Nchi inayumba- ombwe la uongozi

Nchi inayumba- ombwe la uongozi

Joined
Feb 7, 2013
Posts
16
Reaction score
5
OMBWE
Tuzimulike asasi, za umma na binafsi,
Malengo yake asisi, tuanze kuyaasesi,
Hasa wetu maafisi, muhimu tuwadadisi,
Ombwe linaoneka, wakuliziba ni sisi

Akali tunaiona, kwenye zetu taasisi,
Kwenye viti wametuna, hasa waziba nafasi,
Wengi waliojazana, wanatia wasiwasi,
Ombwe linaonekana, wakuliziba ni sisi

Ukiwachunguza sana, hukikosi cha kuhisi,
Jinsi wanavyokazana, kwa malengo binafsi,
Vya umma kuvigawana, ajenda kutufirisi,
Ombwe linaonekana, wakuliziba ni sisi

Rajua wengi hawana, wamekosa akhlasi,
Huduma bora hakuna, japo kila mtu bosi,
Ule ubwana utwana, pia unashika kasi,
Ombwe linaonekana, wakuliziba ni sisi

Siyo siri tumekwama, weledi una nakisi,
Nchi inarudi nyuma, kwa kukosa ufanisi,
Nisemayo si shutuma, bali ni halihalisi,
Ombwe linaonekana, wakuliziba ni sisi
Wanazichota mapema, kisha wanatudhiaki,
Maisha kama kiama, wongo umetamalaki,
Kila kona ni dhuruma, maskini hana haki,
Ombwe linaonekana, wakuliziba ni sisi

Migogoro chungu nzima, siku moja haipiti,
Wafugaji wakulima, machweo ni hatihati,
Wale tuliowatuma, wamekosa mikakati,
Ombwe linaonekana, wakuliziba ni sisi

Tuna mali nchi nzima, faida hatuipati,
Zatitirika hujama, wachache wanadhibiti,
Tumebakizwa yatima, kundi limetusaliti,
Ombwe linaonekana, wakuliziba ni sisi

Kila mtu ameona, mengi yenye ukakasi,
Ni bora tukaungana, wenye nchi ndio sisi,
Yote yanawezekana, tuamkeni upesi,
Ombwe linaonekana, wakuliziba ni sisi

Emanuel. G. Someke
0753191035
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom