kingereza hakikwepeki, hata Wafaransa wamelijua hilo na sasa wapo mbioni kubadilisha mfumo wao. Na hata hao Wamorocco wapo wengi wamekipokea Kingereza pakubwa BBC News - English speaking in Morocco on the increase


[h=1]French finally admit you must speak English to be a real leader[/h]
  • National School of Administration is making English fluency a requirement
  • From 2018 it will be a rule of entry for school producing French ruling class
  • Defies traditionalists including former French President Jacques Chirac
  • In 2006 he pledged to stop the spread of English language internationally
By PETER ALLEN FOR MAIL ON SUNDAY
PUBLISHED: 00:37 GMT, 15 February 2015 | UPDATED: 00:37 GMT, 15 February 2015

2.3kshares
1View comments​

For centuries France has held out against the dull language of 'les rosbifs' just across the Channel.
But now the country's future leaders have been told they must master English – a dramatic climbdown for a nation that has tried to ban words such as 'le weekend' from encroaching on its precious vocabulary.
ENA, the elite National School of Administration in Strasbourg, which produces the French governing class, is to make mastery of English a compulsory rule of entry from 2018.


+2



Nathalie Loiseau, director of the elite National School of Administration in Strasbourg, which produces the French governing class, has said the school will make mastery of English a compulsory rule of entry from 2018

An ENA spokeswoman said fluency in English was essential to run a modern state, and that potential students had to be prepared. The move is in defiance of traditionalists including former French President Jacques Chirac, who in 2006 pledged to stop the spread of English internationally.
[h=2]RELATED ARTICLES[/h]



[h=2]SHARE THIS ARTICLE[/h]Share



'We fight for our language,' said Mr Chirac, himself an ENA graduate, after walking out of a European Union summit when a French business chief spoke in English. 'I was profoundly shocked to see a Frenchman express himself in English,' said Mr Chirac. 'You cannot base a future world on just one language, just one culture. It would be a dramatic decline.'
Nathalie Loiseau, ENA's director, confirmed that the reform reflected a break with the past, saying French words are stuffy and outdated. 'The usual words such as 'sacrifice', 'vocation' and 'commitment' sound half religious, half military,' she said.


+2




The move is in defiance of traditionalists including former French President Jacques Chirac (pictured) who in 2006 pledged to stop the spread of English internationally



Read more: French finally admit you must speak English to be a real leader- | Daily Mail Online
Follow us: @MailOnline on Twitter | DailyMail on Facebook
 


Tatizo kubwa ulilonalo ninavyodhani ni kama walivyo wengi hata hamuelewi kinachongelewa nahisi!
Hakuna Mtu anayepinga ya kwamba Kiingereza SIYO muhimu, Kiingereza ndiyo lugha ya Dunia sasa hivi, kila mtu mwenye akili timamu analijua hilo, Kiingereza ndiyo lugha ya Sayansi na Utafiti Duniani, kila Mwanasayansi analijua hilo, Publications zote ukitaka zikubalike ni lazima uchapishe kwa Kiingereza kila Mtu analijua hilo!

Na ndio maana Raisi Kikwete au sera mpya ya Elimu ya TZ haijafuta Kiingereza bali inataka kufanya Kiingereza kibakie kufundishwa kama somo, na kama kikifundishwa vizuri kama wanafunzi na walimu wakipewa nyenzo za kutosha inatosha kabisa mtoto kuweza kumudu kutumia lugha ya kiingereza bila tatizo lolote lile, labda hatakuwa na lafudhi kama ya Mmrekani lakini ataweza kukitumia kiingereza pale anapokihitaji, lakini pale kisipohitajika basi Kiswahili ambacho ndiyo kinaeleweka na Watz wengi kitumike!

Kuna haja gani nesi wa Hospitali anakwenda kutibu wagonjwa wa Nzega alazimishwe asome kwa kiingereza? Kuna haja gani kijana wa Kitz anayetaka kusomea ufuundi magari VETA alazimishwe asome kila kitu kwa Kiingereza? Kuna haja gani ya Mtz anayefanya kazi kwenye counter ya benki ya kukufungulia na kukupa huduma za kibenki alazimishwe kusoma kwa Kiingereza?
 
Duuuuuu umeua! nimeshangaa mada yake kubwa inahusu lugha, point yake kubwa ya reference ni morroco. Hio morocco hajaweza kusema wanaongea lugha gani.


