Baada ya Sudan ya Kusini kujitenga kutoka main Sudan na kuongeza idadi za nchi katika bara la Afrika na duniani kwa ujumla, inaonekana inaweza kuwa chachu kwa baadhi ya majimbo ama nchi kumegeka,
inaweza kuongeza nguvu kwa nchi zilizokuwa kwenye maelekeo huo na pia inawweza kuwa chachu kwa nchi/majimbo mapya, baadhi ya majimbo na nchi hizo ni kama ifuatavyo
1)TAnzania
Kwa hali ya kisiasa na nchi kukosa mwelekeo wa kujua ni kipi cha kushika kwanza, kuna uwezekano mkubwa wa Zanzibar kutoka kwenye muungano,
Japokuwa muungano ulikuwa na kelele na kutokubaliana kwa baadhi ya Mambo lakini kulikuwa na uongozi Imara na CCM ilikuwa Bora, lakini kwa mwenendo wa CCM kwa sasa na nchi kukosa Kiranja wa kuweza kukemea mambo mazito ya Kifisadi ni wazi Zanzibar inaweza kuwa na sauti na haki ya kujioa kwenye muungano na kutengeneza nchi mpya katika Africa na Dunia kwa ujumla,
Nchi mpya zinaweza kuwa kama hivi
a) Tanganyika,
b) Jamuhuri ya Zanzibar (Pemba na Unguja)
c) Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Unguja
d) Jamuhuri ya Watu wa Pemba
e) Jamhuri ya watu wa Unguja
2) DRC
Ni miongoni mwa Nchi kubwa kabisa Barani Afrika na duniani
Tatizo kubwa la DRC ni Majimbo yaliyogawanjwa kwa minajili ya ukabila, Congo DR pana ukabila mkali kabisa, Baadhi ya Province za Congo zimeendelea sana na sababu zinazotoka kwenye province ambazo ziko nyuma kimaendeleo ni kuwa hizo zimeendelea kutokana na viongozi waliokuwa madarakani wametoka kwenye hizo province
Lakini ni kweli ukifika Province ya Katanga yenye Lubumbashi, Kolwezi, Likasi, Kalemie ni tofauti sana na Province ya Sud (South) Kivu yenye Uvira, Baraka, Fizi nk au province ya Nod (North) Kivu yenye Bukavu, Kamanyola nk
WAtu wa Katanga wameshaweka wazi kuwa Kabila kama hakupita kwenye uchaguzi wa mwaka huu basi Katanga Province itakuwa nchi, same time na watu wa province zingine nao wanataka wape independent, kwa minajili hiyo kuna uwezekano wa kuwa na zaidi ya nchi tano kutoka DRC (Time will tell)
3) Morocco
Polisario wamepigana kwa miaka mingi mno kutaka kutoka Morocco na kuwa na nchi yao ya Sahara Magharibi, haya mapinduzi ya nchi za kiarabu na kupatikana kwa uhuru wa Sudan ya kusini ambao walikuwa almost wanafanana kwenye kutafuta uhuru wao,inawatia Chachu kubwa kwa watu wa sahara Magaharibi, kuongeza nguvu zao za kudai Nchi "yao"
4) Somalia na SomaliLand nchi inayojiendesha yenyewe lakini bado haijajitangazia uhuru wake,
5) Baada ile issue ya Biafra Nigeria inaonekana kana kwamba bado wapo Pamoja, lakini muendelezo wa siasa za Kidini na Kikabila zinaonyesha wazi uwezekano wa nchi kumegeka
mitizamo yenu ni ipi wana JF
Zenj wajikate, wasituzingue wabara kwa kelele zao za taarabu. Waishie kuimba nyimbo zao huko za bata na samaki. Ngoja nitafute binti nioe kabla ya Ramadhani.
zenj kwani hakuwa nchi hapo zamani ??? Jee kiti chao katika UN walikiondoa wenyewe au kiliondolewa???
Kuwa na Jamhuri ya Pemba au Unguja nafikiri hizi ndio dhamira za kanisa itokee hivyo lakini kwa fikra zangu haiwezekani kwani wazenj wameamka na wanamuelewa adui yao
HIyo ya DRC ina ukweli na giza kidogo. Kwanza hakuna ukabila mkali, zaidi ya Ituri ambako kulikua na vita la ukabila. Kungine kupo sawa (nilifanya social study huko).
