Nchi inaongozwa kimjini mjini.

Mwangaza

Senior Member
Feb 26, 2008
198
64
Wadau,

Wahenga hawakukosea waliposema utatambua matendo na moyo wa mtu kwa kauli zake, na mtoto wa nyoka ni nyoka. Kwa nasaha hizo za wahenga tunangalie kauli mbili tu za Ridhiwani Kikwete.
Kauli ya kwanza; “..Ndivyo nilivyolelewa na wazazi kuhusu namna ya kuishi".
Kauli ya pili ; "..mjini tunaishi kimjini si kila kitu unachomuona nacho mtu ni chake.."

Nijuavyo mimi;

Kuishi kimjini mjini ni kuishi kwa ujanja ujanja (yawezekana kwa shughuli halali au halamu), kuishi kwa kupeana kazi/dili/michongo kwa kujuana bila kujali ufanisi (hii ni mbaya inapoingizwa kwenye sekta za serikali/chama), na mambo yanayoenda na hayo.

Tafsiri ya nukuu;

Kama Baba kamlea mwana kuishi kimjini mjini hivi, Bila shaka Baba naye anaishi kimjini mjini vivyo hivyo.(maana kama mtoto wa nyoka ni nyoka,hata mzazi wa nyoka ni nyoka)

Rais anapoisha kimjini mjini;

1. Nchi inaongozwa kimjini mjini,
2. Uteuzi wa mawaziri,wakurugenzi,maRC,majaji,MaDC,wabunge na viongozi engine nao hufanywa kimjini mjini bila kuangalia sifa.
3. Mikataba ya kinyonyaji isiyojali maslahi ya Taifa inafanywa kimjini mjini
4. Mambo muhimu kwa Taifa mfano ishu ya katiba mpya yanafanywa kimjini mjini bila kujali mahitaji ya wananchi. Ushahidi ni Huu muswada wa katiba ulivyoandaliwa kimjini mjini ukizuisha masuala muhimi yasijadiliwe.

5. n.k n.k..(wadau mnaweza kuongezea 5,6,7...).

BINAFSI NAWEZA KUSEMA AHSANTE RIZ1 KWA KUTUFANYA TUMJUE ZAIDI JK NA KWA UNDANI NA ANAYOFANYA KIMJINI MJINI
 
Dogo anajifunza siasa,nadhani alikuwa katika harakati za kutaka kuaminisha umma kuwa pamoja na kuwa mtoto wa Rais bado maisha yake ni ya chini na ya kawaida kama vijana wa Mwananyamala,sinza na kwingineko (mjini mjini).

Isipokuwa linalonipa mashaka ni hili la yeye kuazimishwa magari ya kifahari na marafiki zake.Inaonyesha kama anaishi maisha ya kawaida (yaani ya kufikiri kesho nitakula nini?) sasa magari ya kifahari anayatakia nini toka kwa marafiki zake?.Kama si utoto basi atakuwa "anatamaa sana" na pengine hili ndilo linalotushawishi kuwa atakuwa ana "ukwasi" wa kueleweka na si "ukata" kama anavyodai.

Kinachomgharimu ni ujio wake wa kasi katika siasa usio pima marefu na mapana ya siasa.Marehemu Nyerere ana watoto tena wengi tu,mbali na matatizo yao binafsi hawakuwa na harakati za kujipendekeza kwa watoto wa matajiri au mafisadi kiasi hicho kama inavyofanywa na ridh1.

GARI ya thamani tena ya kuazima si bure!anayekuazima lazima tu atakuwa na interest maalum na wewe unayeazima lazima utakuwa na interest zako kama vile kuuza sura (kuonekana mtoto wa rais anapita bwana hasa madem).Hatushindani kwa ubora wa magari ndani ya siasa bali kuwatumikia watu.Iwapo siasa hawezi atoke si "UBISHOO" ambao sasa unamtafuna.

Hatuhitaji kujua anafika mara ngapi ikulu,au mara ngapi ameenda nje ya nchi,ila si amini kama yeye mtoto kipenzi cha Rais (baba) huwa anaishiwa mpaka anakopa kwa marafiki!!!!Bilashaka Ridh1 atakuwa mfujaji wa pesa tu kwani anachopata si sawa na mimi mtoto wa kabwela nisiye na nasaba yoyote ya kueleweka.
 
Toyota Cami yake anaendesha muda gani kama anaishi kimjinimjini na magari ya kifahari ya kuazima?
 
Back
Top Bottom