Nchi hii hatuna polisi (hali mbaya mpakani Mutukula)

Nchi hii hatuna polisi (hali mbaya mpakani Mutukula)

TRANQUILITIST

Member
Joined
Oct 28, 2012
Posts
84
Reaction score
35
Hali si shwari mpaka wa mutukula upande wa tanzania. Kuna vurugu kubwa zinaendelea hapa mpakan.
Mutukula ni mpaka kati ya tz na uganda. Vurugu hizo kati ya wananchi na uongozi wa halmashauri ya wilaya ya misenyi zimesababishwa na kitendo cha polisi kumkamata m/kiti wa mtaa kwa kile kilichodaiwa kuruhusu kujengwa kwa vibanda vcya wafanya biashara wadogowadogo eneo la stand.
Baada ya polisi kumweka pingu m/kiti huyo, wananchi wameandamana wakipinga hatua hiyo.
Wakijibu mapigo wameng`oa beria ya ushuru wa mazao na kuchoma moto kibanda cha kutozea ushuru huo.
Katika hatua nyingine wamebomoa madirisha na milango ya ofsi ya afsa mtendaji wa kijiji huku wakichoma bendera ya ccm iliyokuwa maeneo hayo.

Cha kushangaza polisi wamekuja kwa kuchelewa sana japo walipata taarifa mapema, hivo hawajasaidia chochote kwa sababu uharibifu ulishafanyika. Sijajua hali ya usalama ya mipaka yetu, lakini kama mipaka yote ipo hivi kiusalama, nchi hatuna.
Mfano mpaka huu na polisi wachache mno na mwanajeshi mmoja wa usalama wa mpaka. Naiomba serikali kudumisha ulinzi mipakani.
 
Tuna wala rushwa walio rasmi wanaovalia magwanda na kushika bunduki.
Jeshi limeoza kuanzia JUU HADI CHINI
 
Duh ni kweli mkuu hali ya mipaka ya hii nchi ni mbaya sana...askari wanachojua wao ni kupiga pesa tuu za magendo ila mambo mengine hawajui.......
 
ukiona majaji wenyewe ni vihiyo iweje hawa maaskari washika virungu?Tz hamna meritocracy katika kuajiri
 
Back
Top Bottom