Nchi ni Rais na msimamo

Super Brain

Member
Apr 17, 2016
45
38
Nianze kwa kuwapa pole TZ na pongezi pia katika hii transition period.

Nimesoma historia za mataifa mengi yaliyopiga hatua ghafla kama China,Japan,Russia(Urusi),Marekani,Cuba,Ujerumani,Italia,Korea nimegundua kuwa nchi ni raisi kwanza.

Rais akiwa na nguvu,msimamo usioyumba hakika bora tu awe na lengo zuri kwa taifa taifa huwa na njia nzuri ya kusonga tena haraka ili mradi asiyumbe,awe na msimamo thabiti.

Namsoma Mao,Hitler pamoja na udikteta wake vision Yake kubwa ilikuwa ni kufanya ujeruman liwe taifa la viwanda alifanikiwa kama Mussolini kuifanya Italy iwe taifa lenye nguvu.

Kilichowaponza ni ugomvi na tamaa za kutawala mataifa mengine wanavyotaka.

Bila Mao China haingekuwa pale hivyo kama wewe ni kiongozi Mkuu wa nchi ujue kuwa wewe ni dereva hivyo ukiwa na nguvu na mengine yatapata nguvu.

Unaweza ukawa na katiba nzuri lakini isiwasaidie.

Rais akishakuwa na vision hakuna mtu atakayekuzingua kwenye maswala ya msingi.

Ukibana watu wa juu wa chini watajiseti wenyewe.

Na mwisho wote watanywea kufanya upumbavu na nchi itakwenda.......
 
HUO NDIO UKWELI. BAHATI NZURI MAGUFULI KAISHASEMA HARUDI NYUMA KATIKA KUJENGA NIDHAMU YA UTENDAJI KAZI SERIKALINI.
 
Watanzania walizoea kubembelezwa sana sasa amekuja JPM mzee wa kutumbua wanaona si sawa sababu haendi kama walivyozoea. So far JPM yupo sawa na njia anazotumia kutumbua ni sahihi kabisa ila in the long run itabidi azipe taasisi meno ili zisimamie vyema

Nilisema nitakua mtu wa mwisho kuamini tunahitaji katiba mpya ili tupige hatua. Naamini tunahitaji kiongozi imara ili tupige hatua, katiba haijisimamii inasimamiwa.
 
Tatizo liko wapi tukiwa na katiba bora halafu na kiongozi imara.

Mleta mada ekuja na vioroza vya nchi chache sana ukasahau mifumo ya hizo nchi walijaribu kugandamiza sana wananchi wao lakina waliponadilika na kuimarisha demokrasia ndipo waliposonga mbele kwa kasi.

Kama sio demokrasia hata Magufuli asingepata huo urais.

Ni lazima pawe na Mifumo inayomfanya rais awe imara lakini pia afanye majukumu yake bila upendeleo .

Ni dhahiri Magufuli anakwama kwenye kuwawajibisha wanasiasa waliokua wanatoa maelekezo kwa watendaji wanaoitwa majipu leo.

Hakuna meneja au mkurugenzi wa bandari mwenye jeuri ya kufunga flow meter ya mafuta bila kupewa maelekezo toka kwa waziri na waziri amepokea toka ngazi za juu.

Hakuna kamishna wa TRA mwenye mamlaka ya kusamehe kodi ya mabilioni ya sh. Bila kupata maelekezo toka kwa waziri wa fedha.

Leo hii kuna mawaziri watatu wameshatuhumiwa kwa kukiuka maadili ya uongozi lakini Magufuli amewaacha na kukaa kimya kama vile hasikii. Ni rahisi kupambana na wale anaowateua lakini akumbuke pia wapo waliokua wanawasimamia.

Kikwete alithubutu kwa wakati tofauti kuwapeleka mawaziri mahakamani.
Kila zama na mbwembwe zake.

Tanzania na dunia kwa ujumla mfumo wa kidikteta hautawezekana tena.

Hii ncho ina makabila 125. Yote yalikua na mifumo yake ya utawala wa kichifu. Hakuna kabila lililofanikiwa kulitawala lingine bila mapambano makali kutokea na kushindikana kwa zoezi hilo.
Ndio maana wote tumebaki kama watani tu .

Kama kuna mtu anataka kuwadanganya watawala anakosea sana.

