Nchi hujengwa kwa ufisadi!?

  • Thread starter Sesten Zakazaka
  • Start date

S

Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2017
Messages
5,563
Likes
8,842
Points
280
S

Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Joined Sep 10, 2017
5,563 8,842 280
Ni maneno ya jamaa flani shabiki wa chama kimoja cha siasa kinachoshiriki katika chaguzi za marudio za udiwani bila kumtaja kama ni wa chama tawala au upinzani.

Nilikutana nae akiwa kavalia sare ya chama chake na mimi nilikua sijui kama ni mwanachama wa cha hicho, nikamtania kwa kumwambia 'ndugu yangu kumbe na wewe upo na mafisadi!' Jamaa wala hakupinga, na huku akitabasabu akanambia wewe hujui kua nchi inajengwa na mafisadi?
Angalia katika nchi yoyote ufisadi ukiachiwa kwa kiasi fulani panakua na furaha na uchumi wa mtu mmoja mmoja unainuka na watu wanakua na furaha! Inawezekana serikali isiwe vizuri sana kimapato lakini watu wananeemeka kutokana na mzunguuko wa pesa.
Akanambia hebu rudi nyuma ukumbuke kipindi cha ukamataji wahujumu uchumi miaka ya themanini hali za watu zilivyokua! Kukuta watoto wakitembea wamevaa kaptura matako nje ni jambo la kawaida, chakula, nguo na bidhaa muhimu ilikua shida kila kitu kwa foleni na rushwa, eti hadi alipokuja Mwinyi na kulegeza masharti ya biashara ndio watu wakapumua na kukazaliwa mafisadi waliotajirika wakati huo na kuibuka tabaka la wafanyabiashara wakubwa na wakati wenye exposure kubwa kimataifa
Akaniambia hata nchi zilizokua na ma marais wazalendo kupindukia wakati huo kama Burkinafaso chini ya Sankara Thomas ilikua imetopea kwenye umasikini uliobobea mpaka walipokuja viongozi waliolegeza kamba ufisadi ukatamalaki kidogo eti ndio maisha ya watu yakaanza kutononoka!
Akazidi kusema kuna wakati Zanzibar kipindi cha utawala wa Salmin Amour serikali ilikua haina pesa lakini wananchi wake walikua na furaha sana na ndio kipindi Zanzibar ilipojengwa kisawasawa na viwanda, mahoteli makubwa na hata vilabu vya soka vyenye nguvu vikiajiri wachezaji kutoka kote Afrika mashariki ndio viliibuka! Kwamba hata Dubai yenyewe imejengwa na mafisadi na ulaya pia ilijengwa wakati wa primitive accumulation of wealth ambao ni ufisadi tena wa kimataifa na baadae ikatokea mapinduzi ya viwanda baada ya kupata mitaji! Ila akatoa angalizo kua watu wafanye ufisadi hukooooo nje ya nchi walete hela ndani na mambo ya kuulizana umepata wapi eti yasiwepo!
Eti hata hawa jirani zetu Kenya wakati wa Mzee Jomo Kenyatta na wakati wa Baba Moi ufisadi ndio uliijenga Kenya na ikawa nchi ya viwanda na watu walikua na furaha sana

Sikukubaliana na jamaa yangu lakini kaniacha na tafakuri ya hali ya juu! Nyie mwaonaje wadau?
 

Forum statistics

Threads 1,237,195
Members 475,497
Posts 29,280,990