Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 40,314
- 72,740
Tumefika mahali pa kuacha Naibu Spika mteule anaikosesha nchi mjadala mpana wa budget kwa kiburi chake na hakuna mwenye busara wa kuliona hili?
Wabunge wa upinzani wameshtaki kuwa hawatendei haki hivyo akiwa anasimamia vikao hawataingia, lakini kinachotangazwa ni kuwa Wabunge wamegomea bunge.
Huo sio ukweli hata kidogo, kama kuna tatizo Wenyeviti wa Bunge wangeweza kuendesha vikao kama kawaida wakati huu Spika mwenyewe akiwa hayupo lakini la ajabu Naibu spika anang'ang'ania kila siku awepo ili watoke kwa makusudi mazima ambayo wenye busara wanashindwa kuliona hilo.
Kwa kauli zao za chini kwa chini (labda kuogopa kushughulikiwa) wa CCM wamekuwa wakilalamika kuwa kwa uwepo wao pekee hakuna cha maana kitakachorekebishwa katika budget hiyo.
Swali langu jee wale wazee na wengine wenye busara katika kushauri nchi hii kwenda katika misingi ya uhakika ya kusonga mbele wamepatwa na nini hadi kukaa pembeni na kumuacha mteule huyu wa Rais (ndio ukweli) akiharibu mfumo huu wa mihimili mitatu ya nchi kwa jeuri ya kugangamala lazima aongoze vikao?
Nina uhakika Ndugai angekuwepo asingeruhusu hilo liendelee kabla ya kuwekwa sawa.