Kama Tanzania ingekua na kabila moja au mawili na moja lenye nguvu kulipiga lile dhaifu na kisha kulitawala kwa nguvu hapo ingekua rahisi kwa wale wanye nia ya udikteta kufanikisha azma yao.

Pia kuna dini tofauti zenye itikadi tofauti. Huyo dikteta atatoka dini gani ili asionekane kama anaupendeleo wa kidini?

Kuna mfumo wa vyama vingi hivyo suala la Rais dikteta ni gumu sana kwa nchi hii.

Rais kutimiza wajibu wake sio lazima awe dikteta.
Hivi kama Rais anajua wazi kwamba akifanya ujinga akiwa madarakani atakapotoka madarakani anasweswekwa ndani bila huruma atajituma tu kwa uadilifu.

Kama sheria inakukataza kula rushwa na TAKUKURU ipo huru hapo udikteta wa nini?

Bunge likitimiza wajibu wake wa kuisimamia serikali udikteta wa nini hapo?Mawaziri wakawa sio wabunge na kuliacha bunge liwe huru kuwabana watendaji wabovu kuna haja gani ya kumtwisha Rais mzigo wa udikteta peke yake?

Leo hii tunashangilia udikteta bila kujua kuwa rais dikteta ni lazima awatendee sawa watu wote bila kujali dini,kabila ,ukanda na uchama.

Dikteta kwenye vyama vingi atafanyaje kazi wakati anataka apendelee chama chake.

Udikteta ni kwa nchi yenye chama kimoja na kwa mtu aliyeingia madarakani kwa mtutu wa bunduki. Lakini tumchague mtu halafu ageuke awe mungu ni vigumu na ni kuota ndoto za mchana.

Magufuli ni kazi yake kuwafukuaza au kuwastaafisha wale wote wanaofanya vibaya kwa kufuata sheria zilizopo tu na sio lazima awe dikteta.

Ukiwa na sheria na katiba nzuri itaelekeza tu nani wa kutumbua nani wa kubaki na ukimuacha utaulizwa. Leo hii Magufuli akiacha majipu mengine yanayotuhumiwa hakuna mtu wa kumuuliza kwa sababu katiba imamlinda asiulizwe.

Mtu mmoja hawezi kuwa bora kuliko sheria na katiba zetu huku ni kulitukana taifa letu na katiba yetu aliyoapa kuilinda.
Katiba ndio kila kitu iwe ni hii iliyopo au nyingine hakuna mtu aliye bora kuliko katiba.
Katiba ndiyo inayomuongoza na sio ubora wake. Mapungufu yake yanaonekana kutokana na katiba kukosa nguvu ya kufanya baadhi ya mambo. Mfano kumchunguza rais aliyeondoka madarakani na kumshtaki ni vigumu. Sasa dikteta atawezaje kuongoza wakati hawezi kumshtaki rais aliyestafu kama taifa?
 
1000 digit hakuna taifa la ulaya ambalo hakijapitia udikteta ninachokisema ni kama wenzangu walivyonena kuwa katiba husimamiwa,kama kiongozi ni mbovu hata katiba iweje,lakini we unavyoona wananchi hitaji lao la msingi ni katiba kweli?Wananchi wanahitaji uwajibikaji na maendeleo katiba haina nguvu kama walivyokuwa na shauku ya kuona mafisadi wanawahibishwa uchumi upae hata marekani demokrasia ilikuwa baada ya maendeleo kupata mwamko Mkubwa hats France,Poland,Belgium, German,Italy na nchi nyinginezo
 
Baba dikteta pia mara nying huwa kinyume na katiba nashangaa unapouliza dikteta atawezaje kuwajibisha viongoz waliopoita wakat katiba hairuhusu?Ukishasema dikteta maanake nje ya demokrasia........
 
