ong'wafaza
JF-Expert Member
- Apr 30, 2012
- 262
- 115
Ndugu wana JF,
Kumekuwa na mtazamo kwamba nchi yetu imegubikwa na maovu mengi yakiwemo mambo ya ufisadi,biashara haramu na upigaji dili yakitamalaki miongoni wa wananchi na hata baadhi ya viongozi kwa muda wa miongo kadhaa.Na kwa mkutadha huu,nchi imepinda.
Mimi pia ni miongoni mwa wanaouona ukweli huu.
Kumekuwa na maoni mbalimbali miongoni mwa jamii kuhusu namna ya kujinasua na madhila haya kama nchi.
Baadhi ya wananchi wamekuwa wanapendekeza kuwa zitungwe sheria kali zitakazoweza kusaidia kuinyoosha nchi ikiwemo kubadili katiba ya nchi.
Wengine wamekwenda mbali zaidi wakisema kuwa pale nchi hii ilipofikia,na ili iweze kunyooshwa,panahitajika tupate kiongozi dictator .
Nadhani sasa ni wakati muafaka kwa sisi wanajamvi kutoa mchango wetu kupitia uzi huu ili tusaidie tumsaidie Mheshimiwa rais wetu katika jitahada za kuinyoosha nchi badala ya kubeza juhudi zake
Si vyema pia kwa sisi kama Wadau wa Serikali kukaa kimya bila kuchangia lolote.
Binafsi napendekeza tuanze na kutengeneza katiba ya nchi itakayokidhi na kutanzua matatizo yaliyotufikisha hapa kama nchi.
Kwa kuzingatia hili, uhuru wa kutoa maoni na kujieleza uwe mpana zaidi ili mradi sheria,kanuni na taratibu zetu tulizojiwekea zifuatwe.
Je,wewe una maoni gani?
Karibuni tuchangie kwa staha tusaidie kuinyoosha na hatimaye kuijenga nchi yetu.
Nawasilisha.