Pia Fizi, Uvira, Baraka, Bukavu vyote pipo south Kivu. Nord Kivu ni Goma Beni, Butembo etc na Maniema ni Kindu.
South Kivu na katanga kweli kuna discrepancy ya development level sababu mining ilianza Katanga enzi za ukoloni ila tofauti hiyo inaenda ikifutika sababu mining imeanza South Kivu pia (mostly gold, tin, cassiterite coltan etc).
Balcanisation (nchi kujigawa kama sudan) ni threat ipo kwenye nchi nyingi za Africa ila sio kitu rahisi kutekeleza sababu ya strong nationalist feelings. Leo ukiambiwa we sio mtanzania, ni mtanganyika, utasita sana kabla ya kukubali. Unless uoneshwe clearly mafaa ya balcanisation.
DRC imeamua kwenda pole pole toward federalism. Kwa leo kija jimbo lina governor, provincial assembly chaired by a speaker, a budget etc
Binafsi nadhani ni more sustainable solution.
Habari RR,
Kabla sijaanza ningeomba nikusahihishe kuwa hakuna Mining kubwa ianyofanya kazi Upende wa East Congo, uchimbaji uliopo ni wa wachoji tu, japo mining iko karibu kuanza maeneo ya Twangiza
Ni Kweli hakuna modern Mining ila kuna small scale mining kama Aurex, na zingine ndogo ndogo sizijui jina.
Sijuhi unazungumzia ukabila upi ambao hujauona DRC, Kivu ilikuwani province moja tu yenye Sud, Nod Kivu na Maniema (Manyema) na iligawanyika na kuwa Province Tatu na kila Province ikiwa na na dominant tribe (ndio maana nasema Province ziligawanywa kwa misingi ya kikabila).
Dhumuni ya Mobutu kugawa Kivu sio kwa sababu ya Kabila. Wakati wa Mobutu kulikua na sheria: you can only be a gover if you are not from the province. na it worked. Lengo ilikua ni experiment ya kuona kama smaller provinces zinaweza kua more governable. Na ilivo kubali kukawa na project ya kubadilisha katiba na kugawa Congo in 24 provinces (ambayo imekamilika in the new constitution)
South Kivu ina makabila makubwa mawili japo kuna mengine madogomadogo, kuanzia Makobora, Baraka, Fizi, Lubondja, Misisi Mpaka Lubichako huko kote wapo Wabembe ambao ndio baba wa Vita na Upande wa Kuanzia Uvira, Bukavu Mpaka Nord Kivu wapo wa-Bashi ambao hawaelewani vizuri na Wabembe. makabila mengine ni kama Waferero,Wavira,Warega, Wabwali nk\
Uvira sio washi, ni Wavira na Wafulero. Ubembe kuna wabembe na wabwari, Nord Kivu kuna wanya ruchuru na wanande. Kabila kubwa ya south Kivu ni warega na sio wabembe. Vita wanao pigana wabembe sio against makabila mengine, ni against FDLR na FARDC (armed groups from national and rwandese army) na FARDC wa fizi wengi ni wanyamulenge moving with their families.
Lakini Tatizo kubwa hapa lipo kwa Raisi Kabila na Kabila la Wanyamulenge(Watusti) ambao wapo kwa wingi Minembwe, Wabembe (Mayimayi) hawamkubali kabisa Raisi kabila, kwao kabila ni kama Mtusti na uwepo wa watusti Jeshini na kwenye sector nyingine wanaona ni kana kwamba ni Kabila ndio chanzo, Hivyo uchaguzi wa mwaka huu unatatizo kubwa sana, Iwapo kabila atashinda kuna uwezekano wa watu wa Sud Kivu kutomkubal na kuanzisha vurugu za kujitenga
Katanga kwenyewe kuna kabila nyingi. na wote wanajiunga kumsupport kabila not on the ground of kabila lake (mama yake is from MAniema) ila on the ground of fulfilled electoral promisses through Moise Katumbi who promotes the private sector.
South Kivu hawampendi kabila sio sababu he is not from south kivu (mbona last time walim-vote wakijua he is not?) ila ni sababu he did not realise the electoral promisses.