Poor you cc: limetumbuka

Hapa ni kujifariji mkuu,ukweli utabaki kwamba kuzungumza kiingereza fasaha ni gear ya kufanikiwa katika nyanja nyingi sana,kuanzia kwny uchumi,michezo,sanaa,siasa n.k katika dunia ya leo.Wafanyabiashara wakubwa,wakandarasi na wajasiriamali wakubwa wa Japan na China wanazungumza kiingereza vizuri tuu,the same applied kwa quatar,Dubai na India ili waweze kujenga International Business relationship na kuimprove Market share,

Rwanda nayo imeshift kutoka french na kuamua kuipa kipaumbele English.
 
Watanzania hata Kiswahili hawajui.

Wanatafuta mchawi wakati tatizo lao uchafu.

Hata wakibadilisha mambo kwenda Kiswahili watajikuta hawakijui.

Then what?

Tubadilishe kwenda kwenye lugha za makabila?

Hata lugha ya makabila watoto wengi wa sasa hawakijui...
 

Upo sahihi mkuu,
 

Nafikiri mimi na wewe tumebanana kwenye nyuzi kadhaa kuhusiana na hili jambo, ila naona hatufikii hitimisho. Msimamo wangu siku zote umekua kwamba lugha zote mbili ni muhimu kusoma kwa kuzitumia, yaani zikisaidiana. Teknolojia zetu zote zimeletwa na maelezo kuandikwa kwa Kingereza. Na inafahamika huwezi kuwa mahiri kwa lugha bila kuitumia katika mawasialiano. Lazima uongee japo kiduchu ili uzoee na kuitumia.

Nimekumbana na Watanzania waliofika fomu nne na wana matatizo kabisa kwenye lugha ya Kingereza, yaani mtu hadi SMS ya Mpesa iliyoandikwa kwa Kingereza inabidi anipe nimtafsirie. Nenda sasa hivi kwenye duka la dawa Dar, angalia chupa zote na satchet, maelekezo pamoja na side effects zote zimeelezwa kwa Kingereza.

Narejelea tena, lugha lazima uongee kiasi ili uwe na uwezo wa kuitumia, na ndio ni muhimu wahadhiri wawe wanafunza kwa lugha zote mbili, anaweza akatumia Kiswahili sana, lakini anasukumia na Kingereza ili kumzoesha mwanafunzi kusikia jinsi Kingereza hutumika katika maongezi.
 
Unachokosea ni kuniita muongo...hayo meingine yanayohusu vyuo vikuu na wageni kulazimishwa kusoma kikorea nakuachia mwenyewe na watunga sera wa korea. Mhimu ujue tu kuwa sera huwezi kuiingiza kwa pupa, mambo yanaenda kwa utaratibu...vijana wengi wanaokuja kuanza degree ya kwanza vyuo vingi nchini korea ya kusini wanapiga ung'eng'e hata mgeni kama mie wananisikiliza. Nafundisha power electronics full english, miaka 3 ~ 5 iliyopita vitu hivyo havikuwa rahisi hapa korea.
 



Ndio maana nasema haujanielewa na hilo tatizo la kutokuweza kutumia Kiingereza halipo TZ tu bali hata Kenya, Uganda, Malawi kwa kifupi Afrika yote inayojiita Anglophone liko na nimekumbana nalo sana tu wako watu wengi hata Nairobi kwenyewe wana shida kubwa sana na lugha ya Kiingereza, ninakuhakikishia watu wenye uwezo wa kutumia Kiingereza kwa ufasaha ndani ya Nairobi haupati 40% na hapo sijaongelea Kenya nzima ambayo inakwenda mpaka Turkana na sijui Machakosi, leo hii Raisi wa Kenya akisimama kuhutubia wananchi wa nchi yake ni chini ya asilimia 30% ya Wakenya ndiyo wanaweza kuelewa raisi wao anasema nini na hii ni pamoja na Watoto kusoma Kiingereza kitupu shuleni kwa zaidi ya Miaka 14!

Hivyo cha kuangalia hapa ni ubora wa elimu, Miaka ambayo Mtz au Mkenya anajifunza Kiingereza ni mingi mno lkn bado matumizi ya lugha hii bado ni ya maelite iwe Kenya, UG au Zambia hivyo basi kama ubora ukiboreshwa na Kiingereza kikafundishwa kwa ufasaha kama somo hakuna haja ya mtoto kusoma kiingereza kwa Miaka zaidi 10 ndiyo aweze kukitumia!

