Nchemba Nakukumbusha how you were so wrong about Arumeru East

AcinonyxJubatus

Senior Member
Nov 3, 2010
125
20
Niliahidi ikifika Jumatatu ya tarehe 2 April nitakukumbusha mataputapu uliyokua unatoa ukijitahidi kuaminisha uma kua sisiemu itashinda Arumeru Mashariki. Dogo nilikuambia hii sio Igunga, hapa watu sio masikini wakupembua ukweli.
Lusinde wako uliyefikiri anakusaidia yuko wapi.
Wana Arumeru wamekujibu kuwa Sera sio matusi, wameyakataa, Sera sio kugawa Bendera vitambaa na kofia, hayo pia sio mahitaji yao, Sere sio kuwarubuni na elfu tanotano wakati wanajua baada ya huu uchaguzi ukweli ni kwamba hamtawakumbuka. hiyo pia wamekukatalia.
Oooh Eti Arusha mjini hakuna maendeleo kisa mmemchagua Lema - Hiyo pia wameikataa.
Pole sana na mitazamo yako isiyo sahihi.
Ila nakukumbusha Tena, Tanzania ya leo imebadilika, watu hawadanganyiki. Ugua pole dogo.
 
Hahahahahaa! atakuwa hata mke wa mtu hakuambulia!
Pole bana, japo wewe ndo wanakuona jembe!
 
Huyu bwana mdogo alikiri kuwa wanatumia matusi badala ya hoja za msingi eti kwa sababu watu wameru ndo wanapenda kusikia matusi hayo.
Kauli hii ilikua ni fedheha kwa wameru.
CCM wameanza na matusi na sasa wanamaliza kwa matusi.
 
Huyu bwana mdogo alikiri kuwa wanatumia matusi badala ya hoja za msingi eti kwa sababu watu wameru ndo wanapenda kusikia matusi hayo.
Kauli hii ilikua ni fedheha kwa wameru.
CCM wameanza na matusi na sasa wanamaliza kwa matusi.

Ila mi naona kama vile walitumwa hawa jamaa. Maana siamini kama waliweza kuongea matusi kama yale ktk kampeni yenye upinzani kama ile.
 
Back
Top Bottom