Watu wa Katanga chini ya Moise wanaajenda za chinichini za kutaka kujitenga iwapo Kabila Hatapita kwenye uchaguzi wa mwaka huu, na hizo siasa za kujitenga zilianza tangu miaka ya 60, Hofu hiyo imeingia Zaidi baada ya ya Wakasai chini ya Mkongwe wa siasa za DRC Tshekedi kuingia katika kinyanganyiro cha uraisi,
Wakasai hawana Tofauti na Wabembe katika kumpinga Kabila kuwa sio Mcongoman, na kuna kampeni kali sana kutoka kwa Wakasai walioko Lubumbashi (Katanga) za kusimamia na kuhakikisha Kabilahawi raisi,
Wakasai ndio kabila kubwa ya Congo na huwezi kuwalinganisha na wabembe who are merely a milliuon people. Na msingi wa kumpinga Kabila ni kuzisaidia mining companies in Katanga and not in Kasai. Na ndio maana recently alitoa 10 000 eti ya kuifufua Miba (Miniere des Bakwanga) a diamond company.
kwa Kabila pia akichaguliwa kuna wasiwasi wa Wakasai kutoka Kasai zote mbili kutaka kujitenga
Zaidi ya Katanga HAKUNA PROVINCE IMESHA TISHIA KUJITENGA> na katanga walianza in the 60's a movement called Cessecion Katangaise
Province zingine Bandundu, Kinshasa, Bacongo hazina kelele sana na ziko karibu sana kutokana kuwa zinasema LUgha moja Lingala na KIcongo
Zingine zote ambazo hujazitaja hapo zinaongea kiswahili. Aproximatively 40 000 000 of congolese speak Swahili making it the first swahili speaking country of the world. kutoongea lingala on a large and official scale haimaanishi hakuna umoja
Naona una ujuzi wa juu juu tu wa Congo, Naomba nikukosoe kidogo:
Nikirudi kwenye mada in genera nasema tena: federalism is a more sustainable solution for the COngo na Congo imeanza kuelekea federalism. Hatua ya kwanza ilikua kujaribu kugawa Kivu, it was succesfull. Hatua ya pili ni kmugawa provinces zingine. kila province inakua na executive yake (governor and ministers) na pia legislative (bunge). Mgao huu utaifanya serikali ya jimbo kua karibu zaidi na wanainchi na kuipa nafasi serikali ya federal level ku-focus kwa maswala ya defence na international relation (trade and diplomacy, state representation on international arena etc).
Hatua ya tatu itakua kuipa kila jimbo a judicial.
Republic Of South Tanganyika. (Lindi,Mtwara, Ruvuma) Yaja hiyo! Ngoja muziki wa gesi (Mnazi Bay) na Uranium (Tunduru na Namtumbo) na mafuta pwani ya miji ya Lindi na Mtwara. Patachimbika nasema kama naota leo.
Republic Of South Tanganyika. (Lindi,Mtwara, Ruvuma) Yaja hiyo! Ngoja muziki wa gesi (Mnazi Bay) na Uranium (Tunduru na Namtumbo) na mafuta pwani ya miji ya Lindi na Mtwara. Patachimbika nasema kama naota leo.
Mikoa ya Kusini ni bomu linalosubiri kulipuka. Rasilimali kibao zimeanza kuwatoa imani na utu Watawala wetu. Na mazowea ya uporaji na kutojali ni kichocheo cha ndoto ya wanakusini. Gesi toka Songosongo inawanufaisha watu wa mikoa mingine Gesi ya Mnazi Bay ikiunganishwa na ile ya Songosongo kuelekea Mwanza (rejea mipango ya NSSF kujenga bomba Mnazi Bay- Dar-Mwanza) itakuwa uamsho tosha kwa wenyeji wa huko. Tusubiri tuone!Nillishawahi kuweka thread inayozungumzia hili, niliandika taifa linalofuata baada ya Sudan ya kusini ni Tanzania ya Kusini. Waliniponda watu sana lakini mpaka sasa watu wa kusini wanahoji kwa nini gesi isafirishwe kwa mabomba mpaka Dar au Tanga??? Wao hawastahili maendeleo kama kanda zingine za nchi hii??!!!<br />
<br />
Wana uchungu hao maana mpaka bandari zao zimetelekezwa (Mtwara &Lindi)<br />
<br />
Kilimo ndo usiseme, korosho hamna kitu tena!!!