Nchi iko vitani, Tanzania bila misaada ni bure | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nchi iko vitani, Tanzania bila misaada ni bure

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by gollocko, Feb 12, 2012.

 1. gollocko

  gollocko JF-Expert Member

  #1
  Feb 12, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 2,830
  Likes Received: 1,544
  Trophy Points: 280
  Nchi iko vitani, hivi ndivyo limeripoti leo gazeti la majira likimaanisha kuwa Tanzania hupata misaada kama nchi zilizovitani huku wabunge wakiikosoa serikali kwa jinsi inavyotumia misaada hiyo!

  Lakini hebu tujiulize hivi Tanzania bila misaada hatuwezi kufanya kitu chochote? Maana majengo na miundo mbinu yote mikubwa na muhimu ni kutokana na misaada mfano,asilimia 80 ya barabara zote nchini ni misaada, uwekezaji karibu wote kwenye kusambaza maji kwa wananchi ni misaada, uwekezaji katika nishati na madini ni misaada, reli ya Tazara,Uwanja wa Taifa,Ukumbi wa Bunge na mambo mengine mengi huwa ni misaada, hata bugeti ya nchi kwa mwaka asilimia 40 ni misaada!

  Hivi kweliI Tanzania hatuna uwezo wa kujiendesha wnyewe mpaka tutegemee misaada kwenye kila kitu?
   
 2. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #2
  Feb 12, 2012
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Misaada inamsaidia mheshimiwa rais kupata sababu ya kwenda kupiga misele nje ya nchi. Tukiiondoa atapata sababu gani tena ya kwenda nje? Si atazimia huyo!
   
 3. T

  TEMILUGODA JF-Expert Member

  #3
  Feb 12, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 1,367
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Hayo ndiyo madhara ya ukoloni mambosasa kwani utawala umejijengea ngao ya kulinda ULAFI,UROHO,UBINAFSI NA UCHOYO.BILA NGUVU YA UMMA Nchi itateketea kwani ni umma wenyewe utakao pima maendeleo pale ulipo kwa mfano maji,maji safi,barabara,umeme,elimu,afya,huduma za jamii nyinginezo,kilimo,madini,utalii,utawala bora,usalama,michezo,siasa safi na amani itokayo moyoni.KWA UCHACHE TU. NAWASILISHA.
   
 4. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #4
  Feb 12, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Nadhani hata hizi nchi zinazotupatia misaada zinachangia kwa kiasi kikubwa kutulemaza serikali inakuwa haijishughulishi kwa vile inajua mwisho wa siku kuna misaada ila isingekuwepo alternative ya msaada nadhani rasilimali na sources zote za mapato tungezitumia vizuri
   
 5. Hagga

  Hagga Member

  #5
  Feb 12, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Labda si lugha nzuri lakini nasikitika kusema kwamba tumekuwa na viongozi walevi, walevi wa madaraka mfano wa mfalme Luis XVI.Wafaransa walipogundua hilo walifanya lililositahili, mfalme na malkia waliondolewa na adhabu yao ilikuwa ni kukatwa vichwa.

  Miaka 50 iliyopita the Asian Tigers [Sngapore,Taiwan,Hong Kong na South Korea] hazikutofautiana sana na Tanzania.Leo hii wamepiga hatua kubwa mnno.Rasilimali zote zinatumika kwa ajili ya maendeleo ya nchi na watu wake,hakuna rushwa.

  Leo hii Tanzania imejaa wezi watupu, mtu wa kwanza kuwajibishwa ni raisi maana katiba inampa mamlaka makubwa kulinda rasilimali zetu ila yeye ndo mwizi namba moja akishirikiana na wezi mashuhuri wa ndani na nje ya nchi.

  Watawala wetu wakuu ni wezi, wajinga, wapumbafu na wenye ufinyu wa fikra.Sijutii kuyaandika haya maana ndo ukweli.
   
