Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,599
- 46,244
USA, Canada, Russia, Brazili, China, Australia, India, Argentina ambazo ni nchi kubwa zaidi duniani na zilizopiga hatua kubwa za maendeleo zote zinatumia mfumo wa utawala wa majimbo kujiendesha.
Ni vigumu sana kwa nchi kubwa kama Tanzania kuweza kupata maendeleo ya haraka kwa mfumo wa uongozi centralised sana/ unitary kama tulio nao sasa. Sababu ni nyingi ikwemo
Hakuna uharaka wa kufanya maamuzi, maendeleo yanayahitaji uharaka kuamua mambo. Mfumo tulio nao sasa hautoi fursa hiyo. Jambo dogo linalopaswa kufanyiwa uamuzi ndani ya wiki moja linaweza hata kuchukua zaidi mwaka kwa sababu ya mlolongo mrefu wa uamuzi. Tumeshudia baadhi ya mambo yakisubiria hadi Rais afike mahali kuyatolea uamuzi. DEDs, RCs na DCs wanasubiria mambo yaamuliwe wizarani au na Rais au kusoma upepo ndipo watakeleze. Kwa nchi kubwa hivi tutuchakua hata miaka 200 ili kuleta maendeleo kwa mfumo huu
Vipaumbele tofauti vya maeneo na jamii tofauti za watu, kuna kanda au mikoa kipaumbele chao kikubwa ni miondombinu ya biashara, wengine ni kilimo, wengine ufugaji, wengine uvuvi n.k Kipaumbele ni muhimu sana kwenye jamii. Ukifanya mradi wa kujenga shule nchi nzima wakati kuna maeneo wanazo shule za kutosha na walihitaji barabara unakuwa umepoteza rasilimali tu, ukijenga uwanja wa ndege mahali watu wanahitaji kwanza maji masafi ya bomba unakuwa unatapanya rasilimali adimu tu. Hili ni tatizo kubwa sana kwenye unitary states ambazo ni kubwa.
Usimamizi dhaifu wa rasilimali, Mfumo wa unitary unazifanya rasilimali nyingi kuwa kama hazina mwenyewe japo zinasemwa ni za wote.Umilikaji wa rasilimali ni jambo muhimu sana katika kuzithamini, kuzitunza na kuzitumia kwa usahihi. Msitu unaosimiwa na jimbo utakuwa na uangalizi mzuri zaidi kuliko serikali central, watu wanaouuzunguka wataelewa huo msitu ni maisha yao na watoto hivyo wakiuharibu wao ndio watakuwa wachuma janga wa kwanza, vivyo hivyo kwa maziwa katika uvuvi, ardhi n.k
Muono tofauti wa mambo mengi ya kijamii.
Kuna jamii ziko conservative sana na zinataka kubaki na mtindo wake wa maisha wa muda mrefu, mila na tamaduni zake, nyingine ziko conservative kidogo na hazioni shida kuachana na mila na tamaduni zake nyingi. Unaweza kukuta waziri au mamlaka inajikita katika kutafuta vazi la taifa na kuna watu wanapenda hivyo ila wengine wao wanataka kuvaa suti au kanzu tu sasa hapo kunakuwa na mpishano mkubwa sana amabao ungeepukika kwa watu kufanya mambo kimajimbo.
Udhaifu katika uwajibikaji wa viongozi na kuwatuza viongozi. Udhaifu mkubwa wa mfumo centralised/unitary ni ugumu wa kumwajibisha kiongozi moja kwa moja. Leo hii mkuu wa mkoa au wilaya akiharibu lawama kubwa anatupiwa Rais au waziri, pia anaweza kuondolewa au asiondolewe. Pia mkuu wa mkoa,.wilaya au DED anayefanya vizuri anaweza kuondolewa kirahisi na wakati wowote. Katika mfumo wa utawala wa majimbo hayo mambo yanawekwa vizuri kwa sababu wananchi wenyewe ndio wanaamua nani anafaa kubaki, kuingia au kutoka.
Katiba mpya bila mfumo wa majimbo itakuwa sawa na kupata nusu mkate tu.