Nchi inaendeshwa na 'KITENGO'?

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Posts
49,320
Reaction score
117,611
Kuna vitu vinajitokeza kipindi hiki cha uchaguzi
ambavyo vinapaswa kuulizwa
je nikweli wananchi wa Tanzania ndio wasemaji wa mwisho wa masuala ya nchi hii?
au kuna watu kwa aakili zao na utashi wao wamejipa 'jukumu' hilo?

Kingunge alisema 'KITENGO' ndio kiliamua nani awe mgombea wa CCM na sio
wanachama......na Ukisoma gazeti la Raia Mwema wanasema watu wa 'usalama'
walimwambia Ngeleja awaambie wazanzibar kumchagua 'mgombea wa kitengo'
ndio akashinda....maswali yanajitokeza
1.kitengo kinaendeshwa na nani hasa?
2.Ni watu wangapi wanaofanya hayo maamuzi?
3.Ni kweli maamuzi yao yote ni kwa faidaya Taifa?
4.Wananchi wakipishana maamuzi na 'kitengo' maamuzi ya wananchi yataheshimiwa?
5.Nguvu ya 'kitengo' kwa tume ya uchaguzi ni halali?
6.kuna faida ya kushiriki uchaguzi huku 'kitengo' kimeshafanya maamuzi?
7.Je tuna demokrasia kweli au tunaruka ruka ttu na maigizo?

========
Some interesting comments:
 
The Boss Hata mimi nilishangazwa katika hiki kipindi cha demokrasia ya vyama vingi eti Usalama wa taifa wanaingia kwenye vikao vya ccm kumchambua mgombea atakayepeperusha bendera ya ccm.

Kama taifa bado kazi tunayo. Naamini mwaka huu 2015 wa uchaguzi, hautokuwa wa haki kama ulivyokuwa wa 2010
 


Na hakuna anaetaka kujadili hili
huu ni mwiko mkubwa demokrasia
 
Na hakuna anaetaka kujadili hili
huu ni mwiko mkubwa demokrasia

Hapo huwa nashindwa kuelewa, hata waandishi wa habari wanashindwa kuhoji na kuuliza maswali magumu. Utakuta mwandishi wa habari anauliza maswali huku akiogopa tena anauliza maswali ya kujipendekeza kwa kujichekeshachekesha. Huu Uhuni wa Usalama wa taifa kuingia kwenye vikao vya ccm utaisha lini? sasa hivi nchi haiongozwi na chama kimoja, ni demokrasia ya vyama vingi. Hiyo Taasisi iachwe ifanye kazi zake kwa ufanisi bila ya kuingiliwa na wanasiasa au kuingizwa na kugeuzwa kuwa kitengo cha upelelezi cha ccm.
We need to vocal TISS to be free
 


Waandishi wa kuaminika kama wa Raia Mwema wana ripoti tu hili bila kuuliza maswali
 
Kabisa Mkuu ni mwendo wa kihuni huni tu na kifisadi fisadi mwanzo mwisho.

Kikweli hilo linajulikana , huko katika Ikulu yetu kumejaa Wahuni na Majambazi, kuliko huku mitaani. Wezi wa Twiga na wanyama wetu, mikataba feki, kshfa za kuiba pesa zet na mambo kibao ya kihuni yanaanzia Ikulu.
 
Tangu kukatwa, niliona hili neno "kitengo" lilinifanya niwaze kidogo tu kwa siku hiyo ila leo maswali yanazidi kuwa mengi. Najiuliza pamoja na mambo mengine, hii nchi ni ya "kitengo" ama ya WATANZANIA??
 
Usalama wa taifa wana sub standards sana.
Wanaacha mambo muhimu ya nchi wanafanya siasa.
Hiko Kitengo kinatakiwa kijulikane ni kina nani hasa?
Wao ni kama nani watuamulie rais wa nchi?
 
Waandishi wa kuaminika kama wa Raia Mwema wana ripoti tu hili bila kuuliza maswali

Hilo pia ni tatizo, waandishi wetu wa tanzania hawajui kwenda deep na kufanya investigation ya habari, wanachofanya wao ni kukimbilia kuandika habari nusu nusu bila ya kwenda deep wakaja na habari kamili. Kwa kweli sasa hivi ccm imeshikilia kila sehemu muhimu ya hii nchi. Jeshini, usalama wa taifa Polisi na Magereza, hao wote wakistaafu wanapewa ukuu wa wilaya na mikoa, kama sio nafasi za ubalozi. walewale walioshindwa wana wa-recycle na kuwarudisha kwa njia nyingine. I know lots of Top military who think this country belong to ccm, wanajisahau kuwa nchi ni ya watanzania.

Wengi wananyemelea vyeo ccm
 
Tangu kukatwa, niliona hili neno "kitengo" lilinifanya niwaze kidogo tu kwa siku hiyo ila leo maswali yanazidi kuwa mengi. Najiuliza pamoja na mambo mengine, hii nchi ni ya "kitengo" ama ya WATANZANIA??

For now 'kitengo' ndo wenye final say
 
Usalama wa taifa wana sub standards sana.
Wanaacha mambo muhimu ya nchi wanafanya siasa.
Hiko Kitengo kinatakiwa kijulikane ni kina nani hasa?
Wao ni kama nani watuamulie rais wa nchi?


Hawajijui nafasi yao
badala ya kuwa 'loyal subject to the Republic'
wao nao ni loyal subjects to CCM......so shameful
 
Kwa hali ilivyo ni bora iwe hivyo kwa muda. . . . . . " kuna mambo labda hayahitaji mjadala na labda kuna mambo yakiwekwa wazi kabisa itahitajika nguvu kubwa zaid kutuliza jamii" hizi ni aasumptions ambazo zinaweza sababisha nchi kuelekezwa nini cha kufanya . . . . .

Naamini ni kwa faida ya wengi na ya muda mrefu. . .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…