 6. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #6
  Feb 12, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,255
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Tanzania ikitaka kuheshimika iache kutegemea sana misaada, badala yake inatakiwa viongozi wafanye miundombinu ili tuweze kujitegemea zaidi. Kuna member mmoja siku moja alinifurahisha sana alisema kwenye mikutano ya kimataifa anaposimama Mtanzania kuzungumza ndio watu wanapata nafasi ya kwenda kuvuta fegi, hii yote inatokana na kudharauliwa sababu ya kutegemea sana misaada!
   
 7. gollocko

  gollocko JF-Expert Member

  #7
  Feb 12, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 2,830
  Likes Received: 1,544
  Trophy Points: 280
  Duh! Bro una hasira sana na hawa mfisadi
   
 8. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #8
  Feb 12, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Tanzania bil misaada inawezekana na kwa akili yangu there is no free gift or aid. Hivyo ndiyo maana tunawapa mali zetu bure kisha tunaendelea kuwapigia magoti kwa misaada kisha wanatudhalilisha kwa fedheha kabla ya kutupa misaada hiyo.

  Imefikia sehemu tuseme no misaada.
   
 9. The Mockingjay

  The Mockingjay JF-Expert Member

  #9
  Feb 12, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 380
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Inawezekana sana tu bila misaada na uchumi kupaa kama yafuatayo yatatekelezwa:

  1. Viongozi wakate mirija yote ya rushwa
  2. Watumishi serikalini wawe waaminifu kwa manufaa ya umma
  3. Serikali iache kuwa kikwazo kwa local SMEs kuwekeza
  4. SMEs zikishamiri zitachangia kodi la mapato biashara
  5. SME zikishamiri zitatengeneza ajira kwa vijana
  6. Serikari ikikusanya kodi kubwa ya mapato itaweza kuwalipa watumishi wake vema, kuimarisha miundombinu yake hata na wabunge kuongeza posho zao sababu uchumi utakuwa unasupport hayo matumizi

  Kwa kifupi, serikali inahitaji local SMEs more than ever now to cover wigo la misaada iliyopungua.
  Serikali isaidie SMEs ili zije ziwasaidie kwenye mapato.
   
 10. MGAWARIZIKI

  MGAWARIZIKI JF-Expert Member

  #10
  Feb 12, 2012
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 306
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hivi tufikirie wewe ni Baba mwenye nyumba unafamilia hutaki kujishughulisha unategemea misaada na hata ule msaada unaoupata badala ya kuutumia vizuri ukawa kama mtaji wakukutoa sehemu duni na kukupeleka sehemu yenye uhafadhali unautumia vibaya kwa kutegemea utapata msaada tena kesho je kesho ukinyimwa utakimbilia wapi? viongozi wetu hawana akili ya kujitegea hawaangalii future ni sawa na mtu ambaye amekula akashiba na kuamua kuchoma moto kienge cha chakula akitegemea njaa haitauma tena! badilikeni viongozi wetu jaribuni kujifunza kutoka kwa majirani nasikitika sana inaniuma sana wanaJF!
   
 11. February

  February Member

  #11
  Feb 12, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wengine hatujasoma hilo gazeti. Naomba upost tuchangie vizuri
   
 12. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #12
  Feb 12, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Post hiyo habari kama ilivyoripotiwa na gazeti ili tuchangie vizuri siyo kama ulivyoiweka sasa.
   
 13. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #13
  Feb 12, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Hizi tena ni porojo za weekend, haya bana vuta siku kwa kuangalia uchangiaji wa thread yako.
   
 14. mzurimie

  mzurimie JF-Expert Member

  #14
  Feb 12, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 6,151
  Likes Received: 1,604
  Trophy Points: 280
  misaada itaendelea kulisha viongozi
   
 15. N

  Naytsory JF-Expert Member

  #15
  Feb 12, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,593
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mkuu hivi nikiwa naihudumia familia yako na wewe utajiita baba mwenye nyumba? Au mimi ndiye baba wa hiyo familia. Hii ni katika jamii zetu na hata kwa taifa letu, baba yetu anakuwa omba omba halafu tunajisifia hivi tusipopimwa akili tumetendewa haki kweli? Napata aibu ndani ya Tanzania yenye rasilimali nyingi e Mwenyezi Mungu tuinulie viongozi watakaothamini UTU wa Mtanzania na kurudisha heshima Tanzania.
   
Loading...