Angalia ni kwanini Mtz anaondoka ana kwenda kusoma Japani na akifika huko anafanya kozi ya kijapani kwa mwaka mmoja halafu anaanza kusomea digrii yake? Hili linawezekana vipi? Inawezekanaje Mtz au MK aende kusoma Urusi na atumie mwaka mmoja kujifunza Kirusi halafu aweze kusoma degree na kumaliza kwa kirusi? sasa ni kwanini kwenye kiingereza tunatumia miaka zaidi ya 10 lkn bado matokeo ni mabaya?

Hivyo basi utaona ya kwamba muda tunaotumia kujifunza kiingereza ni mwingi sana kwanza ukiniuliza mimi mtoto wa kikenya anakwenda shule kujifunza karibu Kiingereza tu na tungeweza kuutumia kujifunza mambo mengine ya maana mwaka mmoja unatosha kabisa kwa binadamu mwenye akili za wastani kujifunza lugha na kuitumia kwa umakini hivyo hakuna haja ya kusoma miaka 20 kiingereza halafu bado watu wana tatizo na hicho hicho kiingereza!

 

Nakuita Muongo kwa maana Korea Kusini Elimu ni ya Kikorea kuanzia chekechea mpaka Chuo Kikuu na kama kuna kozi ya kiingereza basi ni kozi maalumu hata shule za Kiingereza kwa maexpert zipo, lakini Lugha rasmi ya kufundishia Korea ni kikorea kuanzia chekechea mpaka Chuo Kikuu!

Wakorea kuongea kiingereza haimaanishi kwamba Elimu yao ni kiingereza, HAPANA wanaongea kiingereza kwa maana Kiingereza kama Somo limetiliwa mkazo na mpaka wana native speakers wanaofundisha Kiingereza au Wakorea wanaosomea kuwa walimu wa Kiingereza huwa mpaka wana programm ya kwenda kukaa mwaka mzima serikali inalipa kwenye nchi ya Kiingereza ili waweze kufundisha Kiingereza vizuri, lakini Kiingereza kinafundishwa kama somo tu na kwa kuwa kinafundishwa vizuri ndio maana watoto wanaweza kukiongea!
 
Kwa hiyo huoni kuwa hiyo ni transition stage ya kuja baadae kuhamia kwenye kiingereza?
 

DUH HUJANISHAWISHI BADO, INAMAANA YA (50) KWAKO IMEFANYA VIZURI?? NA APO BTN YA 4 NA YA 49 MBONA HAUJATAJA NI AKINA NANI?? NAAMINI HAPO NDO WAMEJAA WAONGEA KIZUNGU U WAMAANISHA NINI??
MM WADAU TAHMINI HII YATIA SHAKa
 
Kwa hiyo huoni kuwa hiyo ni transition stage ya kuja baadae kuhamia kwenye kiingereza?

Haitotokea kwa maana hakuna haja ya kufanya hivyo na hata siku moja hawawezi kukitosa kikorea kwa ajili ya kiingereza, na ndio maana wanafundisha kiingereza kama somo na kwa ufasaha ili kila anayefundishwa pia aweze kukitumia inapobidi, hivyo hata kama kesho lugha ya Dunia ikaja kuwa labda Kichina basi watafanya hivyo hivyo pia watafundisha Kichina kama Somo ila kwa ufasaha ili kila Mkorea aweze kukitumia Kichina lkn SIYO kubadilisha Kikorea kwenda Kichina hilo hawawezi kufanya!
 
DUH HUJANISHAWISHI BADO, INAMAANA YA (50) KWAKO IMEFANYA VIZURI?? NA APO BTN YA 4 NA YA 49 MBONA HAUJATAJA NI AKINA NANI?? NAAMINI HAPO NDO WAMEJAA WAONGEA KIZUNGU U WAMAANISHA NINI??
MM WADAU TAHMINI HII YATIA SHAKa

Usiwe mvivu pitia hiyo orodha tena kwa makini labda utaelewa, halafu hakuna lugha inayoitwa Kizungu!
 

Yale yale ya kuiga tembo kunya.

Unawezaje kufananisha China na Tanzania wakati populations za Beijing na Shanghai tu ni zaidi ya 90% population ya Tanzania?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…