Tatizo takukuru nao ni wala Rushwa na viongozi wanazembea mpaka rais anatoka ikulu kwenda kumfuta mtu ajira ni upunguani wa wale waliopewa madaraka na raisi kuongoza wengine lakini bado wapo dhaifu
 
1000 digit hakuna taifa la ulaya ambalo hakijapitia udikteta ninachokisema ni kama wenzangu walivyonena kuwa katiba husimamiwa,kama kiongozi ni mbovu hata katiba iweje,lakini we unavyoona wananchi hitaji lao la msingi ni katiba kweli?Wananchi wanahitaji uwajibikaji na maendeleo katiba haina nguvu kama walivyokuwa na shauku ya kuona mafisadi wanawahibishwa uchumi upae hata marekani demokrasia ilikuwa baada ya maendeleo kupata mwamko Mkubwa hats France,Poland,Belgium, German,Italy na nchi nyinginezo
sawa jambo jema,ila magufuli kama raia na raisi alipe kodi!huo ndio uzalendo wetu!
 
1000 digit hakuna taifa la ulaya ambalo hakijapitia udikteta ninachokisema ni kama wenzangu walivyonena kuwa katiba husimamiwa,kama kiongozi ni mbovu hata katiba iweje,lakini we unavyoona wananchi hitaji lao la msingi ni katiba kweli?Wananchi wanahitaji uwajibikaji na maendeleo katiba haina nguvu kama walivyokuwa na shauku ya kuona mafisadi wanawahibishwa uchumi upae hata marekani demokrasia ilikuwa baada ya maendeleo kupata mwamko Mkubwa hats France,Poland,Belgium, German,Italy na nchi nyinginezo

Bandiko lako lilikuwa zuri sana, ila umeharibu ulipoanza kupuuza katiba na kudhani Rais anaweza kuwa malaika.
 
1000 digit hakuna taifa la ulaya ambalo hakijapitia udikteta ninachokisema ni kama wenzangu walivyonena kuwa katiba husimamiwa,kama kiongozi ni mbovu hata katiba iweje,lakini we unavyoona wananchi hitaji lao la msingi ni katiba kweli?Wananchi wanahitaji uwajibikaji na maendeleo katiba haina nguvu kama walivyokuwa na shauku ya kuona mafisadi wanawahibishwa uchumi upae hata marekani demokrasia ilikuwa baada ya maendeleo kupata mwamko Mkubwa hats France,Poland,Belgium, German,Italy na nchi nyinginezo

Kama udikteta ulikua bora kwa mataifa ya ulaya kwa nini wasiuendeleze?

Je ,baada ya mataifa ya ulaya kuacha udikteta walirudi nyuma au walisonga mbele zaidi kimaendeleo?

Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa yote lakini alipowatuma manabii wake na mtume wake aliwapa sheria za kusimamia. Hakuwaambia wawasimamie na kuwaongoza watu walivyokua wanataka wao kwa utashi wao. Sheria hizo ndizo zilizokuwa zinatumika kama katiba zao.
Na yeyote aliyezivunja aliadhibiwa vikali.

Ni ukweli na ni wazi kuwa CCM hawana nia ya dhati ya kuileta Tanzania mpya yenye nidhamu ya uongozi. Ndio maana hawataki kumpa Magufuli nguvu zaidi ya Kikatiba. CCM na unafiki ni kitu kimoja. Lengo la wanaCCM wengi ambao wametufikisha hapa sio zuri. Ni kama vile wanaambizana tumwache tu huyu bwanw mkubwa na na tumvumilie tu kwa Muda wa miaka kumi ataondoka na biashara itaendelee na yale waliyokuwa wameyaazimia kule Zanzibar.
Hata Nyerere alifanya vizuri lakini kwa sababu ya kutegemea Jeshi la mtu mmoja alipoondoka mrithi wake akaja na ngoma na wimbo anaoutaka yeye. Mambo yakawa tofauti sana na aliyoacha Mwalimu.Hakuna aliyekua na uwezo wa kuhoji zaidi ya mwalimu kupiga kelele bila kusikilizwa na watawala wakampuuzilia mbali.

Hata huo mfano wa wazi wa uimara wa Mwalimu Nyerere ulivyoshindwa kuendelezwa kutikana na udhaifu wa katiba bado tu hatujifunzi umuhimu wa katiba imara inayokata mbele na nyuma bila kumwonea au kumbeba mtu.

Ukiona mtu anamsifu Magufuli lakini hataki apewe torati kama Musa au Muhamad na sharia basi ujue hao ni majipu ya kudumu. Ndio maana hawataki Katiba yenye kumfanya kila mtanzania na taasisi kutumbua Majipu bila kumtwisha mtu mmoja mzigo.
 
Back
Top Bottom